Uncategorized

THINK LIKE A MAN …MOVIE YA KUANGALIA KAMA BADO HUJAIONA!

By  | 
Ni filamu inayotokana na kitabu cha think like a man….ni nzuri sana ki ukweli.Inazungumzia maisha ya mahusiano na namna wanawake wanavyotumia hiko kitabu kupata tip za kuweza kuwa win wapenzi wao.
 Taraj P.Henson akiitwa Lauren…yeye ni mwanamke mrembo mwenye kujiamini,kujituma na ana kila kitu isipokuwa mpenzi.Mafanikio kibao ila mpweke Na anatarajia akipata mpenzi awe mwenye mafanikio kama yeye.Anakuja kukutana na Dominic waiter na mpishi…..anajifunza kuwa unaweza kukutana na wanaume wenye kazi nzuri,cheo n.k lakini mkawa hamuendani stress tu.Moyo wenyewe unajua wapi penzi la kweli lipo.
Humo kuna Michael Early ambae amecheza kama Dominic…ni mpishi/waiter kikazi .Nimwanaume mwenye ndoto nyingi kila ukikaa nae anataka akueleze mipango yake na matarajio ya baadae.Anachohitaji ni mwanamke wa kumuelewa na kumsaidia/kumuongoza kutimiza malengo yake.
 Gabriella Union amecheza kama Kristen…yeye ni mdada yupo focused na pia anataka sana kuolewa ila mpenzi wake hataki na ni muoga wa ndoa na commitment.Anatumia kitabu hiki kupata tip za kuhakikisha mwanaume wake anakuwa na malengo na yeye hatimae ndoa.
 Chriss brown yupo ila yeye kacheza kama kicheche tu.
Romany Malco amecheza kama Zeke….uhusika wake yeye ni mwanaume kicheche(playboy)haitaji kutulia na mwanamke yeye ni mkikutana umpe mchezo Bhaaasi.Na ana skills za kumpata msichana yoyote anaemtaka.
 Meagan Good ambae humu anaitwa Mya anakutana na Zeke (play boy)…Mya ni msichana anaetafuta mwanaume wa kutulia na yeye na kuwa na malengo ya future kama mke na si playboy.Kwa msaada wa kitabu anafanikiwa kumteka playboy kufall in love na yeye.
Terrence J akitumia jina la Michael…yeye ni mama’s boy….yaani kila kitu ni mama,mama..mama hivi mama vile akikutana na msichana lazima ampeleke kwa mama yake akathaminishe.Ila ni kijana mwenye sifa zote za kuwa mpenzi na mume wa msichana fulani.Anahitajika msichana wa kuweza kuvunja huu umama’s boy na kummiliki yeye.
Kevin Hart anatumia jina la Cedric yeye alishaoa na yupo katika process za talaka na mkewe.Anachofanya ni kuwakatisha tamaa vijana kuhusu ndoa,ndoa ni utumwa..ndoa haina mpango n.k
Ningeweza kuelezea mengi hahahahahah ila kwa uliyeona naamini umepata kitu.Kama bado kuona itafute.

16 Comments

 1. mama 2 Mrs. M

  August 15, 2012 at 12:20 pm

  ok Dina sijaiona, Inaonekana ni nzuri, poa nitaitafuta.

 2. Unknown

  August 16, 2012 at 9:05 am

  Hii mivie ni nzuri sana. Nimeiona na nimesoma kitabu pia.

 3. Anonymous

  August 16, 2012 at 10:02 am

  Kitabu chake kizuri sana. Ukikisoma na kukielewa wala hutapata shida. Nina soft copy yake

  Mimi

 4. Anonymous

  August 16, 2012 at 2:14 pm

  sijaiona but nititafuta kwan yaonekana ni ya ukweli

 5. Anonymous

  August 17, 2012 at 6:45 am

  nimeiona. ni nzuri sana na ina mafundisho ya kutosha hasa kwa wadada

 6. Anonymous

  August 19, 2012 at 6:50 am

  nzuri.ntaitafuta

 7. Anonymous

  August 20, 2012 at 5:44 pm

  Ni movie nzuri sana,lakini mwisho wa siku tunafundishwa mapenzi ya kweli huyapati kitabuni!!

 8. Anonymous

  August 22, 2012 at 7:48 am

  jaman naomba uyo dada apo juu tuwasiliane anitumie soft copy ya hicho kitabu

 9. liz

  August 22, 2012 at 1:06 pm

  NIMEITAMANI JAMANI NI NZURI

 10. ammy k

  August 23, 2012 at 9:25 am

  asante dina, mwenzio huwa nakusubiria uwe unaangalia movi nzuri ukisema tu me kazi yangu kudownload.

 11. Anonymous

  August 23, 2012 at 11:32 am

  huyo dada mwenye hiyo soft copy, unaweza kutupatia?

 12. Anonymous

  August 23, 2012 at 12:40 pm

  ni nzuri sana dina. nimeiona.
  kama una nyingine pliiiiiiiiiiiz.

  uwe na siku ya kutupa vitu vizuri kama hivi.

 13. Anonymous

  August 23, 2012 at 12:50 pm

  Jamani hivi unadown load vipi, mwenzenu mie hata sijui, i like watching movie, zilizotulia kama hivi

 14. Anonymous

  August 23, 2012 at 1:41 pm

  Yap hii Movie nayo tamu kwa wale ambao si wapenzi wa movies za action, japo mwanzoni inaanza kama kuboa flani ila kama ni mtu wa kutaka kufahamu what next ukatulia utafurahi huko mwishoni, dah nzuri n I like most meagan Good n Taraji walivyocheza part zao.

 15. cisca

  August 29, 2012 at 10:54 am

  jamani dada mwenye soft copy nitumie hapa mymice23@yahoo.com

 16. Annastazia Mlaki

  September 11, 2012 at 9:42 am

  Hongera sana dina na wenzako yaani mara nyingi nawasikiliza halafu nampenda sana bi ponza yule wa kitcen party, anatoa dozi safi sana, naomba ukipata nafasi ktk chachandu mnipigie ule wimbo wa kitchen party bahati mbaya zipo sijui tatu hivi we chagua wowote mmoja Mimi naitwa Mrs Annastazia Mlaki

Leave a Reply