Uncategorized

FILAMU YA WOMAN THOU ART LOOSED IN 7 DAYS!

By  | 
Hii filamu nimeiangalia jana nyumbani na leo nikaisimulia katika leo tena!!
Wahusika wakubwa katika hiyo filamu Blair Underwood,Sharon Leal na mchungaji T.D.Jakes ambae filamu hii inatokana na kitabu alichowahi kuandika.Kitabu hicho kinaitwa Women thou art loosed .
Katika filamu ni familia  ya Mr.David Ames  na mkewe Kari wakiwa maejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kike Mikayla.
Familia yenye furaha,amani na mapenzi tele…hakuna tatizo kila siku ni siku njema kwao.

 Yaani walikuwa wanapendana sana kama ambavyo filamu ilitaka tuone.
 Maisha yanakuja kubadilika baada ya mtoto wao wa pekee mwenye miaka 6 kupotea.Inakuwa ni stress sana katika familia hii.Na ndipo hapo inakuja kujulikana siri ya Kari kwamba aliwahi kuwa changudoa,kutumia dawa za kulevya na sexual abused na baba yake akiwa mdogo.Ukweli ambao hakuwahi kumwambia mumewe hata jina alibadilisha ina maana jina mume analolijua sio la kwake.Jambo hilo linaendelea kuleta mpasuko zaidi kwenye familia hii maana mume anahisi lazima kuna mtu wa zamani wa historia ya mkewe anaweza kuwa ndio anahusika na kupotea kwa mtoto.Mke anajieleza kuwa aliamua kuanza maisha mapya na hayo yalikuwa maisha yake ya zamani.Ndio hakumwambia ukweli lakini alifanya hivyo ili aanze ukurasa mpya hakutaka kukumbuka zamani.
Mtoto amepotea kwa siku saba na siku ya saba inakuja kugundulika kuwa kumbe hata bwana David ana siri kubwa zaidi ya mkewe.Na siri hiyo ndio chanzo cha kupotea kwa mtoto wao.Kumbe aliwahi kuwa na mahusiano na mfanyakazi wake wa ofisini.Msichana huyo aliwahi kupata mimba na David akamwambia aitoe kwani yeye ana mke na anampenda sana mke wake.Kweli yule msichana alitoa mimba na mahusiano yao yakaishia hapo ila akabaki na machungu,kisasi ambacho mwanaume alikuwa hajui.Kumbe watu wanahangaika kutafuta mtoto huyu dada ndio kamteka kamfungia nyumbani kwake.
Nimesimulia leo kwenye leo tena maana ni filamu iliyonisisimua  sana hapa nimesimulia kifupi tu itafute utazame..
Kuna dada hapa alinitumia meseji kwenye kipindi mcheki nae kama unaweza kuipata.
*hiyo movie inatwa WOMAN THOUART LOOSED ON 7 DAY na kwa anaye ihitaji inapatikana movie lounge shoppers plaza mikocheni. Natalie wa mikocheni 255657924875.
MSG za wana leo tena kwa ufupi baada ya story!
1.BWANA NDIYO MKOSEFU ZAIDI,ZAI SHY
2.du! Iyo tori noma sana ata wewe msimuliaji umetisha aziza soft kawe

3.yani dinna unajua kusimulia kama nIko natizama video saa hii,.. editha wa kinondon

4.iyo film ni nzuri sana inamafundisho mazuri nimeipenda sana.kijol kibao wa 96.0 tanga

5.mwisho wa simulizi utwambie hilo filamu inaitwaje.Mama frank wa mwenge.

6.Jaman dada dina hadi raha hiyo story nataman kuiona inaitwaje?, RAHEL MWANJA,NIPO SINGDA,

7.Dina hiyo movie ni nzuri sana naomba utuambie jina lake pse – ESTHER WA ARUSHA

13 Comments

 1. Anonymous

  September 24, 2012 at 11:21 am

  ni kweli dina tunashukuru lkn ungekuwa ukituwekea hata soft copy hapo nasi tuwe tunaangali ingekuwa vizuri maana tuko mikoani madukani huku hakuna kuna za bongo move tu.

 2. MOJAONE

  September 24, 2012 at 11:32 am

  Dina mbona hampatikani live kwenye website kolikon??

 3. MOJAONE

  September 24, 2012 at 11:38 am

  Dina ungekua unaweka mada zako za kipindi cha kesho hapa ili nasi wa mbali tuweze kushiriki kwa coment zetu nawe kuzisoma kwenye kipindi au fungua page ya leo tena facebook ili watu waweze kushiriki.

  • dinamariesblog

   September 25, 2012 at 3:40 pm

   Ni kweli ntakuwa najitahidi kuweka hapa ili mchangie pia page ya face book ya leo tena.

 4. mama Glory

  September 24, 2012 at 12:29 pm

  kwenye hii filam mwanaume ndio anabeba lawama zote kwa sababu alisaliti ndoa yake so hayo ndio matunda ya kutoka nje ya ndoa, kwa upande wa mwanamke hana makosa kwa sababu alishaacha ya nyuma na kuanza ukurasa mpya wa maisha yake. wanandoa tueshimu ndoa zetu unapotoka nje ya ndoa ujue ipo siku hicho kitendo kitakugharimu.

 5. Anonymous

  September 25, 2012 at 7:10 am

  duhh… yani hiyo ni bonge la movie nliicheki kama mwezi mmoja hivi umepita, yani hadi raha,kama hujaiona itafute inafundisha, kusisimua na kuburudisha kwa ujumla

 6. Anonymous

  September 25, 2012 at 12:22 pm

  Dina niliangalia hii movie last two weeks and it was so very nice! unlike bongo movies ambazo u can easily predict mwisho wake, hii ni tofauti mnooo…imagine ukweli ulijulikana unexpectedly! ni movie ya kuangali hata mara sita na huchoki! fundisho kubwa nilopata ni kwa mwanamke kutokata tamaa even when u r facing the odd!
  Eva

 7. Anonymous

  September 25, 2012 at 1:34 pm

  dina unajua kututeka kweli yan unasimulia vizuri, kama nilikua naiona jinsi unavyosimulia. ni movie nzur. bealito from dom

 8. robby tanga

  September 25, 2012 at 9:13 pm

  Aisee Dina hii Move ni kali sana na ni nzuri yaani, acha kabisa, uliposimulia niliitamani nikaingia ndani ya blog yako nipate jina lake, ni kwamba nimeishusha nzima nzima through internet na tarehe 24 sept nikaicheki yote, endelea kuwa mbunifu katika movie kama hizi.

 9. Anonymous

  September 26, 2012 at 8:57 am

  HIYO FILAM NI NZURI SN AISEE,SASA INAPATIKANA BEI GANI?NAITAKA ILA NIJUE BEI KWANZA

  • MOJAONE

   September 26, 2012 at 10:55 am

   MAMBO YA BAJET HAYO ETII???

 10. Anonymous

  September 26, 2012 at 10:22 am

  Mie nimeiona long mbona, uliyosimulia ni sahihi lkn pia maana ya filamu ni kwamba maisha ni siri na kila mtu ana siri ila ukigundua siri ya mwenzako isiwe nongwa ujue watu huwa wanabadilika. Pia kikulacho ki nguoni mwako. Thxs tazama pia "Think like men" or "Always be Good".

 11. Anonymous

  September 29, 2012 at 11:03 pm

  Ngoja niisake online. Lol. Raha ya kuwa na mtandao ndio hii…sinunui movie hata moja nangoja Dina arushe mi nitafute maana ziko millions siwezi jua nzuri ni ipi na sina muda wa kupoteza kubahatisha kuangalia movie saa nzima afu nijutie muda wangu.

Leave a Reply