Uncategorized

WALE WA DIET MNAENDELEAJE?

By  | 
Imeshapita wiki sasa toka tuanze ile diet yetu ya mwezi mzima.Diet yetu ni ya juice kwa wingi,maji kwa wingi na mboga mboga.Nilipata ujumbe kwa dada aliyeomba tusaidiane kupeana tips za namna ya kutengeneza juice mbali mbali.Mie natoa kadhaa na kama unazo na wewe tuandikie hapa kwenye maoni.
 Ikumbukwe kuwa juice yetu lazima iwe nzito na isiwe na sukari.Hapa ntakutajia aina za matunda utakazochanganya na kupata cocktail saaafiii.
1.Nanasi na carot unapata juice nzuri na
2.Tikiti maji na ndizi
3.Pesheni na parachichi
4.Embe na limao
5.Embe na nanasi
6.Embe,chungwa na pesheni.
 Zile siku zetu za samaki kumbuka ni samaki choma au wa kuchemsha.
Kuku pia wa kuchemsha au kuchoma.Kumbuka kunywa maji mengi sana angalau hata lita 2.

Mazoezi kama kawa ni muhimu hata kwa dk 30

Kuna hii gym inaitwa AZURA nitaanza kufanya mazoezi hapo siku chache zijazo.Nimeongea na uongozi wa hapo na tumekubaliana nao mambo kadhaa.Nitatoa nafasi tatu kwa wadau wangu humu za kufanya mazoezi bure mpaka utakapo fikia malengo yako.Ni gym nzuri ya kisasa na ipo ufukweni mwa bahari maeneo ya  Kawe.Tutafanya mazoezi pamoja mimi na wewe tukiwa chini ya uangalizi wao ili tupate matokeo mazuri.Tutapima afya kama kuna kisukari,blood pressure na kupewa ushauri katika maswala ya chakula.

Haya basi endelea kutembelea hapa ili upate kujua namna ya kushiriki na kushinda nafasi hii adimu na ya kipekee.

27 Comments

 1. Anonymous

  July 31, 2012 at 1:59 pm

  Mambo dina kuna wallet,kadi ya bank,kitambulisho na kanga,simu

 2. Anonymous

  July 31, 2012 at 2:12 pm

  VERY GOOD.

  John Maembe

 3. Sa

  July 31, 2012 at 4:59 pm

  thanx da DINA ila wengine hatukuona post iliyoonyesha diet full ili twende pamoja

 4. helner

  July 31, 2012 at 6:07 pm

  Nimeipenda hii,i thnk nitakuwa mmoja wa hao watu

 5. helner

  July 31, 2012 at 6:09 pm

  Thank you,for the great tips,hp i will be one of the winner cs real need loose it all

 6. helner

  July 31, 2012 at 6:09 pm

  Thank you,for the great tips,hp i will be one of the winner cs real need loose it all

 7. helner

  July 31, 2012 at 6:10 pm

  Nimeipenda hii,i thnk nitakuwa mmoja wa hao watu

 8. Anonymous

  August 1, 2012 at 5:36 am

  habari za kazi da dina nilikutumia email ya kuomba kushiriki diet lakini hazikua delivered,naweza pata email yako nyingine?kazi njema

  • sally

   August 1, 2012 at 11:23 am

   Ile gym yako iliishia wapi ?

 9. Anonymous

  August 1, 2012 at 6:47 am

  Mmambo Dina, nami sijui nilipitwa au? mana sikuona ile Post ya diet so sikuweza kuanza. Unaweza kutuwekea hapa tafadhali? Nilikutumia email pia ila sijapata jibu. Kazi njema

 10. mama 2 Mrs. M

  August 1, 2012 at 6:53 am

  Mambo Dina! natamani niwe mmoja kati ya hao Watatu katika hilo shindano. Maana natamani sana kupungua.

 11. Emmie

  August 1, 2012 at 8:37 am

  Hope ntafwata procedure ili nami niwe mmoja kati ya wafanya mazoez katika hiyo gym.

 12. Anonymous

  August 1, 2012 at 9:08 am

  mie pia naomba the diet plan!

 13. Anonymous

  August 1, 2012 at 10:10 am

  Hey Dina,

  Am on diet with you for a week now but nilikuwa field sikuweza pata gym for last week with all that am about 1.5 kg down, hureeeiiii

  Thank you so much
  Lydia

 14. Anonymous

  August 1, 2012 at 10:15 am

  natamani hiyo nafasi my dear ingeniangukia mimi maana tumbo ndiyo usiseme

 15. Anonymous

  August 1, 2012 at 11:21 am

  BASI DINA USITOE MASWALI MAGUMU JAMANIIIIIIIIIIIII

 16. emu-three

  August 1, 2012 at 11:54 am

  Mazoezi ni muhimu, lakini sio ukitoka hapo iwe kama ngombe aliyekosa majani,akipata majani anavyoyasakamia,….

 17. Anonymous

  August 1, 2012 at 12:29 pm

  habari mamii,tuko pamoja mi naendelea vyema,kwasababu ninabidii sana hasa ya mazoezi kila jion na diet yangu matokeo nimeanza kuyaona na yamenipa nguvu zaidi.mdau wa kiseke,mwanza

 18. Emmie kahere

  August 2, 2012 at 11:07 am

  Dina mie nliku sms but hujanitumia diet mpendwa.,emmie

 19. Anonymous

  August 2, 2012 at 12:39 pm

  Hey dina mbona comments hatuzioni au ni mimi tuuu!

 20. Anonymous

  August 3, 2012 at 7:43 am

  Hapo kwenye juice ya Embe na limao dada Dina umeniacha! hilo limao unakamulia baada ya kublend embe au wakati hujaanza kublend embe unakata limao unachanganya na embe unablend pamoja?

  Juice nyingine wapendwa ni ya papai + Embe na ndizi

 21. R.Ngaiza

  August 5, 2012 at 12:28 pm

  Safije, hongera mom Me hata nsipochaguliwa ntakuja tu. MaZoezi

 22. Anonymous

  August 7, 2012 at 8:23 am

  mazoezi mi najua yataka moyo, la sivyo utachemka.m.kisela

 23. Anonymous

  August 15, 2012 at 11:09 am

  nice one

 24. Anonymous

  August 16, 2012 at 7:58 am

  mamy maswali lini natumbua macho kila saa nisije pitwa na hili maana ninausongo.

 25. Anonymous

  March 21, 2013 at 1:20 pm

  Nimeipenda sana

 26. Anonymous

  March 21, 2013 at 1:23 pm

  Dada napenda sna. Naomba unisaidie post za diet ili nianze ya mwzi naomba unitumie kwenye email tangu bahatimchaki@yahoo.com.damahani kw usumbufu napenda twende kwa pamoja.nitashukuru sna Dada

Leave a Reply