Uncategorized

MKURUGENZI MKUU WA MSD ASIMAMISHWA KAZI

By  | 


 

  

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dkt.
 Hussein Mwinyi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini
Dar es salaam kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia
kubainika kwa matumizi ya dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi
zenye jina la Biashara TT –VIR 30
.

Mmoja wa maafisa kutoka Mamlaka
ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) ambaye hakutaka jina lake liandikwe
kwenye vyombo vya habari akiwaonyesha waandishi wa habari Dawa badia za
kupunguza makali ya Ukimwi (ARVS) zilizoondolewa katika vituo vya
kutolea huduma mara baada ya kugundulika.

Makopo ya dawa za kupunguza makali ya
Ukimwi yakitofautiana vifungashio. Kopo la kwanza kushoto linaonyesha
dawa halisi ya kupunguza makali ya Ukimwi iliyokidhi viwango ikifuatiwa
na makopo 3 yenye dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi yenye jina
la biashara TT –VR 30 toleo namba 0c.01.85 yaliyotengenezwa na kiwanda
cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd. (Picha na Aron 
Serikali imewasimamisha kazi
mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) ,Mkuu wa kitengo cha
Udhibiti na Ubora na Afisa Udhibiti Ubora wa ohari hiyo ili kupisha
uchunguzi dhidi yao kufuatia kuruhusu kusambazwa kwa dawa bandia za
kupunguza makali ya UKIMWI aina ya TT –VIR 30 katika vituo mbalimbali
vya kutolea huduma za afya nchini.
Aidha imepiga marufuku usambazaji
na matumizi ya dawa aina ya TT –VIR 30 toleo na 0C .01.85
inayotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd
(TPI) kufuatia dawa hiyo kutengenezwa chini ya kiwango na kutofaa kwa
matumizi ya binadamu.
Akizungumza leo jijini Dar es
salaam Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema
kuwa hatua hiyo imechukuliwa mara baada ya kubaini kuwepo kwa dawa
bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi katika hospitali ya wilaya ya
Tarime kufuatia ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya
Chakula na Dawa nchini (TFDA).
Amesema kuwa ukaguzi na uchunguzi
wa kimaabara dhidi ya dawa hiyo isiyokidhi viwango ulibainia kuwa
nyaraka zilizopo kuhusiana na dawa hizo unaonyesha kuwa Kiwanda cha
Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) waliiuzia Bohari ya Dawa
(MSD) dawa hiyo bandia toleo namba 0C. 01. 85 iliyotengenezwa nchini
mwezi Machi 2011 na kuonyesha mwisho wa matumizi yake mwezi Februari
2013.

Amefafanua kuwa dawa hiyo bandia
ilikua na dawa zenye rangi mbili tofauti njano na nyeupe na kuwa na
viambata tofauti vilivyopaswa kuwepo aina ya Efaverenz badala ya
Niverapine, Lamivudine na Stavudine na kuongeza kuwa vidonge
vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikua tofauti na
vifungashio vilivyosajiliwa na TFDA.

Dkt. Mwinyi amesema kuwa serikali
inahakikisha kuwa dawa zenye ubora unaotakiwa za kupunguza makali ya
UKIMWI zinaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma kote
nchini na kuwaagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya na kamati za dawa na
Tiba katika vituo vya huduma za afya kuhakikisha kuwa zinapokea,
kuhakiki na kusimamia kikamilifu ubora na matumizi sahihi ya dawa na
vifaa tiba nchini.

Kuhusu upatikanaji wa dawa hizo
amewatoa hofu wananchi na kuwahakikishia kuwa dawa za kutosha zenye
viwango stahili zitaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma
za afya nchini na kuwataka wananchi kutoa kushirikiana na mamlaka husika
kwa kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa dawa zenye ubora wenye
mashaka au uvunjifu wa sheria inayosimamia ubora na usalama wa dawa.

4 Comments

 1. Mie

  October 13, 2012 at 12:19 am

  ndiyo maana mie najilia dawa ya mitishamba sijawahi ugua hata mafua tangia nijijuwe nimeadthirika na niliziogopa baada ya kumuona ndugu yangua wakaribu akipata ugonjwa wa moyo kwa hizi dawa za HIV na bado akawa haishi kulazza hosp. na kingine ni kula vizuri basi na wala ukiniona huwezi jua..na tangia nijijuwe na kuanza kutumia hii dawa ya mitishamba ni miaka 5.. poleni wagonjwa wenzangu kila jambo lina sababu, na c kila muadhirika kaupata ktk uzinifu

 2. Mie

  October 13, 2012 at 12:19 am

  ndiyo maana mie najilia dawa ya mitishamba sijawahi ugua hata mafua tangia nijijuwe nimeadthirika na niliziogopa baada ya kumuona ndugu yangua wakaribu akipata ugonjwa wa moyo kwa hizi dawa za HIV na bado akawa haishi kulazza hosp. na kingine ni kula vizuri basi na wala ukiniona huwezi jua..na tangia nijijuwe na kuanza kutumia hii dawa ya mitishamba ni miaka 5.. poleni wagonjwa wenzangu kila jambo lina sababu, na c kila muadhirika kaupata ktk uzinifu

 3. Anonymous

  October 15, 2012 at 7:12 am

  Jamani hii habari inasikitisha, hata kama ni kutafuta ela hii hapana jamani, kwanini watu hawana huruma huu ni uuwaji, waliosababisha hii wanafaa kuadhibiwa kifo kabisa na inawezekana ndugu zetu wengine wamepoteza maisha kwa dawa hizi feki kutofanya kazi pengi wangekuwepo mpaka leo.

 4. Anonymous

  October 16, 2012 at 5:34 am

  Bora unayejilia mitishamba, manake huu ni uuaji wa moja kwa moja. Hao waliosimamishwa, adhabu yao isiishie hapo.

Leave a Reply