Uncategorized

JE UNAKOSA USINGIZI,TAHADHARI!!

By  | 
Tatizo la kukosa usingizi huenda likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya kusahau au ”Alzheimer” kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana maumbile yanayofananishwa na binadamu.
Vipande vya protini, kwa lugha ya kitaalamu (plaques) au uchafu kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti inayosababisha maradhi haya.
Taarifa zinazohusianaafyaUtafiti uliofanywa na kuchapishwa katika jarida la tafsiri ya matukio ya Sayansi, umeonyesha kuwa punde chembe chembe za uchafu ule ulipoanza kukua kwenye ubongo wa panya, usingizi ukaanza kuwa tatizo kwa viumbe hao.
Taasisi inayosimamia utafiti wa maradhi hayo, (Alzheimer’s Research UK) imehimiza kuwa ikiwa uhusiano huo unaweza kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa Madaktari.
Utafiti wa kutaka kugundua mapema kama mtu anaelekea kukumbwa na maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu katika kutibu maradhi hayo.
Wagonjwa hawaonyeshi dalili kupitia hisia au kumbukumbu zao hadi baada ya mda mrefu wa maradhi kumkumba mgonjwa. Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika kiasi kwamba tiba inakua vigumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana.
Ndiyo sababu wataalamu wanafanya juhudi za kuanza mapema kugundua kama mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa kabla ya dalili hizo kujitokeza.
Viwango vya protini ijulikanayo kama Beta Amyloid kimaumbile hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia panya katika kipindi cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini ambayo hujenga uchafu usiofutika kwenye ubongo na maradhi ya Alzheimer.
Majaribio yaliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Washington yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala kwa dakika 40 kwa kila saa mchana. Lakini ubongo ulipoanza kupatwa na uchafu panya hawa wakaanza kusinzia kwa dakika 30 pekee.Mmojapo wa wataalamu, Prof David Holtzman, alisema: “endapo mapungufu katika usingizi huanza mapema kiasi hiki katika ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo yanaweza kutupa ishara ya wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya.”
“ikiwa matatizo haya ya usingizi yapo, hatuelewi hasa yanachukua mfumo gani, kupungua kwa usingizi kikamilifu au ni tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu tofauti kabisa.”

Hata hivyo, utafiti unaofanyika kwa kutumia panya mara nyingi hayafai kutumika kwa binadamu kwa sababu nyingi zinazosababisha kutatizika na usingizi.
Dr Marie Janson, kutoka shirika la kujitolea Alzheimer’s Research UK, ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya matatizo ya kukosa usingizi na ugonjwa wa Alzheimer.
Aliongezea kuwa: “tayari umekuwepo utafiti unaounganisha mabadiliko katika usingizi huchangia katika matumizi ya ubongo kwa fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna uwezekano wa kuwa mapungufu katika usingizi pia inaweza kuwa ishara na onyo la maradhi ya kusahau au Alzheimer.
Kutoka bbc swahili.

6 Comments

 1. MOJAONE

  September 20, 2012 at 12:47 pm

  YOTE TISA KUMI RAHA YA USINGIZI UWE NA MWENZI WAKO UMPENDAYE USINGIZI UTAKUJA TU UTAKE USITAKE.

 2. Anonymous

  September 21, 2012 at 4:07 am

  hamnazo huyo,nje ya topiki,kipindi cha takeone hakirushwi tena?

 3. RUKY

  September 21, 2012 at 2:09 pm

  KUKOSA USINGIZI NI HATARI SANA MAREHEMU BABA YANGU ALIKUWA NA TATIZO HILO KABLA HAOWA DR WAKE AKAMWAMBIA AKISHA OWA LITAKWISHA KWELI AKAOWA NA KUPATA WATOTO MPAKA TUKA FIKA 7 NAKIPONDI CHOTE HICHO ALIKUWA BADO ANAHANGAIKA NAKUTAFUTA DAWA LAKIN WAPI..MPAKA KUNASIKU ALIVIMBA MPA USO KWA KUKOSA UZINGIZI KABISA NDANI YA WEEK MBILI C KWA MCHANA WALA USIKU AKATUAMBIA ANASHISI KM KICWA KINATAKA KURIPUIKA JINSI ANAVYOJISIKA VIBAYA,AKATOKEA MTU AKAMWAMBIA ANYOWE KIPARA ALAFU TUMUWEKEE MAJANI YA MPAPAI KWENYE KICHWA NA MAFUTA KIJIKO KIDOG NDANI YA PUA SEHEMU ZOTE MBILI HUWEZI AMINI ALILALA CK 3 MFULULIZO MPAKA AKAWA ANASHINDWA KUAMKA KULA BAADA YA HAPO HALI IKARUDIA TENA, TUKAJARIBU TENA HIYO DAWA HAIKUMSAIDIA TENA …SO IKAWA INAMPOTEZEA HAMU YA KULA NA KUDHOOFIKA MPAKA UTUMBO UKAJIKUNJA AKAWAHIWA KUFANYIWA OPARATION AKWA MTU WA KUUGUWA MARA KWA MARA MPAKA ALIPO FARIKI MOLA ALAZE MAHALI PEMA PEPONI

 4. Anonymous

  September 23, 2012 at 10:22 pm

  jaman clouds off line cku zote izo navopenda leotena plz ebu lipien kama ndeni la net joh kampun kubwa

 5. Anonymous

  September 24, 2012 at 1:31 pm

  Huo ni ugonjwa wa kurithi. Nimewahi soma kisa cha mdada aliyepata huo ugonjwa akiwa late 20s na alikuwa na wasiwasi kweli kuwa utampata kwa kuwa ndio ulomuua baba yake. Na kweli na yeye ukampata tena at a very young age wakati uwapata aged people. Na watoto wake wawili wana uwezekano wa kuupta ila wao waliapa kutokupima na kishi kwa negativity kama mama yao.

  Ni ugonjwa mbaya sana. Ni wa kurithi na uwapata wazee zaidi. Huyu dada yeye aliweka record ya mgonjwa mdogo zaidi. Nilisoma Yahoo.

  Yani inafikia mtu anasahau hata njia ya kwenda kwake.

 6. Anonymous

  September 26, 2012 at 10:34 am

  dina mbona hujanijibu kwani siku zina karibia za kwenda chuo kwani natafuta msaada wa mtu au kampuni la kunisaida mkopo wakusoma chuo kwani nimekosa mkopo na hali kwangu ni mbaya hakuna uwezo wa kujisomesha mwanzo nilikua nasomeshwa na serikali but now nimekosa mkopo wa chuo naomba unisaidie kuniulizia niweze kusoma kwa mawasiliano ni 0717175983

Leave a Reply