Uncategorized

SURA MBALI MBALI ZA WALIOBAHATIKA KUWEPO KATIKA KITCHEN PARTY GALA.

By  | 

Watu waling’aaa hatariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Arusha kaa tayari jumamosi ya tarehe 10 mwezi wa kumi na moja tunakuja…itakuwa  katika ukumbiwa Tripple A kuanzia saa saba mchana.

14 Comments

 1. MOJAONE

  October 24, 2012 at 11:23 am

  AKINA DADA 30000 ZIMEWATOKA ETIE KWA WAKE ZETU HUO NI MTAJI TOSHA.

 2. MOJAONE

  October 24, 2012 at 11:27 am

  SHAMIM NIMEKUONA UPO POWA.

 3. Anonymous

  October 24, 2012 at 11:33 am

  watu walipendeza sana,sasa wewe da dina mbona haupo pichani?watu tumejifunza dress code inapendeza sana.

 4. Anonymous

  October 24, 2012 at 11:34 am

  mbona wewe picha yako hujaweka, kama kwenye 8020

 5. Rosalia

  October 24, 2012 at 11:46 am

  Dina,

  sikuwepo ila inaonyesha ilikua tamu, halafu wadada/wanawake WALIPENDEZA SANA. na rangi ya event ilikua poa sana.

 6. Ruky

  October 24, 2012 at 1:11 pm

  jamani nimekufurahia watu walivyokupokea wito…mmependezza kweli…jamani Gea mpaka sura inabadilika kadayat kidog jamani..arusha jamani msije niaibishaaa maana huwa hatabirikagi kabisaaa..thatx dina kwa kutumwagia pic

 7. Anonymous

  October 25, 2012 at 8:52 am

  Wanawake wa Tanzania ni wazuri saana kwa muonekano wa nje ninachotamani ni hiki kitu kilichoanzishwa yaani Kitchen Party Gala iwabadilishe muonekano wao wa ndani hata kwa asilimia 60, japo wahenga walisema "samaki mkunje angali mbichi".Mabadiliko mazuri ya Mwanamke ndani na nje ni mafanikio kwa familia, watu wanao mzunguka na Taifa kwa ujumla maana wanawake ndio WALEZI wa jamii.Lakini wanawake wa chache wa zamani na wengi wa sasa Hawajashika nafasi zao vema, wanawake haswa wa sasa hawana mda na familia zao.

  Wimbi la mmomonyoko wa maadili wa watoto wa sasa yamesababishwa na wanawake ambao hawajashika nafasi zao vema, na sijui wanawake wajao ambao ni watoto wa sasa watakuwaje.

  Ninachoomba hii Kitchen Party gala isiwe TU kama moja ya viburudisho vya wanawake au mradi wa mtu kujiinua kiuchumi bali MABADILIKO YA WANAWAKE.

  WANAWAKE NI KIINI CHA MAADILI.

 8. Anonymous

  October 25, 2012 at 1:50 pm

  samahani Dina mimi nita differ kidogo na sifa hizo hapo juu kwa vile nilikua kwenye event.
  kwenye picha hapa kwa kweli inaonekana mambo yalikua poa.
  Nadhani hii ni mara ya 4 kama sikosei unafanya hii gala ya kitchen party. mapungufu yaliyokuwepo siku ile, sikutegemea yawepo taking into consideration kua uko experienced.
  Naomba niorodheshe mambo machache ambayo niliona yana kasoro ili next time uyarekebishe ukiona kuna umuhimu:
  1. kuna upendeleo wa aina fulani. hata kama mimi na rafiki zangu hatukuweza kulipia meza ya watu 10 kwa vile hatukutimia, sikuona ni kwanini uweke watu mwisho wa ukumbi na mashosti wako wote wawe mbele. kutuchanganya ndani ya ukumbi would make a lot of balance hasa kutegemea mtu kaja saa ngapi.
  2. Ukumbi ulifurika sana mpaka ikawa kero. Mtu ambaye yuko organised unatengeneza tickets kama ni 1000 ina maana utaweka viti 1000. wa 1001 ina maana hatapokelewa no matter ametokea karne ipi. maana kuna time ulijetetea kua kuna watu wametoka morogoro na arusha so you couldnt reject them. Sidhani kama ni sawa.
  3. kwa vile ulijaza sana watu, hata chakula kwa wale waliopakua mwishoni walikosa I must say, waliambulia punje za wali zisizo wa mchuzi. cha ajabu wapakuaji waliminya sana chakula hasa kuku, baadaye zikabaki, wakaanza kupitisha ukumbini ili mtu aokote, lakini wa vile hakukua na mfuatiliaji at least kuwaonyesha wapi wagawe, walizigawa kule mbele kwa mashosti ambao walipakua chakula mwanzo na waliopata chakula cha kutosha, kwa hiyo wa nyuma wakasahaulika tena.
  4. Watu walikaa masaa wamekauka makoo bila kupewa vinywaji maana waandaaji mko busy na kupiga mapicha. maji ya kunywa na juice vilitolewa mwishoni wakati wantu wanataka kuondoka. sina hakika kama yalichelewa kuja au ndio ulikua mpango wenyewe.
  5. nahitimisha hivi, in future, ongeza kiingilio, hata ifike 50,000 ili uweze kumeet your targets ili usilundike watu. uwe na watu wachache ambao utaweza kuwa manage.
  kwa vile wote tunalipia kiingilio sawa, sioni kwa nini kuwe na reserved tables. I think anayekuja mapema akae anapotaka aliyechelewa bahati yake mbaya. mtu mwingine kawahi, lakini kajikuta yuko nyuma kabisa maana all front tables ni za mashosti. sio sawa.
  samahani kama nimekukwaza. unayoona yanafaa ya pick, what you think is bull shit, tia kapuni. Nakutakia Eid el Haj njema.

  • Anonymous

   November 5, 2012 at 9:09 am

   Wala hujakosea sista, hii ndio hali halisi iliyokuwepo………mimi ilikuwa mara ya kwanza kuhudhuria lakini nikajiuliza, mbona kama hii siyo ya kwanza, na mapungufu yanaonekana kama ni event ya kwanza?

   Nafikiri Dina mna nafasi ya kurekebisha haya mambo, otherwise tutaona lengo ni pesa na si vinginevyo…..

 9. Anonymous

  October 25, 2012 at 1:57 pm

  we MOJAONE unamaneno wewe!!!
  Loooh nn elfu 30.mbona nyinyi wanaume mnamatumizi zaidi ya hayo na hakuna wakuwalaumu!!!!! elfu 30 na umejifunza mengi zaidi hata ya hiyo elfu 30 yako uliyotoa.
  Florah (Mama Mario)

 10. Anonymous

  October 25, 2012 at 2:01 pm

  jamani dina me nakupenda umzuri sana,, pamoja na gea nawapenda sana

 11. Anonymous

  October 26, 2012 at 6:02 am

  nataani ningekuepo dina,,,, ila niefurahi kuskia mnakuja arusha jaani karibuni sana tunawasubiri kwa hamu,hope arusha pia twaweza nunua meza tukakaa mashost?getrude waa kenya nae atakuepo?ant sadaka asikose please,,,,,,,uwiiiii,,,,ungu anipe uzima,,,

 12. Anonymous

  October 27, 2012 at 5:51 pm

  SIJUI KAMA NA WADAU WENGINE MMELIONA HILI.. WADADA WAMEPENDEZA NA MAKE UP ZAO ZIMETULIA MNOOO, UNAMTAZAMA MTU UNAPENDA MAKE UP YAKE, SASA KUNA BLOG MOJA INAWEKAGA MAMBO YA HARUSI HARUSI… KHAAAAA! YAANI MARANGI PINK BLUE PULPLE RED.. YAANI NI KICHEKO UKIMTAZAMA MWANAMAMA HAPO.. HILI NALO MUWE MNALIONGELEA KAMA KWELI TUNAPENDANA, TUAMBIANE JAMANI MAKE HIZI TARATIBU, USIJE UKAJUA UMEUPARA KUMBE UMEUPURA.. HAAAAA! WALAHI KICHEKO!!!

 13. Anonymous

  October 30, 2012 at 11:50 am

  je kwa arusha itakuwa shillingapi kingilio?

Leave a Reply