Uncategorized

PICHA ZA WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA

By  | 
 Watu waliingia na kukaaa kwenye siti zao

 Baada ya watu kukaa MC wa Shughuli Bi Gea Habib alinikaribisha kufungua rasmi shughuli yetu.
Nilifunguwa na kuwapa utaratibu wa shughuli nzima itakavyokwenda..
Wadhamini wakuuu wa women in balance kitchen party gala walikuwa Tsn supermarket.Marketing manager kutoka Tsn Lizbet alituambia kwa nini tununue mahitaji yetu Tsn supermarket.Pia walitoa ofa ya kufanya shopping na Tsn,kujishindia vocha za laki 1 na elfu 50 za kufanya manunuzi Tsn supermarket.
 Tulikuwa na msemaji kutoka Nairobi Kenya bi Getrude Mungai ambae ni Life Style Designer of Sex and Relationships.
 Aunty Sadaka mwanasaikolojia…
Tulikuwa pia na Chriss Mauki mhadhiri msaidizi wa saikolojia ya jamii kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.
Tulikuwa tukiburudishwa na skylite band,band mpya jijini na wako saaafi waliohudhuria waliona shughuli yao.
Women in balance kitchen party gala ilifanyika Diamond jubilee vip hall.Jumapili ya tarehe 21 ikiwa imedhaminiwa na Tsn supermarket,clouds fm,cocacola na sossi.
 Picha zaidi zinakuja….

11 Comments

 1. MOJAONE

  October 24, 2012 at 11:30 am

  HIVI NA WANAUME WANARUHUSIWA KUINGIA???

 2. Rukia Bakari

  October 24, 2012 at 12:05 pm

  Getrude 2namtaka tena kwenye nyingine itakayo fuata!aje a2pe habar za miss victoria!nimempenda sanaaa

 3. Anonymous

  October 25, 2012 at 11:16 am

  Veronica
  Aisee Dina nimeipendaje maana mmependeza mno kuanzia ukumbi hadi wahudhuriaji.

 4. Anonymous

  October 25, 2012 at 11:28 am

  Dina na Kamati nzima ya maandalizi Hongera sana kwa kazi nzuri. Kwa kweli ukiangalia mwitiko wa wanawake walio kwenye ndoa na wale ambao wanatarajia kuwa kwenye ndoa utagundua watu wana maumivu kwenye mahusiano waliyopo! Ni jambo zuri kuongea na kina Mama na Mabinti kuhusu namna ya kutunza ndoa zao! Ni jambo jema mno, kwani NDOA imeandikwa kwenye vitabu vitakatifu!!
  Dina, samahani nitoe maoni machache: (1) baada ya siku hiyo watu wapate kutia maoni je wamejengwa na je wataweza kuyachukua baadhi ya mawazo waliyotoa wasemaji! (2) Ni wapi hasa watapenda wataelezwe zaidi kwani ndoa ni pana mno!! (3) Mje mfikirie namna ya kuandaa Gala ya Wanandoa wote wawili wataoko weza kukubali kuja watajifunza sana, kwani kuna watu wanafikiri ndoa ni kitu cha "automatic" kumbe inatengenezwa!! tena tangu mwanzo wa uchumba! Ni hayo tu! Ila mwisho nilishindwa kufika kwani nilikuwa safari!! Ubarikiwe kwa ubunifu mzuri! Irene

 5. Anonymous

  October 27, 2012 at 12:29 pm

  Nice project mama

 6. Anonymous

  October 30, 2012 at 10:20 am

  DINA HONGERA SANA.KWA KWELI MEEANDAA KITU KIZURI.ANGALIZO LINGINE NAOMBA MUANDAE SEMINA ZA VIJANA NA WATU AMBAO WANAJIANDAA KUINGIA KWENYE NDOA.HII ITASAIDIA KUZUIA MPASUKO WA NDOA NYINGI.WENGI WANAFURAHIA KUINGIA KWENYE NDOA WAKATI HAJUI ATAENDA KUITUNZA VIPI HIYO NDOA ILI IDUMU.ITAKUWA VIZURI KUZUIA MADHARA KABLA YA WTU KUINGIA KWENYE NDOA

 7. Anonymous

  November 1, 2012 at 1:15 pm

  Mi kwa kuitizama tu kupitia kwa blogs pamaoja na yakwako kwa Hapa Arusha nadhani itawafundisha mambo zaidi wakina Dada na wakina mama na wakina Baba watashuhudia mabadiriko makubwa tuuu. Maaaana Kujisahau kumekuwa ni kukubwa sana katika Mahusiano Ndoa

  • Anonymous

   November 13, 2012 at 7:44 am

   Kiukweli mie mwenzenu nimeipenda kweli kitchen part gala.Na zaidi ya yote nimekutana phisically na aunty Sadaka, miaka michache iliyopita nilimpoteza mwenzi wangu mtarajiwa (yaani mchumba) sio siri nilikuwa nilielemewa na mzigo ambao sikujua namna ya kuutua.Maisha yangu yote kwa miezi kadhaa nilikuwa ni wakulia tuu.katika harakati za kusikiliza leo tena ndipo nilipomfahamu Aunty Sadaka na Dina huyu huyu akaniunganisha na aunty Sadaka kwa kunipa no ya simu amboyo nilimtafuta Aunty Sadaka na sio siri huyo mama alinisaidia sana kuikubali hali ile na kuendelea na maisha mapya.jamani Dina, Aunty Sadaka nawashukuru sana sana.sina cha kuwapa ila Mungu awape maisha marefu mzidi kuwasaidia watu wenye matatizo mbali mbali katika maisha yetu ya kila siku.Mungu awabariki.Ila pia nilipata nafasi ya kumshukuru Aunty Sadaka mimi mwenyewe kwa kuongea naye sio siri hata yeye alifurahi sana,na sasa Mungu amenibariki nimeolewa na Mungu ametujaalia mtoto wa kike kwa jina la Natalie.kwa ujumal wake naweza kusema Radio Clous is the peopl's station.Dina asante kwa kitchen part gala na Mungu azidi kukuongoza na akubariki katika maisha yako ya kila siku.Thanks Again.Much Love Nicole au Mama Natalie.

 8. Mama'ke Otto.

  November 12, 2012 at 6:19 pm

  jamani Dina hongera sana kwa kuandaa kitu chenye akili, mi nipo Arusha nilipania hiyo ya jumamosi lakini kama wasemavyo, mkamia maji, mwanangu alishikwa na homa ya ghafla saa saba, hapo ndio na pilika za kutafuta kivazi cha chenza,, poor me. Ila nimeambiwa mwezi wa tatu mnarudi tena,, haya uweke picha tuwaone mlivyopendeza..HONGERA KWA MARA NYINGINE….

 9. Anonymous

  November 21, 2012 at 9:45 am

  Dina Honger sana kwa hii issue nimeipenda but naomba mtufikirie na sisi wa huku visiwani Zanzibar tunastahili kupewa!Tunu

 10. Anonymous

  November 21, 2012 at 10:15 am

  karibuni na tanga pia dada dina

Leave a Reply