Uncategorized

JAMANI MNISAMEHE KWA KUCHELEWA KUWAWEKEA DIET HAPA.

By  | 

KATIKA WATU 50 NILIOWAPA DIET NI WATATU TU NDIO WAMENIPA FEEDBACK.INAMAANISHA MLIOFANYA NI WACHACHE SIJUI.ILA NIMEFURAHI MDAU HAPA AMENIPA FEEDBACK NA MATOKEO AMEYAONA…

Hallo Dina, 

Pole na shughuli za kila
siku, sorry nilikuwa busy sana sikuweza kukupatia feedback ya diat yangu thanks
kwani nimeweza kupunguza kilo 7 kwa mwezi mzima wa 8 na sasa naendelea na diat
hiyo kwani nataka kufikia dec niwe walau na kg 80 na kwasasa nina kilo 105
kutoka kilo 112 nilizokuwa nazo before diat. Many thanks i will inform you
maendeleo yanakuwaje na kwa sasa najisikia mwepesi sana nimefurahi.

Yours Catherine!

DIET YENYEWE HII HAPA


JUMATATU
MPAKA JUMATANO
ASUBUHI:supu ya mboga mboga isiyo na mafuta hata kidogo
MCHANA:Juice ya matunda upendayo lita 2 hakikisha ni nzito ili iwe ndio kama
mlo wako.
Wakati wote unakunywa maji mengi angalau lita 2 kwa siku yasiwe ya
baridi.Unaweza kuwa unatafuna matango na karoti kwa mchana kutwa.
JIONI:Ikifika saa moja unaweza kunywa chai bila sukari ukatulia kidogo halafu
ukanywaJuice yako nyingine nzitooo kama uji hivi.Kumbuka juice usiweke sukari.

Huuu ni mpangilio ambao utaurudia kwa siku tatu kuanzia jumatatu mpaka
jumatano.

ALHAMISI
ASUBUHI:SUPU YA SAMAKI
MCHANA:Juice lita 2 na maji ya kutosha huku ukitafuna matango na karoti.
JIONI:Samaki wa kuchemsha au kuchoma na salad nyingi.


IJUMAAA
ASUBUHI:Supu ya kuku na kiazi kimoja cha kuchemsha
MCHANA:Juice lita 2,maji, na mboga mboga upendazo bila kusahau matango na karoti.
JIONI:Kuku choma au wa kuchemsha na ndizi moja ya kuchoma au kuchemsha.Na
salad.

JUMAMOSI.
ASUBUHI:Supu ya kuku na mkate wa brown
MCHANA:Samaki wa kuchoma na mboga mboga
JIONI:Kuku choma nusu,mboga mboga au salad ya kutosha .pia usisahau kunywa maji
ya kutosha na matango ila hii sio siku ya juice.

JUMAPILI.
Kula chochote unachotaka ila zaingatia visiwe vya sukari wala mafuta mafuta.Maji
ni muhimu sana sana kunywa maji mengi.

Ikifika jumatatu unaanza utaratibu wa kila jumatatu mpaka jumapili kwa mwezi
mzima.

MAZOEZI.
Kwa siku zote hizi usiache kufanya mazoezi maana yanasaidia unavyopungua mwili
unakaa vizuri hauwi manyama yaliyolegea.Ruka kamba hata kidogo,situps kwa ajili
ya tumbo.Mengine ntawaekea blog kama hauwezi kwenda gym unaweza kufanya mwenyewe
nyumbani.

PLS usicheat diet yako ntafurahi ukipata matokeo ili nami niwe nilikusaidia au
kukutia moyo na wewe upungue.

Kumbuka mlo wa jioni unaliwa mwisho saa moja pia fuatilia post zangu za nyuma nimekuwa nikitoa tip za kutengeneza juisi za aina mbali mbali.Ni diet ngumu mwanzo lakini ukizoea unapeta tu.

KILA LA HERI!!

14 Comments

 1. Anonymous

  September 15, 2012 at 5:36 pm

  Hi Dina

  Asante kwa kutupa ratiba ya diet ila mie nilikutumia email ukunijibu my dear lakini nashukuru nimeikuta hii ratiba kwenye blog nitajitahidi nifuate then nitakupa majibu.

  Siku njema

  Halima Juma

 2. Emmie

  September 15, 2012 at 6:13 pm

  Yan kwanzia ju3 naanza nayo maana naona ni nzur na itanisaidia.,nafurah sana kuipata kiukwel an i promice ntakupa feedback nzur dina

 3. Anonymous

  September 15, 2012 at 6:57 pm

  Mambo mamii sasa khs pombe je tunaweza kunywa aina gani ya pombe je savana ni poa kweli au?

 4. Anonymous

  September 17, 2012 at 8:28 am

  Asante dada Dina kwa Diet,ila kipimo halisi cha samaki na kuku ni kipi?mana isije kua umeambiwa kuku wa kuchemsha basi ndio kuku mzima!naomba kujua kama ni samaki ni kwa kiasi gani na kwa kuku pia…Ubarikiwe sana.

 5. RUKY

  September 17, 2012 at 8:53 am

  DAAA MI NIIISHIA KATIKATI.. NIMEPUNGUA KG 2 TU KUTOKA NA SITUATION NILIYOKUWA NAYO THANKX KWA DAYAT NTAJARIBU TENA INSHAALAH

 6. Anonymous

  September 18, 2012 at 1:48 am

  Shukrani Dina kwa kutoa hii ratiba ya diet upya. Nitajitahidi kuifuatilia ingawa huku Marekani vyakula vya mboga mboga na juice ni gharama kweli. Ila nitajitahidi kwani uzito wangu ni 87kg nimepima leo hadi roho ikaniuma. Huku niliko mimi ndizi za kupika hakuna je naweza kutumia viazi badala ya ndizi? Nikutakie majukumu mema

 7. ELIUD SAMWEL

  September 19, 2012 at 3:56 pm

  tukushukuru xana da dina kwa kututatulia matatizo

 8. Anonymous

  September 20, 2012 at 6:27 am

  je kuna vyakula vingine tofaut na hivo? kama mimi n mwanafunzi wa chuo nategemea sana vyakula vya kunua hapo chuo na vyenyewe ni kama wali, ugal, chipsi, ndiz…. utanisaidiaje hapo dina?

 9. Anonymous

  September 20, 2012 at 7:55 am

  Mambo bi dada,mi mzima na nashukuru naendelea na diet kama kawaida,nakumbuka nilikutumia picha kabla sijaanza diet na mazoezi,na nimeazimia nikutumie tena picha baada ya diet na mazoezi,nimefanya kwa bidii na matunda nimeyaona,nitapenda kushare na wadau ili niwape moyo zaidi,asante sana.MAMA ISACK WA KISEKE MWANZA.

 10. Anonymous

  September 20, 2012 at 10:13 am

  Kuna mtu nimemsikia leo clouds fm asubuhi yeye anasema unaweza kula kila kitu kama kawaida ila kuna maelekezo ya kufanya sijui kama ulimsikia Dina

 11. Anonymous

  September 21, 2012 at 9:26 am

  DINNA RUSHA DIET YA MAMA ANAYENYONYESHA………………

 12. Anonymous

  November 20, 2012 at 11:45 am

  habari Dina..
  hii diet yako ni nzuri sana..mie nilimpa mama yangu alikuwa na kilo 70 kabla jaanza na hadi wiki iliyopita amepima nikiwepo na nimeona kwa macho yangu zaidi ya mizani 3 ana kilo 65…yeye amekuwa mkweli maana anaifuata diet hii kama ilivyo bila kuongeza au kupunguza,kila ulichokiandika ndivyo anavyofanya…asante maana imemsaidia alikuwa overweight kiasi flani ukilingalisha na urefu wake 167…jamani ifuateni hii diet ni NZURI SANA…

 13. Anonymous

  February 22, 2016 at 11:58 am

  Habari yako, diet uliotuma ni nzuri nataka kujua namna ya kutengeneza iyo juice

 14. joyce mallya

  September 15, 2016 at 11:44 am

  Mmmmmm iyo ya j3 mpaka j5!!!!

Leave a Reply