Uncategorized

MITUNGI MIZURI YA KUPANDIA MAUA

By  | 
Katika maeneo mengi ya miji ni kawaida kukutana na mitungi ya maua mizuri kama hii au zaidi ya hii.

 Vyungu hivi vina tengenezwa kwa kutumia cement,udongo,mchanga na nyavu fulani.Bei ya vyungu inategemea na chungu.Kidogo elfu kumi mpaka elfu tisini kwa kikubwa.

Ukitaka wanyama ambao ni pundamilia,swala,simba bei ni maelewano.Wateja wao wakubwa ni wapita njia wanaovutiwa na wanachokiona.
Hapa ni eneo la kawe barabarani  kwenye mradi wa bwana Zadocky mwenye tshirt nyeupe.
Ukipata  vyungu vyako na maua yako inakuwa safi.Pichani ni kijana Mody wa mtongani lakini shughuli yake kubwa ni upandaji wa maua hapo hapo kawe.
Maua ya aina mbali mbali hayo madogo madogo yanaitwa boda boda.
Maua haya yanaitwa Julanta

1 Comment

  1. Anonymous

    April 29, 2017 at 12:18 pm

    Asante dada Dina! Mimi ninapenda sana maua. Natafuta Rose flowers. Je, zinapatikana wapi? Asante

Leave a Reply