Uncategorized

MWANADADA RAIA WA KENYA AJIUA AKIWA NCHINI UINGEREZA KISA UPWEKE.

By  | 
 Mwanadada raia wa Kenya aliyekuwa akiishi na kufanya kazi Manchester nchini Uingereza amejiua kutokana na upweke uliokuwa ukimkabili.Marehemu aliyefahamika kwa jina la Sharon Bukokhe alikuwa ni sales manager wa mradi wa family planning kwa nchi za dunia ya tatu.
 Akiwa anaishi Uingereza mwenyewe toka 2002,mume wake akisoma na kuishi nchini Afrika ya Kusini,mama yake akiishi Virginia Marekani,dada yake akiishi Canada..Ndugu pekee aliyekuwa Uingereza ni kaka yake lakini ni mbali sana na alipokuwa akiishi yeye.Jambo ambalo lilimpa upweke sana na kuamua kujiua.Marafiki aliokuwa akiishi nao wanasema alikuwa ni mtu mwenye furaha,akili na mbunifu kiasi amabcho ilikuwa ngumu kujua kama angeweza kufikia hatua hiyo.Mara nyingi alikuwa akisikika kusema ana upweke na anaimiss familia yake na mumewe.
Sharon Bukokhe aliyekuwa na miaka 28 kabla ya kujiua alifanya utafiti wa njia mbali mbali za kujiua kupitia laptop yake.Laptop ilikutwa ndani kwake mlango ulipovunjwa na mwili  kukutwa chini.Kabla ya kujiua alijiremba,akapaka rangi ya kucha na kuvaa vizuri kama mtu anayeenda kwenye mtoko flani kisha akajimaliza.
 Kwasababu hiyo hiyo ya upweke aliwahi kugundulika anaugonjwa unaoitwa bipolar disorder.Ugonjwa huu unakufanya uwe na mood swing ambazo ni dalili ya ugonjwa wa msongo mawazo(depression).

10 Comments

 1. Anonymous

  December 6, 2012 at 11:44 am

  LOH! MH! SIJUI HATA NISEME NINI, NAOMBA UMALIZIE HIYO STORY DINA, NDIO KAJIUA KWA KUNYWA SUMU? KAJIPIGA BASTOLA? KAJINYONGA? KANYWA POMBE KALI KWA WINGI? AU KITU GANI? NA JE AMEACHA UJUMBE KUWA SABABU NI UPWEKE AU WATU WANAHISI TU HIYO NDO SABABU? HEBU FUATILIA MAMA UTUJUZE KWA KINA TUKATE KITU YETU
  CHARITY

 2. Habbie

  December 6, 2012 at 11:46 am

  Wonders shall never end!
  Kama mtu amefikiria kujiua why asifikirie kuachia post alonayo na kuwafuata ndugu zake?

  Any hidden secret??

  Anyways . . . .R.I.P!

 3. Yvonne

  December 6, 2012 at 1:05 pm

  Hi Dina, Inasikitisha sana. Plse naomba nijibu haya maswali hata kwa msaada wa Aunt Sadaka.

  1.Umejuaje kama alikuwa anafanya utafiti wa kujiua kupitia Lap top yake?

  2.Sio ugonjwa kweli??? Coz anaonekana alikuwa na kazi nzuri familia yenye uwezo why ajiue??

  3. Kama kweli ni upweke na ugonjwa wa akili, si angefungasha amfuate either mume wake, mama yake au hata Kaka yake?
  Nitafuhi sana ukinijibu.

 4. Anonymous

  December 7, 2012 at 5:40 am

  Hi Dina, Ukweli inasikitisha sana tena sana kwa Umri wa Mdada huyo, na Why Mume wake Awembali na yeye kiivyooooo!!!!!! kama sio kumchanganya nayeye huyo mume kuwa mbali huko aliko asiishi na Mkewe???? Fuatilia kwa udani kifo cha Mwanadada huyo kiukweli

 5. mama Glory

  December 7, 2012 at 7:50 am

  hakuna ugonjwa mbaya kama kuwa mpweke, ndio maana siku zote nasema kazi inayokufanya ukae mbali na mkeo au mumeo bora uachane nayo.

 6. Anonymous

  December 7, 2012 at 11:27 am

  Hi Dina kiukweli hali ya huyo dada usiombe ikakukumba cha msingi inabidi tujifunze kushirikishana mawazo huwa inasaidia ila naamini kabisa upweke unaweza kukufanya ukafanya maamuzi km ya huyu dada hata km ni millionea..na zaidi kuomba mungu, Dina tupe details its interesting story.

 7. Martha Jacob

  December 12, 2012 at 7:04 am

  Inasikitisha saana jaman.

 8. Martha Jacob

  December 12, 2012 at 7:05 am

  Jamani inasikitisha saaana.

 9. Anonymous

  December 17, 2012 at 1:16 pm

  Inawezekana kabisa, kisaikolojia upweke unaweza kukuua na hasa unapokuwa na mawazo yasiyopata suluhu kutoka kwa yeyote aliye karibu na wewe, halafu na jamii vile vile inaweza kuchangia kwa sababu nchi kama za wenzetu ni tofauti na kwetu huku abambo unaweza usiwe mpweke sana kwani ni rahisi sana kuweka ya moyoni mwako hata kwa mtu asiye karibu na wewe ila umeonana naye first time lakini siyo kwa wenzetu, nadhani mmemmipata.

 10. Anonymous

  December 28, 2012 at 4:29 pm

  Aisee dinah hakuna ugonjwa mbaya kama upweke unaweza kujikuta unafanya mambo ya ajabu sana au ukishdwa kabisa unajikuta unajimaliza kwa kunywa pombe kupitiliza au kunywa sumu kabisa inaumiza sana hakuna kitu kibaya kama kuwa mbali na mwenza wako au familia yako,may her soul rest in peace

Leave a Reply