Uncategorized

ALIYEFANYA MAUAJI YA FAMILIA YA MWANAMUZIKI JENNIFER HUDSON,AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.

By  | 
Mwaka 2008 ulikuwa mgumu kwa mwanamuziki wa nchini Marekani Jennifer Hudson.Tarehe 24 october alipoteza kaka yake,mama yake na mpwa wake ambao waliuwawa kwa kupigwa risasi.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambae jana alihukumiwa kifungo cha maisha anaitwa  William Belfour.Mtuhumiwa aliwahi kumuoa dada wa Jennifer anaeitwa Julia lakini walitengana kwa kutokuwa na maelewano mazuri.Katika ugomvi huo alimwambia ukiniacha mimi nitaiua familia yako yote halafu mwishoni nitakuua na wewe.
Mama wa mtuhumiwa akilia kwa uchungu baada ya mwanae kuhukumiwa kifungo cha maisha.
Jennifer akiwa na mama yake katikati ambae aliuwawa wakati dada mtu Julia mwenye nguo nyeupe akiwa ameondoka nyumbani kwenda kazini.Aliingia nyumbani na kumpiga risasi mama yao kwa nyuma mgongoni.

Na Kaka yake Jason Hudson aliuwawa kwa kupigwa  risasi  kichwani akiwa amelala kitandani.

Akaondoka na mtoto wa Julia anayeonekana pichani ambae mwili wake ulikuja kuonekana baada ya msako wa siku tatu.Alikutwa kwenye gari iliyotelekezwa akiwa amepigwa risasi kadhaaa kichwani.

Nyumba ya familia yake ikiwa imewekwa maua,misalaba na picha kama sehemu ya kumbukumbu ya mauaji ya familia hiyo.

8 Comments

 1. RUKY

  July 25, 2012 at 3:22 pm

  OMG DU.. IS THIS BECOUSE OF LOVE?????

 2. Anonymous

  July 25, 2012 at 7:27 pm

  Dina hii habari imeniumiza sna! Pamojatna hukumu aliyopewa bado haitarejesha thamani ya roho zilizopotea bila hatia! sasa kama huyo mtoto mdogo wa Julia alikuwa na kosa gani!? Hukumu ni juu ya Mungu

  Mama Careen

 3. Anonymous

  July 26, 2012 at 7:51 am

  May their soul rest in internal peace . Amen….

 4. Eunice

  July 27, 2012 at 9:18 am

  nimeumia sana kwakweli, na roho imeniuma zaidi nikimfikiria huyo mtoto mdogo ambaye hana hatia yoyote jamani, ni pigo kubwa liliwapata wanafamilia ambalo hawataweza kuliziba, mungu azilaze roho za marehemu pema peponi na awatie nguvu wafiwa maana hili jambo ni ngumu kusahau hata ikiwa ni baada ya miaka 10 ijayo

 5. Anonymous

  July 27, 2012 at 2:41 pm

  Ilitakiwa anyongwe mpaka kufa. Naishangaa hiyo mahakama. Watu wapoteze maisha halafu muuaji anafungwa maisha?! Mungu azilaze Roho za Marehemu mahali pema PEPONI.

 6. Anonymous

  July 28, 2012 at 12:21 pm

  cku hzi ukitongozwa shuti uombe na kadi ya clinic uone pale nomo au mana eeeeh hatari

 7. Anonymous

  July 29, 2012 at 5:14 pm

  mh kweli inasikitisha sana jamani na inauma…..

 8. Anonymous

  August 4, 2012 at 1:48 pm

  dina blog yako ni nzur sana m naipenda,unatupa habar nzur kwa kwel,endelea kuwa mbunifu kila ck

Leave a Reply