Uncategorized

POLE ZAMARADI KWA KUMPOTEZA MAMA

By  | 
Juzi jumatano mida ya saa tatu  nikiwa nakuja kazini asubuhi Zamaradi alinipigia simu kuniomba ruhusa kuwa hataweza kuja kwenye move leo ya leo tena kwani usiku wake mama yake alizidiwa sana.Baada ya kuzidiwa wakamuwahisha hospitali ya Hindu Mandal ambapo asubuhi hiyo alikuwa akipumua kwa mashine.
Baada ya kufungua kipindi mida ya saa tatu na nusu nikakuta missed call ya Zama kwenye simu yangu.Nikasema ngoja nipige japo niko studio kujua kulikoni ndio Zama kupokea huku akilia sana ”Dina mama yangu amefariki”
Niliishiwa nguvu hata leo tena ikanipa shida kuendelea kuifanya.
Kwa muda kama mfatiliaji wa leo tena utakuwa umegundua kuna siku Zama yupo kuna siku hayupo.Muda wote huo amekuwa akimuuguza mama yake hata kabla baba yake hajafariki.Mama yake amekuwa akisumbuliwa na kansa ya kizazi kwa muda sana.Na muda wote amekuwa akipambana mpaka hiyo juzi alipoaga dunia.
Napenda kumpa pole Zama na pia kumwambia kuwa mama yake amemuacha akiamini atapambana maana Zama yeye ni wa kwanza kwa mama akifuatiwa na mdogo wake Ummy.Mama alipenda kuwa nanyi lakini safari yake ilifika mwisho.Lakini aliondoka akiamini Zama umpambanaji usisononeke sana bali simama my dear.
Nimekuwa namuona Zama anakuja kufanya segment lakini hayupo sawa ataniambia ”Dina sijalala jana mama alizidiwa tumemkimbiza ocean road,hali ya mama ni mbaya”halafu ataangua kilio na kujikaza na kufanya movie leo akimaliza atawahi hospitali.
Jana saa kumi mama yake Zamaradi alizikwa katika makaburi ya kisutu.
Zamaradi nakuombea wewe na familia kwa ujumla muweze kuzoea hali hii mpya katika maisha yenu.Msisononeke sana bali kuacha mapenzi ya Mungu yatimizwe.

23 Comments

 1. sammy

  November 30, 2012 at 12:00 pm

  yan huwez amin nilivolia hapa na imenikumbusha siku nlipompoteza mama na nilidhan cwez kuendelea na maisha hya ila huwez amin dina nipo na naendelea kuwepo japo penga halizibiki na napenda kumwambia zama ni ngum kuzoea ila kwa uwezo wa mungu kila kitu kitaenda poa,nawapenda sana wote na mungu awalaze pema mama zetu

 2. Anonymous

  November 30, 2012 at 12:48 pm

  mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.

 3. Anonymous

  November 30, 2012 at 12:49 pm

  NI KITU KIGUMU SANA KUKIKUBALI HASA KUONDOKEWA NA MTU MUHIMU KAMA MAMA,ZAMARADI SASA NDIO UMEKUWA RASMI,MAJUKUMU YA WAZAZI NDIYO UMEYABEBA MPENZI,MUOMBE MUNGU AKUONGEZEE NGUVU,UJASIRI,HEKIMA ILI UYAENDELEZE YALE YOTE MEMA ALIYOYAACHA MAMA,TUKO PAMOJA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.MAMA ISAAC WA KISEKE MWANZA.

 4. Anonymous

  November 30, 2012 at 12:56 pm

  pole zama Munngu akutie nguvu.

 5. RUKY

  November 30, 2012 at 1:23 pm

  INALILAHI WAHINA ILAHI RAJIIUNI..TUPO PAMOJA ZAMA TUMUOMBEE APATE AMALI NJEMA…

 6. Anonymous

  November 30, 2012 at 3:04 pm

  Aisee hata mimi nampa pole sana,kwasababu ana hali ngumu sana kulingana na jinsi yeye ndo anabaki kua tegemeo la familia kwasasa!!Dina kaa naye karibu sana kwasababu kupoteza baba na mama ukiwa bado upo kama zamaradi mtoto asiye na ndugu aliye juu yake! inakua ngumu sana kuzoea.Kikubwa ni kumsogelea Mungu ingawa maisha ya wa bongo hapo kwenu ni maisha ya kiibilisi,ukiangalia vizuli utagundua kwamba yanayotendeka hapo Dar hata huku ulaya miji mikubwa hayapo au hayatendeki?starehe zimezidi nakusababisha watu wanamsahau muumba moja kwa moja.Ni hayo tu kwa leo.
  Mdau from The Haque

 7. Anonymous

  November 30, 2012 at 3:06 pm

  poe sana mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
  kazi ya mungu haina makosa

 8. neema alex

  December 1, 2012 at 10:36 am

  pole sana zamaradi…mungu akupe nguvu zaidi

 9. Anonymous

  December 1, 2012 at 9:04 pm

  Pole Sana Zama, Ni Kazi Ya Mungu Haina makosa La Maana Ni Kumuomba Mungu Awape Nguvu Ya Kuikabili Hali Ambayo Mnaifeel Now, I Know How You Feel, Nami Nilishamzika Mama Kiukweli Naelewa..Pole Sana Zama.
  Its Me Crytek

 10. Anonymous

  December 2, 2012 at 7:50 pm

  POLE SANA ZAMARADI KAZI YA MWENYEZI MUNGU MUUMBA WA KILA KITU (SWT) HAINA MAKOSA.

 11. Anonymous

  December 2, 2012 at 7:57 pm

  Pole sana Zamaradi. "Kila nafsi itaonja mauti". Quran takatifu.

 12. Anonymous

  December 3, 2012 at 6:31 am

  Pole sana Zamaradi. Mungu ni mwema kwa kila jambo, mlimpenda sana lakini Mungu kampenda zaidi. R.I.P Mama Zamaradi

 13. aalusinde

  December 3, 2012 at 11:21 am

  Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi,ni safari yetu sote Mungu awape wepesi wa mioyo yenu amina.pole sana Zamaradi na dina

 14. Anonymous

  December 3, 2012 at 9:05 pm

  Inna lillah wain ilaih rajiuun, pole zama M/Mungu atakupa subira kwa hili na mengineyo Dina naomba no ya simu ya Zamaradi ikiwezekana mimi niko nje ya nchi ntashkuru sana naitwa Dada Fatma

 15. Anonymous

  December 4, 2012 at 7:29 am

  pole Zama Mungu awatie nguvu. Wewe hapo juu unayesema maisha yetu huku bongo ni ya anasa kuliko huko kwenu ulaya wewe sio mbongo? Umejuaje kama ni ya anasa kama ww huzifanyi? Halafu unatakiwakutoa boriti kwenye jicho lako ndio uone boriti kwenye jicho la mwenzio. Ulitakiwakumpa Zama pole sio kutuhukumu…shame on u…

 16. Anonymous

  December 4, 2012 at 8:53 am

  mpe pole sana Zamaradi.

 17. Anonymous

  December 4, 2012 at 12:04 pm

  innalilahi waiinailahi rajuun pole Zamaradi

 18. Anonymous

  December 5, 2012 at 7:15 am

  pole sana Zama,mungu atawapa wepesi,Inshaallah

 19. Anonymous

  December 6, 2012 at 4:14 am

  pole mwaya ..Mungu akutie nguvu kipind hiki kigumu cha kumpotaza mama..MUNGU kampenda zaid..dah inauma sana..pole sana

 20. Anonymous

  December 6, 2012 at 10:35 am

  pole zama, pole mamii naelewa unavyojisikia coz nilipoteza wazazi wote wawili. ila kifo cha mama kiliniumiza sana she was a realy friend of mine.si unajua mtoto wa kike na mama? alikuwa mwenyewe nikirudi toka job namkuta barabarani karibu na home ananisubiri anipokee then tunarudi home wote, alinilelea mtoto wangu hadi anafika two yrs yeye ndo akafa. alikuwa akienda ktk semina akipewa chakula anaficha kipande cha kuku au chochote atakachoona kitanifaa ananiletea. wakati naenda kulala alikuwa akinichezea nywele zangu hadi napitiwa na usingizi, ni mengi hayaelezeki kwa kweli. ila siku moja nimerudi nimemkuta ananisubiri barabarani akanipokea akasema anataka aniambie kitu muhimu sana, nikamwambia ngoja niende chooni kwanza, nilipotoka chooni nikamwambia niambie mom' akataka kuongea sauti haikutoka, NIKASTUKA. akanionyesha ishara nimpe peni na karatasi aniandikie nikaleta fasta, hakuweza kuandika zaidi ya kuchora mstari tu. Hakuongea tena mom wangu, akaumwa kama mwezi akaaga dunia. Zama mama mtamu, na kama unapata nafasi ya kulia LIA TENA LIA sana hadi ujisikie nafuu hii itakusaidia, ilinisaidia.natofautiana sana na wale wanaosema usilie vibaya kupiga makelele na kuongea maneno maneno wakati unalia.kwa sasa ni miaka kumi imepita na still naumia.Pole zama uwe unaomba mungu na kumuombea yeye kila siku kabla ya kulala na asubuhi na hata wakati wowote utakaokumbuka. ukipata hela ya HALALI nunua mikeka, majuzuu au katengeneze chochote msikitini au kisima kitakachowasaidia watu huku umeweka nia kuwa unafanya hayo kwaajili ya mama na kumuomba mungu apokee na thawabu ziende kwa mom yetu kipenzi na inshaallah ataondolewa madhambi na kufanyiwa wepesi huko aliko. huna cha kumfanyia tena mom ila hizo dua na hayo niliyokueleza yatakusaidia.Pole tena my dear.

  DA J
  ooh im crying

  • bibi chief

   January 1, 2013 at 11:04 pm

   pole sana umeniliza

 21. Anonymous

  December 6, 2012 at 5:13 pm

  POLE Zamaradi as much as ninavyokupenda nimeumia kusikia umefiwa na mama Mungu akujalie faraja wewe na familia yako yote….lav u

 22. Anonymous

  December 6, 2012 at 8:37 pm

  POLE DEAR SI WEWE TU ZAMA ,HATA MIE MAMA YANGU ALIFARIKI NA KANSA YA KIZAZI .IKANIBIDI NIHAMIE SWEDEN KITU AMBACHO SIKU PANDA KTK MAISHA YANGU YA NYUMA. HUKU NIMEJIKUTA NI MPWEKE ILA SIACHI KUSWALI NA KUWAOMBEA WAZAZI WANGU WAWILI WALOTANGULIA MBELE YA HAKI .KUWA NA FURAHA UNA AFYA NA UNAKAZI .iNALILAHI WAINAILAIH RAAJUUN . ATABAKI ALWAH TU

Leave a Reply