Uncategorized

WAPI ZINAPATIKANA SIDIRIA ZA MWANAMKE ALIYEKATWA ZIWA MOJA?

By  | 
Hello Dina,
Habari ya utendaji wa majukumu ya kila siku.
Mimi ni msomaji mzuri wa blog yako uwa napenda kusikiliza vipindi redioni lakini bahati mbaya sina muda mara nyingi nakuwa katika ajira za watu.
Mimi ninashida nimejaribu kuzunguka maduka mengi nimekwama sasa, natafuta blazia za mtu aliyekutwa na saratani ya ziwa akakatwa ama ziwa la kushoto au kulia.
Naimani kupitia blog yako naweza kupata mwanga kwa hapa nyumbani Tanzania, Dar es Salaam ntaweza kuzipata wapi.
Please nahitaji msaada wenu.
Mhitaji

3 Comments

 1. MOJAONE

  September 25, 2012 at 9:13 am

  Pole Dada .. hivi hizi Braa zinakuwa na ujazo sehemu mmoja ili kuziba pengo la ziwa lilokatwa au inakua patupu?
  Ili nasi tujui tu.

 2. Anonymous

  September 26, 2012 at 9:15 am

  Hi dada

  Pole ila hapo ocean road ukiulizia utapata sio sidiria kuna kitu wanatoa kinafanana na titi unaweka upande uliokatwa titi moja,Coz mie nina mama yangu mdogo alikatwa ziwa na hicho kidude alipata hapo hapo ocean road kuna kikundi cha wamama ambao wanauza na hata bra wanauza ila zina sehemu zote mbili km bra za kawaida tu kwa kipindi kile walikuwa wanauza elf 15 kwa sasa sijajua wanauza kiasi gani

  Ukiweka mtu hawezi kukujua kama umekatwa titi anajua unayo yote mawili.

 3. Anonymous

  September 26, 2012 at 1:21 pm

  Dina pole na kazi na majukumu ya kila siku.
  Nashukuru sana kwa kupost msg yangu na kuniulizia kwa wasikilizaji wa leo tena. Nilipokuwa nikisikiliza kipindi pindi unatangaza nilikuwa na mama mmoja akaniambia hakuna blazire ila kuna matiti ya bandia. Nashukuru amenielekeza nimeenda sehemu husika katika taasisis ya Saratani ya Matiti mwananyamara jengo la S&F House, ghorofa ya kwanza nimepata maelekezo mazuri na ya kuridhisha sana.
  Mungu akubariki kwa kujali jamii inayokuzunguka,
  Asante sana wote.
  Kazi njema na kila kheri.

Leave a Reply