Uncategorized

NG’OMBE WANAOKULA JALALANI

By  | 
 Nikawaida kwa ng’ombe kula majani hata kama wanafugwa manyumbani.Wakati mwingine hula pumba pia zitokanazo na mahindi.Lakini ng’ombe hawa ni tofauti jamani.
 Ng’ombe hawa hupelekwa na watoto na kuachwa hapo hapo jalalani.
 Jalala hili lipo katika barabara ya mbezi africana mji mpya ndilo wanalolitegemea kwa mlo.
 Mbwa hawa ndio wanaowachunga hawa ng’ombe mpaka watakapokuja kuchukuliwa.

 Huyu jike mweusi unaambiwa anatoa maziwa lita 11 mpaka 12 kwa siku wanasema watoto waliokuwa wamewaleta na kuwaacha hapo.Pia ameshazaa mara kumi na mbili.

Hili hapa ni dume kwa ajili ya kuwapanda majike.Mie sijawahi kuona ng’ombe wanakula jalalani sasa sijui hapo wanakula nini hasa.

3 Comments

 1. Anonymous

  August 5, 2012 at 2:49 pm

  Hyo hatar maana nlckia ng'ombe akila mfuko wa nailon anakufa.lilian masika

 2. RUKY

  August 5, 2012 at 7:27 pm

  NI HATARI KWELI NILISHA ONA NGOMBE ANAUMWA TUMBO LIMEVIMBA HAWEZI KULA NGOZI IMEKUWA MBAYA KUMBE KWENYE UTUMBO KUNAMIFUNKO YA PLASTIKI ALIYOKULA NA MISUMARI NA VITU VICHAFU VINGI… MPAKA KUGUNDULIKA NIALIPOTAKA KUFA AKAWAHIWA KUCHINJWA NDIYO AKAKUTWA NAVYO..

 3. Anonymous

  August 6, 2012 at 4:30 am

  Ukistaajabu ya Mussa ………….

  Mimi

Leave a Reply