Uncategorized

MAPISHI:MBOGA YA NYAMA YA KUSAGA

By  | 
Haya mdau nina pishi dogo tu hapa napenda kulishare nawewe.Ni pishi la mboga ya nyama ya kusaga iliyoliwa na ugali pamoja na mboga ya majani ya mchicha.Hapa ntakuekea tu kuhusiana na mboga ya nyama ya kusaga.Ni mboga rahisi kuandaa na pia kuiva upesi.
Nikiwa napika huwa napenda kuandaaa kila kitu kiwe tayari ili nikianza nimeanza,mahitaji yetu kama unavyooona ni karoti,hoho na kitunguu maji.

Nilitwanga tangawizi mbichi nikaichanganya na nyama yangu ya kusaga.

Nikaweka frying pan jikoni na mafuta kidogo tu yalipopata moto tu kitunguu nikaweka na kukikaanga mpaka kikawa brown…
Nikatia nyama na kuikaanga
Halafu nikafunikia kwa dk 5 iive

Nikaweka limao na pilipili….
 Halafu nikaweka zile hoho na karoti,sijatumia nyanya ila ukipenda unaweza kuweka nyanya.
Nikafunikia kwa dk 5 tu…
Kama nilivyosema ni mboga ya haraka sana ndani ya kk 20 tu inakuwa imeiva.Kwangu ililiwa kwa ugali na mboga ya majani ya mchicha.Lakini inaweza kuliwa na wali,ugali,chapati,chips,ndizi za kukaanga au kuchoma,makaroni n.k

10 Comments

 1. lily z

  August 26, 2012 at 3:18 pm

  asante mamiiii

 2. Anonymous

  August 27, 2012 at 8:40 am

  hello dina asante kwa pishi hilo mpenzi,kazi njema

 3. Ammy K

  August 27, 2012 at 11:22 am

  nyama ya kusaga ya kopo au fresh de.

 4. Anonymous

  August 27, 2012 at 7:40 pm

  Safi kwa pish zuri da Dina

 5. Ammy K

  August 29, 2012 at 12:10 pm

  ilikuwa tamu inaelekea. haya mwaya tunasubiri mapishi mengine zaidi ili nasi tupate kujifunza. ASANTE

 6. Disminder orig baby

  August 31, 2012 at 10:03 am

  Asante Dina kwa pishi zuri.
  Naomba leo nikupe jingine lisilo na mafuta.

  1. Ichapue nyama yako kwa spices unazopenda.
  Mimi hupenda kuweka, kitunguu saumu, tangawizi, pilipili manga ya unga, chumvi na kitunguu maji.

  2. Chemsa nyama yako katika moto mdogo. Nyama itachucha maji yake ambayo yataiivisha. Wakati inachemka weka ndimu, iache iendelee kuchemka mpaka ikikaribia kukauka maji unaweka Nyanya ya tunda. Nyaya ya tunda ikiiva unaweza kuweka na nyaya ya kopo kama unapenda.
  Acha ifikie kile kiwango cha mchuzi unachotaka.

  3. Unaweka karoti na Hoho kama dakika mbili tu na kuitoa tayari kuliwa kwa Chapati, mkate, na vingine vingi.

  KIDOKEZO.
  Mimi hupenda kuweka Simba Mbili (curry powder wakati nimeweka nyaya ya tunda) au mwisho kabisa karibu naweka karoti na hoho naweka Royko mchuzi mix.

  Nikiwa naipakua katika bakuli la kusevia mezani hunyunyizia majani ya Cotmir kwa harufu nzuri zaidi.

  Pia karoti wakati nazitayarisha huweka huweka chumbi na ndimu kidogo, naziloweka mpaka wakati wa kuweka katika mchuzi.
  karoti inakuwa na ladha nzuri sana. Jaribu utapenda, hasa kwa kachumbari.

  Pia kwa wale wanaopenda vitunguu unaweza kukiweka kabla hujaweka nyaya ili kupata ladha zaidi ya kitungu. Mimi nachemsha kabisa na kitungu kwa sababu sipendi kula vitunguu ila najilazimisha kwa sababu ya faida zake mwilini.

  MIMI HUPENDA KUPIKA HIVI KWA SABABU SITAKI MAFUTA.

 7. Anonymous

  August 31, 2012 at 2:00 pm

  nimependa hiyo sana Dina mpnz.

 8. R.Ngaiza

  September 2, 2012 at 5:59 am

  Na hasa Na tambi yummy yummy

 9. Anonymous

  September 10, 2012 at 10:07 am

  hiyo si mboga ila ni kitoweo . mboga ni za majani kama mlivyozoea kuita.

Leave a Reply