Uncategorized

MICHEZO YA OLIMPIKI YAANZA RASMI HUKO UINGEREZA

By  | 

Sherehe za uzinduzi Uingereza jana usiku zafana sana na kupata sifa.

 Jana usiku nilikuwa nimekodoa macho kweli kweli kufatilia ufunguzi wa michezo ya olimpiki 2012 uliofanyika nchini Uingereza.

 Na nilipenda vitu vingi sana japo vingine sikuvipenda pia

 Nilipenda sehemu ya Queen Elizabeth kuchukuliwa nyumbani mpaka uwanjani kwa Helcopter.

Akiwa chini ya ulinzi wa James Bond

Pia nilipenda sehemu aliyoonekana Mr.Bean akipiga kinandabaadae akaanza kusinzia na kuanza kuota
 David Beckam aliingia kuuleta mwenge wa olympic akiwa anaendesha boti zile ziendazo kasi
Baadae wana michezo mbali mbali wa nchi zote zinazoshiriki duniani ikiwemo tanzania walianza kuingi.Hapa nilishaanza kusinzia sikuweza kumalizia kwa kweli. 
 LEO hii michezo mbali mbali ikiwa imeanza

Moja ya michezo hiyo ni mashindano ya mbio za wanaume za baiskeli, gymnastics, kuogelea na basketboli.


Watu zaidi ya 15,000 walijitokeza na kushiriki kwenye tamasha la ufunguzi wa
michezo jana usiku.

Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, Jacques Rogge, alisema sherehe hiyo
ya ufunguzi ilionesha yote yaliyo mazuri katika ubunifu wa Uingereza.

3 Comments

 1. RUKY

  July 28, 2012 at 5:18 pm

  YAP UMEJIONEA WATANZANIA TULIVYOTIA AIBU..KWELI HATUKUWA NA WANAMICHOZO WAKUWAKILISHA MPAKA WAKAJIWEKEE MIZEE NA MITUMBO YAO NA MASUTI YAO UTADHANIA WALIKUWA WANAKWENDA OFISINI.. NILIICHUKIA KWELI NDIYO MAANA SEHEMU YAO IMEPITISHWA BILA MAELEZO NA FASTA..NADHANI HAWKUJIPANGA KABISAA..

 2. Anonymous

  July 28, 2012 at 6:58 pm

  lots of money has bn spent aisee..duuuh! Wametisha

 3. Anonymous

  July 30, 2012 at 7:22 am

  unajishushia hadhi kutangaza blog ya DIVA, ni maoni tu

Leave a Reply