Uncategorized

MAPISHI:FIRIGISI NA NDIZI ZA KUKAANGA!

By  | 
 Jumapili nilipata mgeni ikabidi niingie jikoni kumuandalia chakula cha mchana.Chakula kilikuwa firigisi na ndizi za kukaanga na salad kidogo.Nilihitaji vitunguu na karoti kama zinavyoonekana pichani.
 Firigisi zenyewe
Nikaweka sufuria jikoni na mafuta ya kupikia,mie natumia mafuta ya alizeti.
Mafuta yalipopata moto nikatia vitunguuu nikavikaanga mpaka vikawa brown.
Nikaweka firigisi zangu,unaweza kuzikata vipabde vidogo vidogo ila mie nilipendelea kuweka kama vilivyo.Nikaziacha zichemke kidogo kama dk 5 hivi…
Kisha nikatia limao,sikuongeza maji hata kidogo maana sikuwa nahitaji mchuzi.
Baada ya hapo nikaweka chicken masala ya aina hii naipenda sana maana ina harufu na ladha tamu sana.Huu ni mchanganyiko wa karafuu,tangawizi,kitunguu saumu,pilipili,chumvi,mdalasini,binzari,pilipili manga n.k
Nikaweka kijiko kimoja
Nikakoroga na kuongeza maji kidogo,chumvi kisha nikafunikia ziweze kuchemka na kuiva vizuri.
Baada ya dk 10 hivi nikaweka karoti na kukoroga kwa dk 1 kisha nikaipua zikiwa tayari zimeiva.
Pia nikakaanga ndizi kwa kuanza kuweka frying pan jikoni na mafuta ya kupikia.
 Ndizi niliziweka chumvi kabisa.
Mafuta yalipopata moto nikaweka ndizi na kuzikaanga.Zilipokuwa tayari nikaipua tayari kumuandalia mgeni chakula.

Ni chakula kitamu,haraka na rahisi kuandaaa…tayari kwa kuliwa.

22 Comments

 1. Anonymous

  August 12, 2012 at 3:14 pm

  Dina hujaweka nyanya nijibu fasta nipike

 2. Anonymous

  August 13, 2012 at 8:58 am

  OUT OF TOPIC

  DINA LEO UNANIFURAHISHA SANA NA NYIMBO ZAKO TOKA ULIVYOANZA NA JD , DIAMOND, MAZILIMAZILI , IF YOU DONT NEED ME NOW , UWIIII YOU MADE MY DAY THANKS

 3. lily z

  August 13, 2012 at 9:13 am

  wat a delicious meal umenkumbusha firgs cjazla muda natamanije!plz nkarbishe nije kula siku moja.

 4. Anonymous

  August 13, 2012 at 10:24 am

  Asante Dada Dina kwa Mapishi mazuri na rahisi

 5. RUKY

  August 13, 2012 at 11:09 am

  MWANAMKE KUPIKA BWANA. LAKINI DINA UNGETUONYESHA NA WEWE JAPO UKIKOROGA SHOGA.. MWANAMKE UMBEA MBONA HUKUTUONYESHA PIA MKILA NA MGENI WAKO?

 6. Anonymous

  August 13, 2012 at 1:48 pm

  Alisema ni Mhaya, sasa ndizi za kukaanga wapi na wapi?????, au alikuja shem ambaye ni mnyamahanga?

 7. Anonymous

  August 14, 2012 at 5:14 am

  Hii topic ya kupika tafadhali uendelee nayo. Na kama hivi umeweka na picha, safi sana!
  I am a man, napenda sana kupika. Ila malezi niliyolelewa, sikupata nafasi ya kujifunza. Please keep on posting hii kitu. Thank you!

 8. Anonymous

  August 14, 2012 at 10:29 am

  nimekipenda kweli lazima na mimi niandae

 9. Anonymous

  August 14, 2012 at 7:28 pm

  nimependa pishi lako

 10. Anonymous

  August 15, 2012 at 5:42 am

  ok poa nimeipenda sana hiyo dina inaonekana ni delicious

 11. mama 2 Mrs. M

  August 15, 2012 at 7:09 am

  Kwa kweli Dina kama alivyosema mchangiaji hapo juu, jitahidi kuweka mapishi, hata mi napenda sana kupika, kwa kweli umenitamanisha sana! na nimejifunza kitu, siyo kila siku mgeni akija, ooh pilau, wali, chipsi, ubunifu kama huo ndo unaotakiwa kwa mtoto wa kike. Mtoto wa kike jiko babu!!!. Asante Dina!

 12. Anonymous

  August 15, 2012 at 9:39 am

  yaaani mate yananitoka… naenda pika na mimi sasa hivi! Mungu akubariki Dada Dina. Nakuomba uendelee kututumia mapishi mengine. Wengine sie tunajifunzia hapa hapa… Lov u.

 13. kitwitwi

  August 15, 2012 at 1:13 pm

  mimi penda sana kupika nielekeze kiungo ntakipata wapi hapa dar plzzzzzz

 14. Anonymous

  August 16, 2012 at 8:16 am

  Tamu je?

 15. Anonymous

  August 16, 2012 at 9:51 am

  Asante sana da Dina.
  Mie nikiingia ktk blog yako cha kwanza naanzia mapishi kuona umepost nn kipya! haha mwanamke akiwa home sifa ya kwanza apike msoc mtam watu wale washibe ndo story ziendelee..
  Thenk youuu

 16. Anonymous

  August 17, 2012 at 2:09 pm

  yamyam

 17. Anonymous

  August 20, 2012 at 8:19 am

  safi sana dada

 18. Ammy K

  August 23, 2012 at 9:33 am

  uwiiiiiiiiiii mate kutoka, ninavyopenda firigisi mimi acha tu, nitakuomba mwaliko siku moja. unipikie hivyo hivyo. haaaaaaaahaaahaaa, utani tu dada, kila la kheri. me pia napenda sana kupika.

 19. Anonymous

  November 2, 2012 at 1:28 pm

  nimeipenda hiyo Dina

 20. Anonymous

  January 7, 2013 at 11:38 am

  msosi mtmuu huo.I like it

 21. Anonymous

  January 17, 2013 at 9:19 am

  nimeipenda sana maana ndio sifa kuu ya mwanamke mengine yafuate! endelea kutuhabarisha

 22. Habbie .H.

  February 5, 2013 at 4:29 pm

  Yaani hapa nimecopy kila step.
  Asante dada . . nimeipenda kwakweli!

Leave a Reply