Uncategorized

KWAHERI 2012 KARIBU 2013…NA HAYA NI MACHACHE NILIYONAYO YA KUSEMA.

By  | 
Mwaka 2012 ndio unaishia  hivyo na tukijaaliwa
tutaukaribisha mwaka 2013.Kwa muda blog hii imekuwa ikisua sua sana hii yote ni
kwa sababu ya majukumu tu wapenzi wangu ila tatizo hili nalitafutia dawa maana
limekuwa sugu.

LEO TENA NA DINA MARIOS

Wakati 
tunaukaribishwa mwaka 2013 napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa
wasikilizaji wangu wa leo tena,mashabiki wangu mimi kama Dina Marios.Hii yote
ni kwa sababu mwaka 2012 leo tena imeweza kuwa kipindi pendwa na chenye
wasikilizaji wengi wa rika zote japo mlengwa ni mwanamke.

Na mimi kama Dina Marios kuwa mtangazaji namba moja wa kike
anayependwa na mwenye mashabiki wengi Tanzania.Pia kuwa namba mbili kwa
Tanzania kwa jinsia zote nina amini clouds ingekuwa inashika mikoa yote basi ningekuwa namba
moja.Lakini  yote ya yote si mimi bali ni
wewe ambae umekuwa na sisi bega kwa bega kupitia leo tena ya clouds fm.Kupitia
leo tena tumebadilisha maisha ya watu wengi sana kwa kuleta faraja na
furaha.Mfano mzuri ni wakati muigizaji Sajuki akiumwa,taarifa zake zilikuwa
kila mahali lakini hakukuwa na chochote kilichofanyika.
Nilipoamua kumuhoji
Wastara kwa kina juu ya ugonjwa wa mumewe na kuhamasisha watanzania kumchangia
ndipo hapo kila kitu kilibadilika mwisho wa siku India alikwenda na kutibiwa
japo hivi ninavyoandika hapa yupo kwenye hali mbaya sana amelazwa Muhimbili.

Mimi kama Brand manager wa leo tena nikiwa na team yangu ya ukweli Gea
Habib,Zamaradi Mketema,Da Huu kabla hajarudi coconut fm Zanzibar,Aunty Sadaka,Bi
Ponza aliyekuwa producer Moshy Habib na sasa Adrian Kaneno.Wote kwa ujumla
tumefanya kazi kubwa sana ya kukuburudisha na kukuelimisha vya kutosha kwa mwaka 2012 tunasema asante sana kwa kuwa nasi.

  

Mwaka 2012 yamo mambo kadhaa ambayo najivunia kuyafanikisha.
MWANAMAKUKA

Mwaka 2012 nilishiriki katika mambo mengi sana kama
unakumbuka shindano la  MWANAMAKUKA.Nililifanya
chini ya UWF (unity of women friends) kwa ushirikiano na leo tena.Lilikuwa
likihusisha wanawake wajasiriamali wadogo wadogo waliokwama lakini hadithi zao
wa wao kujaribu mara kwa mara licha ya kukwama ndio iliwawezesha kupata
ushindi.
Na zawadi ilikuwa ni pesa taslimu ambazo walizitumia kama mitajiKatika shindano hilo nilipata nafasi ya kutembelea maendeo wanayaoishi
hapa Dar es salaam ili kuwa experience ya aina yake.
 Kama unakumbuka mshindi alikuwa Bi Tatu Mwenda Ngao a.k.a mama keki.

DADA BORA WA KAZI

Mwaka 2012 kupitia leo tena nilifanya shindano la dada bora
wa kazi za nyumbani.Shindano hili lilianza kufanyika mwaka 2011 kwa mara ya
kwanza nah ii ikiwa ni ya pili likiwa na maranikio makubwa sana sana.Shindano
hili linaipa jamii uwezo wa kutambua nafasi na mchango wa dada wa kazi za
nyumbani.Kina dada hawa pamoja na kazi nyingi wanazofanya bado wanadharaulika
na kunyanyaswa majumbani  kisa wametoka
vijijini kuja mijini kufanya kazi.Wanatoka familia za kimasikini,wadogo
kiumri,washamba,hawana elimu ilimradi  fujo
tu.
 Mwaka huu tulikuwa
na mgeni rasmi naibu waziri wa kazi,ajira na vijana mh.Makongoro Mahanga aliyekabidhi zawadi kwa wadada.
Kwa kiasi kikubwa kwa miaka hii miwili jamii imeanza kuelimika kuwa hawa pia
ni watu tena wamebeba dhamana kubwa sana ya maisha yako hapo nyumbani.Kuanzia
wewe na afya yako,watoto wako na hata ulinzi wa nyumba yako kwa nini uishi nae
kama unaishi na mnyama.Katika shindano mabosi ndio hupendekeza kwa nini dada
wake ashinde.Na washukuru sana mabosi woteeeeeeeeeee walioshiriki  jiandae  2013 itakuwa balaaaa.Mwakani nipo kwenye
kuhakikisha kuna kuwa na siku ya dada wa kazi za nyumbani Tanzania.
WOMEN IN BALANCE
Mwaka 2012 pia namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa uwezo wake
nimeweza kusimama na mwenzangu Vida Nasari Mndolwa na kufanya hiki kitu.Women
in balance kitchen party gala.Nilikutana na Vida mwaka juzi akiwa anatafuta Mc
wa kufanya women in Balance nikaongea nae kwa kirefu sana ambapo ilibidi tuunge
nguvu na kuwa kitu kimoja.
 Sababu za mimi kuunga nguvu ni kwa sababu nilikuwa na
wazo hilo hilo ila kupitia leo tena ile sehemu ya kitchen party
yako.Nilishaongea mpaka na team ya marketing kunisaidia kufanikisha but
haikutiliwa mkazo.Hivyo alipokuja Vida ni kama Mungu alipanga iwe hivyoo
tukakaa pamoja na kuiplan vizuri sana.
Na namshukuru sana Vida kwa sababu mie
huwa nina mawazo (ideas)nyingi sanaaaaaaaaaa za vitu mbali mbali vya kufanya
lakini nakosa mtu au team fulani ya kuweza kuyachukua mawazo yangu na
kuyafanyia kazi.Vida yupo agressive kama nilivyo mimi na huwa ananipush kuhakikisha kila tulichopanga kinakuwa. 
 Hivyo
kupitia Women in balance kwa pamoja tumeweza kuanzisha kitu ambacho ni platform
ya wanawake kukutana na kujifunza mengi yahusuyo mahusiano,ndoa,familia,yaani
ulimwengu wa mwanamke ukiacha kazi.Saikolojia ya mwanamke katika mahusiano ya mapenzi au ndoa.
 Nimekutana na kina dada,kinamama wengi
imenisaidia pia kujijengea kujiamini na kukuza Brand yangu ya Dina Marios.Hata mimi mwenyewe nimeweza kujitambua zaidi nafasi yangu katika jamii.Imenisaidia pia kupanua akili yangu na uwezo wangu wa kuwasiliana na watu mbali mbali niwapo kwenye event na hata studio.

DINA MARIOS BLOG

Labda ni kwavile nina mashabiki wengi sana pamoja na kusua
sua sana mwaka huu ku-update blog yetu.Bado ni miongoni mwa blog zinazopendwa sana.Kwa mujibu wa tafiti blog yangu ipo tano bora ikiongozwa na anko michuzi,u turn na jamii forum.Duuuh itabidi mwakani nikaze buti loh.
Mwisho kabisa nawapenda wote mashabiki wangu,nawashukuru wote nyinyi ndio mwanifanya kuwa Dina Marios 2012 mmeniweka juu sana.Japo pia ni kutokana na juhudi binafsi.Yote haya niliyoorodhesha yataboreka zaidi 2013 panapo uzima.
Nawatakia heri ya mwaka mpya 2013 tuendelee kushikamana zaidi na zaidi….mmmuaaaahhhhhhhhhh(busu hilo)

16 Comments

 1. ruky

  December 31, 2012 at 3:45 pm

  Haya tuombe uzima…..Ameen

 2. Anonymous

  December 31, 2012 at 8:02 pm

  NA KATIKA WATU WANAOATHIRIKA NA BLOG HII USIPOWEKA POST NI MIMI DINA,MAANA WENGINE KWENYE REDIO TUMEISHAJARIBU WEEEEEEEEEEEEE MPAKA TUMECHOKA,NIMEBAKI MSIKILIZAJI TU MAANA NIMEKATA TAMAA SANA JAPO UKIANGALIA MIOYO YA WANA LEO TENA NADHANI WANGU UTAKUWA UMEPITILIZA,NAIPENDA LEO TENA,NAISHI NAYO KWA MIAKA NA MIAKA,LAKINI SINA JINSI MAPENZI YANGU KWAKO NDIO YANASABABISHA HAYA,BASI NIKAHAMIA KWENYE BLOG SASA HUKU SINA MPINZANI NI MIE TU KUHAKIKISHA NAINGIA TWENTY 4 7,MATOKEO YAKE NIMEKUWA MUATHIRIKA NO 1 WA BLOGS HASA HII,KASHESHE NI INAPOTOKEA KILA NIKIINGIA NAKUTA PICHA YA MAD ICE UWIIIIIIIII,NILIKUWA NATAMANI KULIA,DINA NAJUA UNASHUGHULI NYINGI SAAAANA ILA JAMANI JITAHIDI MAMA,NAKUPENDA SANA SANA SANA SANA,MUNGU AKULINDE,AKUJAALIE KHERI NA FANAKA KATIKA MWAKA 2013 ILI UENDELEE KUWA MTANGAZAJI BORA NA SI BORA MTANGAZAJI.HERI YA MWAKA MPYA.MAMA ISAAC WA KISEKE MWANZA.

 3. Anonymous

  December 31, 2012 at 8:54 pm

  basi ukiamua kubadilika uwe unatuekea hekaheka km ulivyokuwa unafanya jaman!!!! umetupa jongoo na mti wake

 4. Anonymous

  January 1, 2013 at 6:26 am

  Hi Dina

  Nimefurahi kusikia hivyo nawe pia nakutakia mwaka mpya mwema wa 2013 na uyafanye mengine zaidi ya haya ya 2012.

  Mungu akubariki sana

  Halima

 5. Anonymous

  January 2, 2013 at 6:13 am

  asante kwa busu lakini usipotee sana hasa mimi unanikasirisha ninapoingia na nisikute chochote nilishaanza kukusahau haya kasinge wakola muno waihuka na OYECHONCHE KANDI NINKUNYEGEZA OMULI WEBANGE

 6. Anonymous

  January 2, 2013 at 7:23 am

  thnx mwaya..lov u sana
  kila la kheri 2013 mungu akuongoze inshallah
  hinsy

 7. Anonymous

  January 2, 2013 at 12:30 pm

  yaani hilo busu nahisi umenipiga mimi tu kwa ninavyo kubilivu, ila unajituma sana na unafanya kazi nzuri endelea kaz buti nashauri ungekuwa na mtu wa kukusaidia japo kuwa najua itahitaji mshiko sisi tunaofaidika na blog yako tunaweza kuchangia weka utaratibu tu sh.500 kama kweli unawafurahisha watu kwanini wasichangie hata mia ili upate mtu wakukusaidia any way vigezo na masharti ni muhimu kuzingatiwa

  Mathew Kiondo

  • dinamariesblog

   January 8, 2013 at 10:53 am

   Hahahahahahahaa natafuta kijana bado nikifanikiwa ntawafahamisha.

 8. Anonymous

  January 2, 2013 at 5:13 pm

  Happy new year mdada,braaaavo kwa kazi nzuri,Mungu azidi kutushushia rehema na baraka zake kwa mwaka huu tulioanza na inayofuata.Mama isac umenichekesha Lol. Kwa kweli mad ice alikuwa anaboaje!!kila ukifungua unakumbana na kitu cha mad ice,miaka mia nane! Basi unapata bonge la mtibuko. Usirudie tena mamii.

 9. Anonymous

  January 2, 2013 at 7:39 pm

  asanteee heri ya mwaka mpya. nakuombea dua mwaka huu na upate mume wakooo.

 10. Anonymous

  January 3, 2013 at 2:15 pm

  Happy new year my dear'yani Dinna nakupenda natamani kukutana nawe ila ck moja nitakutafuta mpk hapo kwako Najua ni mkarimu sana,Hongera kwa yote ya mwaka 2012 unatupa changamoto nacc tusipitishe mwaka bila kufanya jambo hatakama ni dogo,(Nakupenda ) mdau mkubwa wa blog ."mama caren" wa kimara.

 11. Anonymous

  January 5, 2013 at 4:55 pm

  ajiri mtu bidada awe ana ku updatia habar huwezi kudominate kote kote

 12. Anonymous

  January 9, 2013 at 1:43 pm

  Da dina kikweli nakupenda sna kupita maelezo yaani niko tayari kukosa nipindi vyote vya cloudsy lakin sikipindi chako mimi ni mdau wako sana naitwa janeth tunaomba uwe unatupia picha za hekaheka kwenye hii blog yako mana gea yeye jamani hata blog hana/ BY JANETH NAISHI TABATA SEGEREA narudia tena nakependa sana mana kuna siku mpaka huwa nawaota usiku wewe,gea na zama

 13. RODA,TBT

  January 10, 2013 at 8:53 am

  happy new year dada dina,i real like what ur doing jaman,god blec u,mwaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!

 14. Anonymous

  January 24, 2013 at 9:23 am

  usijali dina umetishaaaaaaa

Leave a Reply