Uncategorized

NYWELE ZA SALIMA NI NYEPESI SANA ANAOMBA USHAURI AFANYEJE ZIWE NZITO???

By  | 

Mambo Dina?

Hope ur okay. nahitaji msaada wako tena
nilishawahi kuomba nisaidie dawa nzuri ya mba sababu nilikuwa nasumbuliwa mno
mba hadi ikawa kero katika vitu nilivyoshauriwa kutumia nilichagua mafuta ya
nywele ya radiant na shampoo ya zinoral kweli vimenisaidia mno kwani tatizo la
mba kwangu halipo tena.

Kilichonifanya nirudi tena kwenu ni kuwa nywele zangu hazina
mvuto kabisa, zipo very weak, nyepesi. nilishaacha kutia dawa kama mwaka
umepita lakini wapi. naomba kama kuna yoyote anayejua dawa nzuri ya kusaidia
hili tatizo aniambie au kama kuna sehemu naweza kwenda kupimwa na nikapata
suluhisho la tatizo langu nitafurahi maana sasa nimekuwa mtu wa kuvaa mawigi tu
hata kusuka siwezi maana naogopa zitaishia kukatika nywele.

 NISAIDIENI PLEASE NAMI NIWE NA NYWELE NZURI NA ZENYE AFYA
KWANI MWANAMKE NYWELE BWANA.

asante

Salima

18 Comments

 1. Anonymous

  September 15, 2012 at 8:17 pm

  KWAKO SALIMA,
  JARIBU HENNA MBICHI KWENYE NYWELE INASAIDIA KUFANYA ZIWE NZITO. ILA UWEKE MAFUTA MENGI JARIBU ALMOND OIL KWASABABU HENNA INAKAUSHA NYWELE. DAWA USIWEKE ZINAHARIBU NYWELE. NA UKICHANA HAKIKISHA ZIPO MBICHI NA ZINAMAFUTA, USICHANE NYWELE KAVU. USIKAUSHE NA MOTO ACHA TU ZIKAUKE ZENYEWE.

  KILA LA HERI
  LAILA

 2. Evelyn F

  September 16, 2012 at 8:54 am

  tumia radiant steaming au marrow, na waweza tumia zote pia, na kama ukitaka dawa ya nywele nzuri kwa nywele zako, tumia smooth organic, ni dawa nzuri sana, nlikuwa na tatizo kam,a lako, ila kwa sasa, ninaringa hadi naweka purple kwa my nywele

  jarib RADIANT STEMING, ipo kwenye kichupa cha blue hivi na yenyewe ndani ni nyeupe, chupa yake ipo kama ya lotion au shampoo hivi, na Marrow utakuwa unaifahamu pia…………………ALL THE BEST
  Evelyn F

 3. Anonymous

  September 17, 2012 at 10:29 am

  Salma
  Polee sana,kweli mwanamke nywele bwana
  Sasa nenda kwa watu wa GNLD wakupe kirutubisho kinaitwa GROWTH kinajaza nywele sana na pia kinakuza nywele nakuzifanya ziwe nzito.
  Kila ila kheri

 4. Anonymous

  September 17, 2012 at 12:23 pm

  dear Salima, ukitaka nywele ziwe nzuri kwanza kabisa kila ukiretouch hakikisha unakata ncha, osha nywele zako hata mara mbili kwa wiki, nywele inapoota retouch na sio kuzisuka mara kwa mara,na usiache kufanya steaming mara kwa mara, na kama unaweza hakikisha shampoo na conditioner ni vyakwako na sio vya salun maana wakati mwingine ndo vinachanganywa na omo ndio nywele zinazidi kuisha

  • LADY G

   September 18, 2012 at 9:18 am

   MIE NAFANYA KAMA DADA ALIVYOSEMA HAPO JUU NAFANYA STEAMING KILA WIKI,NATUMIA VITU VYANGU MWENYEWE LAKINI STIL ZINAKUWA CHACHE SNA NIKI RETACH NATUMIA PROFECTIVE KUANZIA DAWA, STEAMING,MAFUTA,SHAMPOO NA NAKATA NCHA KILA NIKI RETACH NA MIMI NIFANYEJE,KABLA YA PROFECTIVE NILIKUWA NATUMIA O LIVE OIL PRODUCT,NIKAWA NABADILISHA STEAMING KAMA HENNA,MAYONISE,HONEY AND WHEAT,COLESTRAL NI BAADHI YA STEAMIN AMBAZO NIMESHAWAHI KUTUMIA

  • Rida

   September 18, 2012 at 2:35 pm

   du mpaka hapo umezioverprocess nywle zako kwa kufanya steamning kila wiki. ujasema unaritoucher baada ya muda ngani? kwa ushauri unatakiwa kureoucher baada ya siku 40- miezi 2 katika hapo, piaswala la ncha ni muhimu vip muwekaji wa dawa? maana hao nao nitatizo lingine, kwa muda wangu ni mdogo sana naomba kesho nikipata nafasi ntakushauri njia bora coz ninautaalam wa mwenye kwa miaka 15

  • Anonymous

   September 19, 2012 at 7:36 am

   Lady G, watu wengi hawajafahamu ila profective ni dawa kali kwa watu wenye nywele nyepesi hivyo ukitumia zinazd kuwa nyepesi na chache kabisa…huwa inafaa kwa watu wenye nywele nzito. Olve oil ndio yafaa mimi nilikuwa kama wewe ila baada ya kuanza kutumia olive oil naona mabadiliko ya uzito wa nywele. na pia kwenye kufanya steaming jitahd uwe na dawa moja tu usibadilishe mara kwa mara kwahyo chagua moja na endelea nayo hiyo hiyo. kila la kheri

 5. Anonymous

  September 19, 2012 at 9:27 am

  kwa kweli nywele hazina fomula, kitu kimoja kinaweza kumsaidia huyu na si lazima kimsaidie mwingine, tatizo hatuna madaktari wa nywele kama ilivyo malaria na magonjwa mengine. waliobaki ni makanjanja ili mradi tu kilimsaidia yeye basi anadhani tatizo lake litakuwa kama la SALIMA. Kwa mtingo huu wa huyu alitumia hiki na yule kile dada Salima utaendelea kufanyia majaribio kichwa chako kitu ambacho si kizuri.

  Mimi ushauri wangu dada SALIMA kata kabisa nywele zako tena ikiwezekana KIPARA kisha ngojea ziote ndo uanze kusuka upya na usikimbilie kuweka haya madawa WAZUNGU hawatupendi ngoja madhara ya haya madawa fainali uzeeni a.k.a baadae ndo maana hata vizazi vinapofuka siku hizi wadada kushika mimba inakuwa ngumu.

  • maisa jmary

   May 17, 2016 at 11:51 am

   kabisa yaani kama mimi nshaangaika mpka basi

 6. flora

  September 19, 2012 at 1:52 pm

  flora!!!
  jmn mi mwenyewe swala la nywele linanidhoofisha yn nywele zangu chache,nyepez na zna katika mno nisaidien

 7. Anonymous

  September 20, 2012 at 12:44 pm

  Dina naomba ushauri nahitaji kupata mtoto wa kiume na mzunguko wangu ni wa siku ishirini na nane please wadau nisaidieni mnaojua.

  • Anonymous

   May 31, 2013 at 8:23 am

   Dada nakuomba umtangulize MUNGU kwani yeye ndio kila kitu anaweza kukupa hitaji la moyo wako,Mwanadamu anabahatisha tu,

 8. lady g

  September 20, 2012 at 2:06 pm

  asante RIDA ila uwa nina retach baada ya miez 3 kabla ya profective nilikuwa natumia olve oil lakini mambo yalikuwa ni yale yale nywele zinakuwa chache sna na profective sasa hivi hii ni mara ya pili

 9. Anonymous

  May 31, 2013 at 8:12 am

  Anonymous:- Nakuomba kwamaswala ya mtoto wa jiansia gani mtangulize MUNGU kwani yeye ndio kila kitu, mwanadamu anabahatisha. kaka yangu ni doctor na mke wake ni doctor lakini hadi leo hawajapata mtoto wa kike.

 10. Anonymous

  June 6, 2013 at 10:42 am

  mnaenda nje ya mada kwani kuna watu wanatafuta watoto bila mafanikio hawakuweka dawa kichwa wala kutumia makemikali jamani tuombe tu mungu atupe afya njema.

 11. Anonymous

  August 27, 2014 at 6:57 pm

  Dada naomba ushauri nina nywele za asili yani sijaweka dawa hahitaji ushauri nitumie mafuta gani mazuri na stimng gani ili zisikatike na kuharibika.

 12. Anonymous

  December 16, 2014 at 9:07 am

  ushaur wang km azjaota wait zioteote ndo uretouch na ucpende badilisha dawa mafanikio cku zote ayaj Kwa haraka km tunavyoyaitaj so settle na dawa moja km mwaka ndo uchukue maamuz ya kubadlisha mm nlkua natumia dawa ya beutful begginin mwazon nkaanza kuona nywele znazid kuisha znakua chache nkaamia Kwa olive oil nayo yabox mwanzon mabadiliko ckuyaockuyaona BT ss HV nywele zng ni ndefu na zenye afya ,BT hapa pia inategemeana na aina ya nywele km ushajua nywele zako nyepes uctumie vtu vya kulainsha zaid km steam in ya mayonise aifai Kwa nywele nyepes anza olive oil dawa ya box na steam in ya korestral mafuta ya radiant ndo utumie utaona mafanikio

 13. maisa jmary

  May 17, 2016 at 11:48 am

  duuh me ndo nashindwa kabisaa cha kufanya nywele yangu inakuwa nyekundu na inakatika natumia organ oil dawa, steaming natumia marrow na radiant na lotion natumia oliver oil bt waaapiii!!?

Leave a Reply