Uncategorized

HUYU NDIO MISS TANZANIA 2012-2013

By  | 
 Brigette Alfred kutokea
Kanda ya Kinondoni (Sinza).Akiwa amewabwaga wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo.Na kujipatia zawadi yake ya Gari aina ya Noah na pesa taslim Tsh ml 8.Hongera sanaaaaa!!
Juzi watu wengi waliokuwa wakifatilia miss Tanzania walikuwa wakilaumu sana kuwa zawadi ni ndogo,na kuwa gari aina ya Noah sio zawadi ya maana kwa mrembo wetu wa mwaka huu.Ila nakumbuka zawadi iliyotangazwa awali ilikuwa ml 8 hii ya Noah ilikuja julikana siku ya shindano.Ulikiwa ukiingia kwenye mitandao ya kijamii kama facebook,twitter ndio kulichafuka.
Mie nilikuwa na swali kidogo kwa ndugu zangu watanzania.Hatujui kwa mwaka huu kamati ya miss Tanzania walikuwa na bajeti kiasi gani.Ila swali langu ni kwamba tuache kwamba kila mwaka mshindi amekuwa akizawadiwa gari.Wewe unadhani mshindi awe anapewa zawadi gani kulingana na maisha yalivyo hapa kwetu Tanzania.Pia washiriki wengi wanakuwa ndio wapo vyuoni au wamemaliza kidato cha nne au sita.Bado ni mabinti wadogo wenye ndoto na malengo mengi ya baadae.
Zawadi gani itamfaa?pengine gari tumekariri labda kuna namna tunaweza kumuwekea msingi mzuri wa kimaisha huyu binti.Tufikirie binti kama huyu baada ya hapo gari inahitajika kwenda service mara kwa mara,petrol iwepo ili gari  ikae barabarani na hana kazi inayomuingizia kipato.!!

11 Comments

 1. RUKY

  November 5, 2012 at 12:39 pm

  BORA WAWE WANAPEWA MIKATABA YA KUSOMESHWA MPAKA ATAKAPO SEMA BASI..LABDA NA NYUMBA YA KUISHI… JAMANI SHULE MUHIMU KWAKWELI HAKUNA ATAKEYEWEZA KUKUNYAGANYA WALA KUKUNYANYASA NAYO NA WLA C GARI USEME LITAKUTIA HASARA YA MAFUTA KILA SIKU…MSHINDI MREMBO MASHALAAH

 2. Anonymous

  November 6, 2012 at 10:08 am

  KWANZA MI NAWAPONGEZA KWA KAZI NZURI YA KUTUPATIA MREMBO HASAA,PILI NI KWAMBA WATANZANIA WANATAKIWA WAELEWE KWAMBA MAPUNGUFU NA CHANGAMOTO ZIPO KWENYE KILA JAMBO KINACHOTAKIWA NI KUWASHAURI KAMATI YA MISS TANZANIA ZAWADI ITAKAYOFAA KWA MREMBO WETU,LAKINI PIA ZAWADI YA GARI SI NZURI KABISA KWA MREMBO KWANI NDIO CHANZO CHA KUMWINGIZA KWENYE TAMAA MAANA WAREMBO WENGI BADO NI WADOGO SANA NA HAWAJAANZA KUJITEGEMEA SASA ANAPOPEWA GARI MAFUTA,SERVICE NDIO ANAPATA WAPI????NDIO MAANA BAADA YA HAPO ANAANZA KUZITAFUTA SASA PESA ZA MAFUTA NA SERVICE MAANA SI WOTE WANAOSHINDA WANAKUWA NA UWEZO WA KULIMUDU HILO GARI.

 3. evalyne Tagatta

  November 6, 2012 at 11:08 am

  Wawe wanapewa nyumba ya kuishi na kazi kama inawezekana kama anasoma awe anasoma na akaunti yake wamuwekee pesa sio gari

 4. Anonymous

  November 6, 2012 at 12:12 pm

  Dina unasema hana kipato asijali mapenejee tupo tutamjazia tu mafuta na gari litaingia barabari bila ya wasiwasi sasa ninachotafuta ni nambari yake ya simu please dina wewe ni rahisi kupata namba yake fanya utaratibu basi niipate comission utapa dina please…please…please.

 5. Anonymous

  November 6, 2012 at 12:19 pm

  Vipi mbona miss tanzania wa mara hii hakuvaa croun vipi au wameshaichakachua akina lundenga.mtoto mzuri sana huyu tena ni bikira kabisa daaaah wakubwa wanafaidi hakiya Mungu.

 6. Anonymous

  November 6, 2012 at 12:20 pm

  Haya nenda kwenye mashindano ukavae kichupi binti eeeeh

 7. Anonymous

  November 6, 2012 at 4:54 pm

  Ila ni mzuri jamn, i hop atatuwakilisha vilivyo huko mbeleni. Mungu akutangulie, na kp on kujitunza.

  Colleta

 8. Anonymous

  November 7, 2012 at 6:50 am

  she deserve to be a miss Tanzania, ila nashauri apewe nyumba na asomeshwe then apate kazi nzuri, mbona nacy sumary alipewa nyumba na gari na kazi nzuri so na hawa wangeendelea kufanya hivyo ona wema mpaka leo hata kibarua hana lkn angesomeshwa zaidi kwa kiwango alichoshia akaendelezwa angekuwa na kazi yake nzuri wala asingetanga tanga kwa ajili ya maisha

 9. Anonymous

  November 8, 2012 at 3:37 pm

  Nyumba. Kuna apartments nyingi tu zinauzwa. Hata kama hataitumia leo anaweza ikodisha na ikawa source ya income. Hakika ni karembo!

 10. Anonymous

  November 9, 2012 at 3:41 pm

  shigongo keshapata kazi hapa,kudadeki zake!

 11. Anonymous

  November 20, 2012 at 9:31 am

  subirin vibwanga vyaka nae ''coming soon'' iyo ilo gar litaingia barabarani na petrol itajazwa tuu na service pia itapatikana wachumba si wapooo…

Leave a Reply