Uncategorized

WEWE UNGEFANYAJE?ni kichekesho tu lakini!

By  | 
Mdada mmoja mke wa mtu alikuwa akisumbuliwa sana na jamaa mmoja aliyekuwa akimtaka kila siku, hatimae akamwambia mumewe. Mume akamwambia mkewe, we kubali tuu, ila mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu.
Mdada akafuata masharti ya mumewe na hatimae wakaingia chumbani na yule bwana , mumewe akiwa tayari na panga uvunguni mwa kitanda. Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona ana makovu makubwa kifuani na mgongoni;
MKE: Heee mbona una makovu hivyo??
JAMAA: Niwe mkweli tuu, kwako dia!! mie nina tatizo sana la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania, nilishafumaniwa mara kumi na tisa, na wote walionifumania niliwaua. Ila jaribio la mwisho nilidakwa na mapolisi nikatumikia kifungo cha miaka 27 jela, Lakini ninavyopenda wake za watu sitaacha kuua. Hivi sina muda tangu nitoke huko jela hivyo nina ukame wa punda na nilipokuona moyo wangu ukakudondokea. Na nitatulia na wewe.
MKE: Heee! Haiwezekani jamani!!….jamaa akaendelea kuvua nguo alipomaliza mdada akaanza kujitahidi kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni aje kumuokoa, mume akabana kimya, kila mdada akijitihadi kupunga mkono hakupata jibu, mdada akalalamika kwa maumivu makali mpaka jamaa akamaliza shughuli zake akatokomea.
MKE: Huku akilia, ndio nini umenifanyia? Mbona hukutoka??
MUME: We we we, Weeeee mama naniii!!.. mwenyewe umesikia keshaua 19 ulitaka niwe wa ishirini?
 

22 Comments

 1. Anonymous

  September 25, 2012 at 3:42 pm

  ahaaahahaha

 2. Emmie

  September 25, 2012 at 4:21 pm

  Huyu mwanaume nae hana mapenz yakweli maana angetafuta hata cha kufanya il amsaidie mkewe.

 3. Anonymous

  September 25, 2012 at 6:39 pm

  kumbe na wewe dada dina una sifa za ukomedy hongera sana yani nimecheka hadi mbavu zimeniteguka shauli yako itakubidi unichangie matibabu yaani sipati kusema haya bwana – mdau wako richie wa ughaibuni

 4. Anonymous

  September 25, 2012 at 7:06 pm

  Tehe tehe teheeee…. Nimechekaje!

 5. MOJAONE

  September 26, 2012 at 4:13 am

  Duu!! Dina .. NIMEISOMA MADA HII KWA JAZBA KUBWA NIKITEGEMEA NITAJIFUNZA KITU UKIZINGATIA KUWA NAMI NI MWIZI MKUBWA WA WAKE ZA WATU LKN MIE HUWA SIUWI NA SIJAWAHI KUFUMANIWA, MWISHO NAGUNDUA KUWA NI FIX TU, TENA IMEMTOA KIFUA MBELE MABEGA JUU NA MAFANIKIO MAZURI YA ZOEZI HILO LA MWIZI.

  EVERY THING CAN GO SMOTHLY ONLY IF YOU KNOW HOW TO ANSWER.

  • Majoy wa majoyy.blogspot.com

   September 28, 2012 at 11:53 pm

   Hahahahhaaaa One ipo cku yako utabambwa ndo utakoma lol

 6. Anonymous

  September 26, 2012 at 5:56 am

  umenifurahisa kwa kweli dd dina umenifanya siku nione nzuri asbh asbh kwa kuingia ktk blog yk jmn binadam kwl tuna vituko

 7. Catryn

  September 26, 2012 at 7:36 am

  Ha ha ha, so funn! Ila mmhh!!

 8. Anonymous

  September 26, 2012 at 9:19 am

  Hi Dina

  Hii kali sasa huyo mwanaume angemfuatilia kwanza kujua ni mtu wa aina gani yy kamruhusu tu mkewe eti aje haaaaa pole yake mie nadhani tungeachana na huyo mume siku hiyo hiyo kwa kuogopa kupambana na mwanaume mwenzie so kamuachia maumivu mkewe kwa kuingiiwa na jitu lenye ukame kwa muda wote huo haaaaaaaaaaaaa

 9. gosbety

  September 26, 2012 at 10:11 am

  Kama alivyofanya huyo jamaa na mimi ningefanya hivyo hivyo kwani nini bana si kwa siku moja tu hakuna mbaya, ningekaa huko chini mpaka jamaa atapomaliza haja yake japo roho ingeniuma sana mke wangu kufanyiwa kitu km kile huku nikishuhudia. Mweeee!

 10. Anonymous

  September 27, 2012 at 5:50 am

  duuu jamaa kaonyesha udhaifu kinoma kwa mkewe hata aminiwa tenaaaaaaaaaaaa

 11. Anonymous

  September 27, 2012 at 6:18 am

  Hahaha hahahah Dina umeitoa wapi hii maana ni kali. Nimecheka hadi nikasahu kama kesho nina mtihani. Kweli duniani kuna vituko!

 12. Anonymous

  September 27, 2012 at 9:29 am

  Huyu mwanaume hakuwa makini kwa sbb alitakiwa ajue kwanza mgoni wake anaonekanaje….unaweza jitu la miraba nane, kwa nini aamue kwenda kujificha chni ya uvungu? anyway ni kichekesho kizuri!!

 13. MOJAONE

  September 27, 2012 at 11:33 am

  HAPO NDIO UJUE DINA KUWA WENGINE SIO MADUME NI MIDUMEDUME.
  ANGALIA KTK UCHAGUZI WAKO USIJE UKAANGUKIA MIDUMEDUME.

 14. Anonymous

  September 27, 2012 at 1:41 pm

  huyu mwanaume hana mapenzi na mke wake, mwanaume mwenye mapenzi ya dhati yupo tayari kufa kwa ajili ya mke wake

 15. Anonymous

  September 27, 2012 at 6:54 pm

  hahahaha,mwenye mke alitakiwa apambane kwa ajili ya mkewe sio kuogopa na kukaa akisikilizia mwezie anaumizwa.

 16. Anonymous

  September 28, 2012 at 10:42 am

  hahahaahhaah kufa mchezo kwiiiiiiiiiiiiiiiii

 17. Anonymous

  September 30, 2012 at 7:13 am

  huyo dada kumkomesha mumewe akakubali tu kitendo asiumie masikini ila kweli kuuliwa bora niwe kimya

 18. Anonymous

  September 30, 2012 at 9:05 am

  Mi naona mke na mume wote wapumbavu. Kama mama angekataa kufanya chochote na huyo mbaba then angeepusha aibu ambayo imempata. Ujinga mtupu

 19. MOJAONE

  September 30, 2012 at 11:12 am

  MAJOY .. USINIOMBEE MABAYA.
  HATA HIVYO NIPO NJIANI KUTUBU BAADA YA KUPATA JIBU LA TUPO WANGAPI.

 20. Anonymous

  October 1, 2012 at 8:07 am

  ha ha ha ha ha ha..bo bo bo bonge la storyy

 21. Anonymous

  October 1, 2012 at 8:08 am

Leave a Reply