Uncategorized

NI KWELI KWAMBA WASICHANA WA SIKU HIZI HAWAJUI KUPIKA??

By  | 

Nilikuwa namsikiliza Bi Ponza juzi anasema wasichana wa sasa hawajui kupika kabisa.Wengi wanaendekeza urembo sanaaa lakini kupika hawajui,ni kweli??
Nimekuwa nikisikia ili umkamate mwanaume pamoja na mautundu mengine uwe unajua kumpikia mahanjumati.Hivi ni kweli katika maisha tuliyopo wanaume wanajali sana kuhusu mapishi au mwanamke anaempikia madikodiko??

16 Comments

 1. Anonymous

  September 10, 2012 at 4:57 am

  Dina hilo lina ukweli kwa maana wadada wengi wanajisahau wanafikiria kujipodoa na mambo ya kitandani tu,lakini inapaswa na mapishi pia wazingatie maana kila siku baba anakula chakula cha housegirl ukiuliza eti wako bize na kazi bac hata hiyo jumapili kila kitu ni dada wa kazi,tubadilike jamani….

  • Anonymous

   September 10, 2012 at 8:47 am

   Wasichana wa siku hizi ni wavivu, viburi na nyumba chafu wanapoishi. Ukiwaona mjini wanang'aa nadhani wanaogopa kucha za kubandika zisidondoke na zisiungue wakipika.

 2. mzushi

  September 10, 2012 at 7:44 am

  me naona utandawazi umezidi kani kwa jamii ya sasa mdada wa chuo hajui hata kupika ugali kwa madai kuwa eti ye hapendi kuula so kwanini ajue jinsi ya kuupika. SO MY DEAR SISTERS YOU GOT TO CHANGE.

 3. Anonymous

  September 10, 2012 at 8:32 am

  Hiyo ni kweli kabisaaa Dina. Huoni hata barabarani? Mdada mwambie kuna msusi mzuri wa brazillian aaaaahh, atakwenda hata kama ni Bagamoyo. Waume zao wala hawajui mara mwisho kuwapikia msosi ni lini.

  Wanaume wengine hawana matatizo ya kula hata akipika nani mradi kimeiva tu lakini wadada nao wasichukulie kama ndo loop hole. Mwanamke unatakiwa utenge muda wa kuipikia familia yako hata mara mbili au tatu kwa wiki especially mumeo akiwepo.

  Mimi

  Wengi wanafikiri eti ukiwa na mautundu, mzuri wa sura na vikorombwezo vingine ndo wamemaliza. Wapiiii, mtabebewa hadi mkome.

 4. RUKY

  September 10, 2012 at 9:07 am

  ASIKWAMBIE MTU DINA MWANAMKE KUPIKA, NA MWANAUME HUWA ANAJSIKIA VIZURI KUPIKIWA NA MKE WAKE. SEMA WANAWAKE TU WA WANAOJIITA WA MUJINI HAWAAMINI HIVYO WANADHANI MUONEKANO WAKUVAA VIZURI TU NDIYO ISHU… NA KWELI KABISA WADADA WA SASA HAWAJUI KIPIKA MPAKA AIBU

 5. Anonymous

  September 10, 2012 at 9:37 am

  Hii ni kweli kabisa, mwanaume ni mapishi na hayo ya urembo na mapenzi yanafuata. mwanaume ukimpikia vizuri ataenda kote lakini lazima arudi kwako kula chakula chako. me mume wangu hata tukigombana jumapili lazima tu reconcile kwasababu ndo cku niko home na jikoni nasimamia show me mwenyewe.

 6. Anonymous

  September 10, 2012 at 11:33 am

  jiko muhim kwa mwanamke sio tu huku hata ulaya ukikaa na wazungu ukakuta mwanamke hajui kupika then mwanamke wa kiafrika unapika basi lazima mwanaume atalizungumzia hilo na kwa afrika ndio muhim sana hata kama utakuwa mzuri kama malaika kupika ni kigezo kikubwa sana kwa mwanaume tena akiwa anakula chakula kizuri hawez kuwaza mwanamke wingine hata angekuwa anampa nn ni mahaba watu wa pwani tunasema yani mwaname ataona tofauti yako na mwanamke mwingine yyote kupitia mapishi

 7. Anonymous

  September 10, 2012 at 9:49 pm

  Yaani siku hizi ni hasara tupu kwa wadada tunaowaoa miaka hii.Tangu mambo ya kujiremba yatokee akili zao zote ni kutafuta namna ya kubadilisha maurembo kichwani mikononi,miguuni masikioni,shingoni kopeni,nk.Dina ukitaka kuhakikisha hilo jaribu kufikiria mara nyingi unapokutana na akina dada wenzanko mahali popote unapoweza kujumuika nao huwa wanaongelea nini hasa? Jibu ni maurembo tu, mara umesuka wapi, mara umenunua wapi hiki na kile nk.Hakuna anayeulizia mambo ya mapishi maana hayo yamewapita kisogoni.

  Pia, mtindo wa kuwa na wasichana wa kazi majumbani kwa wazazi kumewafanya wasichana wengi wanapokua kwa wazazi wao tangu wanazaliwa ,wanakua, wanaenda shule, chuo nk wanakuwa wanafanyiwa kila kitu na hao wadada.Kuna wengine ambao wanasoma karibu na nyumbani hata kama yuko bweni huwa wanarundika nguo hadi kuzipeleka nyumbani zikafuliwe na dada wa kazi.ndio maana hata wengine wanaokufua wala kupiga pasi.Kama huamini hebu jaribu kuchunguza viazo vingi vya vurugu katika ndoa huanzia hapo baada ya mwanamke kutojiweza kila kitu na kuachia kila jambo mikononi mwa mdada wa kazi.kwa nini nisimpende anayenifulia, nipikia na kunipelekea maji bafuni jamani?

  Wadada wa siku hizi wengi mzigo tu, na tena ukioa waliokulia nyumba zileeee za hali fulani ambapo pana wadada wa kazi wasiopungua wawili, watatu ndo kabisa hata wanaume ni tabu tupu hawajui wajibu wao kwa wake zao,wao ni kudai starehe tu.Nayasema haya kwa uthibitisho kabisa, ningekuwa naongea ana kwa ana na wewe ningekutajia majina elefu kidogo.

 8. Anonymous

  September 11, 2012 at 1:12 pm

  kweli tupu

 9. Anonymous

  September 11, 2012 at 8:46 pm

  The only way to wins a man's heart is through his stomach, talkin with experience ha ha ha ha watajibeba wasiojua kupika kazi ipo, wanadhani kupika ni kitandani tu imekula kwao!

 10. Anonymous

  September 12, 2012 at 2:38 pm

  Kweli mwanamke kupika m ma hubby daily anakula chakula nchampikia kazi kwenu mnaoendekeza urembo

 11. Anonymous

  September 13, 2012 at 4:40 pm

  Hayo nimeyaona sana na kwa wengi huku ughaibuni wadada wa kibongo hawajui kupika aiseee du! wakati wa sherehe za pamoja kina mama wanapoagizana kupika hao wadada warembo utawaona wanakimbilia kuleta matunda au kachumbali,na wengine kusingizia kukosa muda kumbe hawajui kupika.Sasa cha ajabu,wakati wa kula ndio wa kwanza kushambulia mabeseni waliopika wenzao.Yaani ukiwaona wengine walivyo warembo na wametoka familia za kujiweza utawahurumia kuona hawajui kupika na ndio maana wanaume wengi wanawa-date miaka na kuwaacha wamewala na kuwamaliza baada ya kugundua ni mzigo tu.Na huu uzungu wa kuingia jikoni wanaume ndo kabisaaaaaa wanalaza miguu juu.Na kuna wanaume wameishaolewa na wake zao, kila chakula kikihitajika mgeni kafika kama ndugu utaona mwanaume anaingizana jikoni maana mkewe ni pambo la sebure yeye ni kuangalia na TV na kubadilisha chanels kwa kwenda mbele.Kina dada kama mnasoma hizi comments mjirekebishe kwani ni hatari sana kwa mtindo huo.tena kama huku ughaibuni hakuna taabu kupika ni kuturn on jiko mambo yanaenda. Je ungekuwa bongo ambako lazima uchochee mkaa na umeme wa shida ndio mngelala na njaa au kushinda hotelini/mgahawani kila siku.

 12. Anonymous

  September 14, 2012 at 5:24 am

  Me nadhani wanaume wanatofautiana interests. Mimi nilikuwa mpenzi sana wa kupika madikodiko but mume wangu amenifanya sipendi tena kupika sababu mara nyingi anarudi home late keshakunywa pombe zake na michemsho au nyamachoma za bar, so msosi wako wa home hali au anagusa tu ili kutoa lawama, nikajionea ujinga huu nimeacha, siku hizi tunakula cha housegel tuuu…….. ha ha haaa

 13. Anonymous

  September 17, 2012 at 11:23 am

  Nilikuwa siamini kama wanaume wanapenda kupikiwa na wake zao nilikuja kugundua nilipoanza kusoma masomo ya jioni, Mr akawa hana raha ya chakula pindi chakula kikipikwa na dada wa nyumbani, mpaka siku akaniambia "Plz mboga uwe unapika wewe at least wali utapikwa na rice cooker" So wadada nashauri mzoeshe mume kula chakula kilichopikwa na wewe mke kuzidisha umuhimu wako kwake.

 14. Anonymous

  September 17, 2012 at 6:46 pm

  Wala tusijidanganye .wanaume .hawajui .wanachotaka .tudinge tusinge tongozwa wala kuolewa .hwajitambui .utapikaweeeee .na atakutenda .

 15. Anonymous

  December 10, 2012 at 12:09 pm

  MEN ARE VERY INTERESTING CREATURES KWA KWELI ,MY HUBBY LOVES FOOD SO MUCH NA MOST TIMES ITRY COOK FOR HIM BUT SIONI KAMA NINGEKUWA SIO MREMBO ,NA SIJUI MAUJANJA NINGE MKEEP SO UKWELI NI KWAMBA THIS THINGS GO HAND IN HAND LAZMA UWE MREMBO KIDOGO ,MAJAMBOZZZZ ,NA UJUE KUPIKA AT LEAST HIS FVRT DISHES.
  SO NYIE MNAO ZANI KUPIKA TUU NDO SHUHULI YENYEWE UNAJIDANGANYA TRY AND BALANCE EACH AND EVERYTHING UTANIAMBIA

Leave a Reply