Uncategorized

MABALOZI WA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSTELI ZA WASICHANA WA SEKONDARI WAZINDUA KAMPENI YA “ELIMU YAO, WAJIBU WETU”

By  | 

 

Mratibu wa mabalozi wa
kampeni ya uchangiaji katika ujenzi wa mabweni Rebeca Gyumi ambaye ni pia ni
mtangazaji wa kipindi cha fema akielezea jinsi walivyojipanga kuhakikisha
wanachangisha  fedha za kutosha ili lengo
la TEA likamilike.

Mabalozi
wa kampeni ya TEA katika ujenzi wa hosteli wakiwaomba wananchi kushiriki
kampeni hii kwa kuchangia kwa kutuma ujumbe CHANGIA TOFALI kwenda kwenye namba
15564. Katikati ni Mkurugenzi wa uhamasishaji wa TEA Seif Mohamed.

Mkurugenzi
wa uhamasishaji wa Taasisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Seif Mohamed akiielezea
kampeni ya kuchangia ujenzi wa hosteli 30 zitakazowahudumia wanafunzi wa kike
wa sekondari 1,504 nchini katika mikoa nane huku mabalozi wa kampeni hiyo wakifuatilia
mazungumzo hayo kwa umakini katika uzinduzi wa muungano wa TEA na Mabalozi hao
uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini DSM.

 

Jokate
Mwegelo (kulia) akielezea imani yake kwa watanzania  na kuwaomba raia wanaoiombea mema nchi yetu
kuguswa kama walivyoguswa wao kujituma katika kuchangia kampeni hii ambapo
ujumbe mmoja wa CHANGIA TOFALI ni shilingi 250/=, Kushoto kwake ni Mwanablog
maarufu na mwanamitindo Mariam Ndaba

Mabalozi
wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika picha ya
pamoja, kutoka kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Rebeca
Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA), Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa
blog)  Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili
Miss Tanzania 2006) na asiyekuwepo ni Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004)
ambaye alikuwa na udhulu na atakuwepo katika kampeni zinazoendelea.

 

Nancy
Sumari ambaye ni Miss Tanzania  2005 na
pia mrembo aliyefikia ngazi ya juu katika mashindano hayo ya urembo akielezea
jinsi alivyoguswa na kuamua kujitoa kwa asilimia mia moja kusaidia kampeni
hizi. Katika kampeni hii TEA inakusudia kuchangisha jumla ya shilingi bilioni
2.3

Waandishi
wa habari waliofika kuhudhuria uzinduzi wa ‘Elimu yao, Wajibu wetu” kampeni
iliyoandaliwa na mabalozi waliojitolea kwa hiari kuhakikisha fedha hizo
zinapatikana. Kiasi chote kitakachopatikana katika kampeni hiyo kitaingizwa
katika mradi huu.

 

Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja
mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono
jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za
kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia
wasichana wa shule za sekondari 1,504.

Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na
Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania
2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss
Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa
namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na
TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.

Lengo la Mabalozi hawa ni kuhamasisha uchangiaji na
kuwezesha kujenga zaidi ya hosteli 5 kati ya 30 ambazo TEA imepanga kujenga.

Katika Uzinduzi huo uliofanyika Tarehe 31/07/2012
katika hoteli ya Serena Jijini DSM kati ya mabalozi hao na Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA) ambapo ni Faraja Nyarandu pekee ndie  alikosekana kutokana na kubanwa na majukumu
mengine lakini alithibitisha uwepo wake katika kampeni zinazoendelea.

Leave a Reply