Uncategorized

UMEWAHI KUWEKA MAISHA YAKO HATARINI ILI KUOKOA MAISHA YA MWINGINE???

By  | 
Kijana mdogo pichani  Nelson Fonangwan mwenye miaka 16 amefanya hivyo.Alikuwa amelala nyumbani kwao na kuamshwa na kelele za majirani ambao walikuwa wakiunguliwa na nyumba.
Aliamka na kwenda kuangalia nini kinaendelea akakuta nyumba ya jirani ikiungua na mama mwenye watoto wawili akihangaika kuvunja dirisha kwenda kumuokoa mtoto wake mdogo Adam mwenye miaka 2.
Mama alivunja dirisha bila mafanikio huku moto ukizidi kuwaka ndipo Nelson alipokuja akavunja dirisha na kuingia ndani kumuokoa mtoto.Mama akapiga simu 999 ikaja gari ya zimamoto.
Akisimulia moto ulivyotokea mama wa mtoto anasema alikuwa ameenda nje kutupa uchafu akiwa amemuacha mwanae mdogo jikoni.Kurudi mlango ukawa umejifunga na kumbe aliacha fying pan jikoni ikaanza kuungua na baadae moto kuanza kuwa mkubwa.Alijitahidi kuvunja dirisha na mkono ambao aliumia sana huku akipiga kelele ndio kijana Nelson kutokea na kumsaidia.
Tukio hili lilitokea nchini Uingereza maeneo ya Southampton.Kijana Nelson Fonangwan asili yake ni Cameroon lakini yupo huko kimasomo akisomea health and social care,maths na english.

11 Comments

 1. Anonymous

  October 1, 2012 at 4:12 pm

  Soo touching. Ndio wajue wa afrika tulivyo na upendo regardless of race.

 2. MOJAONE

  October 2, 2012 at 5:47 am

  NI USHAJAA WA HALI YA JUU UNATAKA MOYO.

 3. Anonymous

  October 4, 2012 at 1:21 pm

  waafrika tuna roho sana,Mungu ambariki uyu kijana

 4. Anonymous

  October 4, 2012 at 5:50 pm

  Big up

 5. Mohamedsalum

  October 6, 2012 at 11:18 am

  ujasiri wa hali ya juu!

 6. Anonymous

  October 10, 2012 at 6:49 am

  waafrika tunaupendo kutoka moyon,sio kama wenzetu wazungu. Ujasiri wa hali ya juu sana ameonyesha

 7. Anonymous

  October 12, 2012 at 12:59 pm

  Mungu azidi kumbariki huyu kijani na asome kwa bidii

 8. Anonymous

  October 23, 2012 at 9:39 am

  so much touching.

 9. Anonymous

  October 24, 2012 at 9:46 am

  Safi saaana kijana huo ndio utu!! lkn course unayosoma huo mchanganyiko wake hata sijauelewa!! HEALTH & SOCIAL CARE MATHS & ENGLISH??? kweli ulaya balaa!!!

 10. Anonymous

  October 25, 2012 at 8:41 pm

  big up kaka nimeipenda

 11. Anonymous

  October 29, 2012 at 12:39 pm

  Waafrika bwana, hivi kwa nini hamjiamini. Eti oooh sisi waafrika tuna upendo, yaani kuona tu ni mweusi kaokoa mweupe imekuwa nongwa, Hivi mnadhani hakuna watu weupe wanaookoa watu weusi. Binadamu wote tuna roho sawa tu, chuki, upendo, ubaguzi hautegemei sana rangi ni malezi na mazingira na ndio maana kuna waafrika ni wabaguzi balaa.

Leave a Reply