Uncategorized

UTAMADUNI WA VITU ASILI VYAIPANDISHA RWANDA KIUCHUMI

By  | 
Kwa hali ya
kawaida utaona ni ngumu kuamini kwamba kitu kama utamaduni kinaweza kuwa chanzo
kikubwa cha uchumi kukua katika nchi husika.

Nchi ya
Rwanda imekuwa moja kati ya nchi baarani Afrika ambayo imefanikiwa kukuza na
kuendeleza utamaduni na sanaaa mbao tayari imekuwa ikichangia kalibia asilimia
60 ya mapato ya nchini na kuwapatia ajira vijana kwa urahisi.
Mapato haya
yamekuwa yakitokana  na fedha za kigeni
ambazo wamekuwa wakitoa watalii kutoka nje ambao hasa wamekuwa wakihamasika
kununua vitu vizuri vya asili ambavyo vinatengenezwa kiasilia na wasanii wa
sanaa za utamaduni nchini humo.

 Mbali na  kuteka soko la watalii wamekuwa na vivutio  vya asili ikiwemo vyakula na ngoma.Taasisi zinazohusika na mambo ya utalii wamekuwa mstali wa mbele kutangaza vivutio hivyo ndani na nje ya nchi ukilinganisha na sisi wabongo ambao tunavivutio lukuki na tumeshindwa kunufaika navyo.
Sijui idara zetu hapa Tanzania zenye dhamana ya mambo haya ya utamaduni  zinafanya nini.Inafahamika sisi ni the best more than Rwanda kwa vivutio,sijui tunakwama sehemu gani ama tatizo liko wapi!

12 Comments

 1. MOJAONE

  October 2, 2012 at 9:32 am

  DU!!! KUMBE DINA ULIKUA HUJUI ..
  CC NI WAVIVU WA KAZI NA TUNAPENDA SANA SHORTCUT.
  NA NDIO MAANA TZ INAONGOZA KWA KUWA NA MAFREEMASON WENGI AFRICA KWA SABABU WANATOA PESA KIRAHISI.

 2. Anonymous

  October 2, 2012 at 11:23 am

  mada ya leo na chris ilikua poa tho mmetoka online ila big up

 3. Doreen

  October 2, 2012 at 12:30 pm

  Yaani ukitaka kuumiza moyo wangu onyesha maendeleo ya nchi ya Rwanda, naumia sana. Yaani hawa wa juzi tu wanatupita kwa kasi ya maendeleo. Kibaya zaidi wana ratiba ya usafi katika siku moja ya wiki, watu wote wanatoka kufanya usafi, nikiliangalia jiji la DSM nasikia kichefuchefu kwa uchafu. Hongera Rais wa Rwanda na Wananchi wake.

 4. MOJAONE

  October 2, 2012 at 1:39 pm

  KTK REPORT ILIYOTOLEWA NA SHIRIKA LA ASSN INASEMA KUWA MTZ ANAONGOZA KWA KUPENDA STAREHE. NA HIYO NI KWELI KABISA YAANI TOKA SAA 4 YUPO BAA, USIKU ANAKESHA KWENYE KUMBI ZA STAREHE MPAKA ASUBUHI AKIENDE KAZINI PICHA HAIENDI MPAKA UTOE RUSHWA, NGONO NDIO USISEMA, SALOON ZIMEJAA W/WAKE WANAOJIPAMBA NK..
  TUTAPATA WAPI MUDA WA KUFIKIRI MAMBO YA UBUNIFU.

 5. Anonymous

  October 2, 2012 at 4:51 pm

  Dina hii mada jibu lake sahihi lipo kwenye INTELLECTUAL PROPERTY RIGHTS LAW (IPRs), Tanzania inaweza faidika through protection of traditional knowledge and folklores. Rwanda wanatumia IPRs ndo sababu wanavuna matunda yake. sijui lawyers,policy makers na intellectual property rights experts wako wapi na ina maana hawajaona hii money making opportunity inapotea bure? Samahani kwa kuchanganya lugha.

  • Anonymous

   October 4, 2012 at 9:14 am

   nimependa mchango wako ni kweli tupu.., yaani wataalamu wa watz hawajui kunusa where money is!Rwanda is going places for sure….ni muda muafaka kwa tz kuamka na kuchangamkia opportunities zinazojitokeza au zilizopo.

 6. Anonymous

  October 3, 2012 at 5:47 am

  OUT OF TOPIC

  Samahani Dina, jana niliangalia kipindi cha take one cha Zamaradi, alikuwa amependeza sana kichwani. Mwisho wa kipind akasema ametengenezwa kwa Mariam, kama umependa uwasiliane kwa namba ya simu iliyokuwa inapita kwenye screen. Sikuwa na simu karibu ili kunakili namnba.
  Sasa, naomba umwambie Zama kuwa naomba hiyo namba ya kuwasiliana naye ili nimtafute huyo Mariam. Namba yangu ni 0754 593839

 7. Anonymous

  October 3, 2012 at 5:53 am

  wenzetu wanafanya ya kwao na kujivunia ya kwao sie tuko bize kukopi na ku paste fleva kisha tunaita muziki wa kwetu na ndiyo maana haupendwi nje ya nchi yetu. Tujaribu kujivunia ya kwetu jamani.

 8. Anonymous

  October 3, 2012 at 8:50 am

  Sisi siyo wavivu ila tunakatishwa tamaa na comment za watu wenye negative attitude, wbinafsi na waroho. Suala la viongozi wa kigeni kuja Arusha halafu kutafutwe kampuni ya kigeni kuandaa burudani na kuimport wasanii kama sisi hatuna utamaduni imenikata stimu sana na nilipata hasira sana kusikia ile habari aliyotoa Gerald Hando kwenye PB. I was about to cry yaani. Wasanii tunao wazuri sana na kwenye kiwanda cha burudani Primetime promotions wanaaminika Africa mashariki na kati na tunaelekea kukimbiza Afrika nzima…..I hate these people waroho wasiotaka maendeleo ya watanzania wenzetu.

 9. emu-three

  October 3, 2012 at 11:16 am

  Taifa lisilo kuwa na utamduni ni koloni la wengine. Na utamduni ukiwekezwa vyema ni rasilimali!

 10. Anonymous

  October 5, 2012 at 9:33 am

  leo kiswahili hapo kimekuacha ua so gud hope umepitiwa u mix up r and l usinunie nmekwambia wewe 2

 11. Anonymous

  October 17, 2012 at 8:39 am

  huyo waziri ya hiyo sekta ya utamaduni yuko wapi? na je nasoma kweli maoni ya watanzania wenye nia ya kujenga nchi yao na wenye uchungu na nchi yao. ila wadau machosema ni kweli kabisa ukizingatia Rwanda ni nchi ndogo sana ukilinganisha na nchi yetu na sisi tuna vivutio vingi lakini tumeshindwa kuvitumia hiyo yote inatokana na uongozi kutosimama imara.

Leave a Reply