Uncategorized

JUISI YA MCHANGANYIKO WA EMBE,TIKITI NA MACHUNGWA.

By  | 
Kila siku asubuhi lazima nibebe juice ya kunywa nikiwa ofisini.Na juice yangu mie ni ile ya matunda matupu na maji kidogo bila SUKARI.
Juisi hii pichani ni ya mchanganyiko wa tikiti,embe na chungwa.Nikishaosha matunda vizuri kabisa nachukua kisu na kukata kata nyama ya tikiti na kuisaga kwenye blander nikiwa nimeweka maji kidogo nasaga na mbegu.Nina chujio kubwa yale ya juisi kisha nachuja japo unaweza usichuje pia.Nachujia kwenye bakuli kubwaa linalotosha vizuri.
Namenya embe 2 nakatakata kisha nayasaga kwenye blander ambayo naweka maji kidogo ili isagike vizuri.Nikimaliza nachujia mle mle kwenye bakuli nililoweka ile juisi ya awali ya tikiti kisha nakoroga vizuri.

Machungwa yanakuwa manne nayakamua juice yake pia. Kubwa ni kuwa makini mbegu zisiingie kwenye juice.Baada ya hapo nakoroga vizuri mchanganyiko huo ambao unakuwa mzitoo saafi tayari kwa kunywewa. Naifurahia juisi yangu japo sijaweka sukari lakini ni tamu kama nimeweka sukari.

14 Comments

 1. Anonymous

  September 5, 2012 at 5:55 pm

  Du inaelekea tamu sana hiyo juice jamani japo haina sukari.

 2. RUKY

  September 6, 2012 at 9:19 am

  THAT GOOD MPENDWA ITAKUPENDEZESHA MPAKA RANGI YAKO YA MWILI ITAZIDI KUWA NZURI…..

 3. MOJAONE

  September 6, 2012 at 10:21 am

  HATA MIMI NIMEACHANA SIKU HIZI NA MIJUICE YA POUDER SIJUI TANG NA NYINGINEZO NA NIMEGEUZIA UBAO KTK JUICE FRESH .. KTK MCHANGANYIKO WOTE LAZIMA PARACHICHI IWAPO.

 4. MOJAONE

  September 6, 2012 at 10:29 am

  HATA MIMI NIMEACHANA SIKU HIZI NA MIJUICE YA POUDER SIJUI TANG NA NYINGINEZO NA NIMEGEUZIA UBAO KTK JUICE FRESH .. KTK MCHANGANYIKO WOTE LAZIMA PARACHICHI IWAPO.

 5. MOJAONE

  September 6, 2012 at 10:29 am

  HATA MIMI NIMEACHANA SIKU HIZI NA MIJUICE YA POUDER SIJUI TANG NA NYINGINEZO NA NIMEGEUZIA UBAO KTK JUICE FRESH .. KTK MCHANGANYIKO WOTE LAZIMA PARACHICHI IWAPO.

 6. MOJAONE

  September 6, 2012 at 10:29 am

  HATA MIMI NIMEACHANA SIKU HIZI NA MIJUICE YA POUDER SIJUI TANG NA NYINGINEZO NA NIMEGEUZIA UBAO KTK JUICE FRESH .. KTK MCHANGANYIKO WOTE LAZIMA PARACHICHI IWAPO.

 7. Anonymous

  September 6, 2012 at 12:32 pm

  aksante kwa kushea na sisi jambo jema kama hilo, na mimi ntaanza kunywa juice ya bila sukari, thanks mummy

 8. Anonymous

  September 6, 2012 at 4:05 pm

  hiyo packing "maji ya kilimanjaro "(chupa) ndo kidogo haijaleta mvuto.
  idea, content are all good. hakuna containers zenye mvuto? inakua kama juis za darajani bhana.

  ni mtazamo wangu!

  mdau znz

 9. Mariam irankunda

  September 7, 2012 at 11:54 am

  Dina kabla yayote naanza na salam na tena na wapongeza kwa kazi yenu nzuri yakuelimisha jamii na ku wasaidiya watu wakiwa na matatizo mm ni msikilizaji wenu mzuritu wa vipindi vyenu kama vile leo tena hekaheka napenda kusema tu asanteni sana kwa kazi zenu na mungu azidi kuwapa moyo kama huo nimimi msikili zaji wenu mariam irankunda nawapenda sana sana ww geya habibu na zamaradi

 10. Anonymous

  September 7, 2012 at 1:16 pm

  Ntaijaribu hii, hapo kwenye machungwa unakamua 2 kawaida au ulimaanisha kuyasaga pia kwenye blander?
  Asante

 11. Anonymous

  September 7, 2012 at 4:11 pm

  Safi sana Dina mdogo wangu. Ila ushauri wangu wa bure …nunua contena special la kubebea hiyo juice; hata chupa za watoto wa shule ni better; nachoogopa ni kuwa hizo chupa za maji unazotumia hazikutengenezwa kwa ajiri ya ku re use…utakunywa sumu bure upate kansa.

 12. Anonymous

  September 8, 2012 at 9:21 am

  Ni kitu kizuri Dina<ila ushauri tafadhali tafuta chupa maalum kwa juice,usiweke kwenye hizo za maji,yaweza kuwa kontiminetedi ukapata fudi poizoni bure.

 13. Anonymous

  September 13, 2012 at 2:57 pm

  Nimekupendaje Dina…unaweka both comments…hata zenye kukuchallenge. Utafika mbali kwa hiyo tabia. Maana wabongo wengi hawapendi kuwa challenged ndo maana hawa learn

 14. Anonymous

  October 4, 2012 at 7:15 am

  nice dina, kama yamekuingia naomba tuonyeshe kuwa umekubali idea za wapenzi wako, tuwekee picha nyingine ya juice ikiwa katika container yake ili na sisi tujisikie kuwa huwa unatusikiliza na kufanyia kazi ushauri wetu kama sisi tunavyokufuatilia mafunzo yako na kuyafanyia kazi yale yaliyo ndani ya uwezo wetu…. tuoneshe upo pamoja nasi basi shost,, picha ya container ya juice plzzzzzzz

Leave a Reply