Uncategorized

WANAWAKE WATANO WENYE NGUVU AFRICA

By  | 

Hatua ya kumchagua mwanamke kuwa mwenyekiti wa tume ya Muungano
wa Afrika, imekuwa dalili ya kuongezeka kwa viongozi wanawake Afrika.Hawa ni baadhi tu ya wanawake shupavu wa Afrika.

Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika.
Alichaguliwa tarehe kumi na tano mwezi Julai baada ya kinyang’anyiro kikali kati
yake na mwenyekiti wa zamani Jean Ping. Bi Dlamini-Zuma, mwenye umri wa miaka
63, ni mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo.

Ngozi Okonjo-Iweala, waziri wa fedha wa Nigeria. Bi Okonjo-Iweala, mwenye
umri wa miaka 58, ameshikilia nyandhifa mbalimbali za kimataifa, katika sekta ya
fedha .Aliheshimika sana wakati akiwa mkurugenzi mkuu katika benki ya dunia kwa
miaka mitatu, kabla ya kushindana katika kinyang’anyiro kuwa rais wa benki hiyo.

Ellen Johnson-Sirleaf, rais wa Liberia ana umri wa miaka, 72 na alitajwa kama
mshindi wa tatu wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011. Tuzo hiyo imetolewa miaka
sita baada ya yeye kuchaguliwa rais wa Liberia na kumfanya kuwa rais wa kwanza
mwanamke barani Afrika.

 Fatou Bensouda, mwendesha mkuu wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya
jinai, ICC. Bensouda mwenye umri wa miaka 51, aliteuliwa katika wadhifa huo
mwezi Juni mwaka huu na kuchukua nafasi ya Luis Moreno-Ocampo kutoka Argentina.
Kabla ya hapo Bensouda alikuwa naibu mwendesha mkuu wa mashtaka tangu mwaka
2004.

Joyce Banda, rais wa Malawi. Bi Banda mwenye umri wa miaka 62, amefannya
jambo la kihistoria kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo. Pia yeye ni
mwanamke wa pili kuongoza nchi ya ya kiafrika. Anaheshimika kakam mwanaharakati
wa haki za wanawake.

story kwa msaada wa bbc swahili.

2 Comments

  1. Anonymous

    July 27, 2012 at 5:05 pm

    Mbona hujamuweka Migiro, Mogella, Amina. Rekebisha sentensi wanawake watano maarufa walio madarakani kwa sasa Afrika

  2. Anonymous

    August 1, 2012 at 9:24 am

    this is inspiring, women lets wake up..we can do more than there

Leave a Reply