Uncategorized

HILI SUFURIA UKILITAZAMA SUPU ILIYOPIKWA HUMO HUWEZI KUITAMANI,LAKINI….

By  | 
  Hapa imepikwa supu ya hatarii yenye mchanganyiko wa makongoro,utumbo,mkia,ulimi n.k
  Nikiwa Arusha bar ambayo nimeisahau jina mida ya saa kumi na mbili
jioni kibaridi kikiwa kinapuliza hivi ndio nikauona mzigo huu.Niliona
sufuria limebebwa na kuwekwa juu ya meza ghafla watu kibao wakalizunguka sufuria kujipatia supu.
 Hapo unasimama unachagua kipande unachokitaka unakatiwa katiwa na kuwekewa supu kwenye kibakuli huku ikiwa ni ya motoooo.
Baada ya nusu saaa tu sufuria lilikuwa jeupeeee mzigo umekata.Nilipewa jina la supu hii lakini nimelisahau kwa sasa maana muda kidogo umepita.

6 Comments

 1. RUKY

  December 11, 2012 at 6:07 pm

  DINA ARUSHA KWA MAMBO YA MAANKULI HAPANA CHEZEA KABISA MI MWENYEWE NIMEPAMISS ILE MBAYA…

  • Anonymous

   December 13, 2012 at 11:48 am

   kweli arusha ndo kwenyewe kwa mambo kama hayo. Kuna TRUPA, MTURA, MAKANGE, CHAKULA CHA WAATHIRIKA NK.

 2. Anonymous

  December 13, 2012 at 4:40 pm

  Yaelekea tam san maana udenda wanitoka

 3. Anonymous

  December 14, 2012 at 6:18 pm

  Huku Arusha masuala ya supu supu, mitori na vingine vizuri ndio mwake,,, huwa sufulia nje hatuliangalii bali ndani kwenye uhondo..karibu tena na tena

 4. Anonymous

  December 17, 2012 at 6:17 am

  dada dina!hiyo bar inaitwa freedom ipo sakina hapo supu asubuhi saa tatu na jioni saa 11.

  Ila sehemu za mambo kama hayo zipo nyingi mno arachuga kila moja na umaarufu wake. karibu

 5. Anonymous

  December 28, 2012 at 8:39 am

  HAPO BILA UBISHI NI KENI GARDEN, ARUSHA

Leave a Reply