Uncategorized

NAKUOMBEA SANA REHEMA CHALAMILA URUDI KAMA ZAMANI.

By  | 
Hii ndio picha iliyotawala vyombo vingi vya habari hasa blogs inayomuonyesha Ray C akiwa Ikulu alipokwenda kumshukuru raisi kwa msaada wa matibabu aliompatia.Wote tunaofatilia masuala ya burudani tunajua kwa kipindi kirefu mwanamuziki huyu alikuwa katika hali mbaya iliyotokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Inapofika hatua mtu amekuwa mteja kabisa wa madawa hayo inakuwa ngumu kuacha.Tuna waona ndugu zetu,jamaaa zetu na hata majirani zetu wenye watoto wao waliozama kabisa katika kutumia dawa hizo.Ray C amekuwa miongoni mwa hao sema utofauti yeye ni mwanamuziki aliyependwa na kukubalika na wengi.Iliwaumiza wengi kuona kipaji hicho kinapotea bure nikiwemo mimi sikuchoka kupiga nyimbo zake na kutamani arudi kama zamani.
Binadamu tunaweza kuanguka au kuangushwa na madhaifu yetu na jamii inayotuzunguka kutuhukumu kutokana na matokeo ya kuanguka kwetu.Ray C ulianguka na pengine ulijaribu mara kadhaa kunyanyuka lakini ukaishia kuanguka tena na tena na tena.Jamii ilishiriki kukusaidia mpaka raisi kuingia kati kukusaidia yote ni bahati kwani ni wengi waliopenda kupata msaada kwa namna nyingi kulingana na matatizo na shida zao.
Naomba kweli uwe umeona adha uliyoipata kutokana na madawa na iwe imetoka MOYONI mwako kuwa una NIA ya kurudi upya.Ninaposema kurudi upya simaanishi katika muziki.Hata usiporudi kwenye muziki tena ilimradi umejirudishia thamani uliyokuwa umeipoteza.Wanasema kuacha madawa ni ngumu unaweza ukaacha kabisa ukawa sober lakini baadae ukajikuta umeanza upya.
Niliwahi kupewa story ya kaka mmoja aliyekuwa akitumia dawa za kulevya lakini kwa sasa ameacha.Yeye alikuwa mteja haswaa kila mtu alimshindwa kabisa na kumsusa.Lakini mama yake hakuchoka kumuhangaikia ili aache.Ilifika wakati akawa anaiba mpaka vitu vya nyumbani ili akauze avute unga.Akawa anampa ahadi kila siku mama yake kuwa anaacha.Ataacha wiki wiki ya pili mama anamkuta kwenye viambaza vya ukuta anabembea tu.Mama akanawa mikono na yeye akabaki kumtazama tu akaacha kumsemesha.
Siku moja amerudi nyumbani usiku ana njaa sana akawa amekaa nje maana hata wa kumfungulia mlango hakuna.Mara mama yake akatoka ndani akiwa amebeba chakula anachoenda kuwapa mbwa.Akawa anamuita mama yake ”mama….mama”mama yake kimyaaa wala hakumuitikia.Mama akafika bandani akawapa mbwa kile chakula kisha akarudi ndani akafunga mlango.Yule kaka akawaangalia wale mbwa wakila kile chakula akawaza jinsi gani alivyopoteza THAMANI pale kwao kiasi kwamba wale mbwa wana thamani kumzidi yeye.Siku hiyo hiyo alichukua uamuzi kuwa imefika wakati wa kurudisha thamani aliyopoteza kwake,kwa familia yake na zaidi kwa mama yake.Aliondoka pale nyumbani akaenda kufanya kazi ya kuhakikisha ana acha kutumia dawa za kulevya.Alikaa muda bila ya kuonana na mama yake wala ndugu zake siku aliporudi akawaambia kaacha bado hawakumuamini.Kwa matendo ndio familia ilimuamini kwa kadri muda ulivyozidi kwenda.
Imepita miaka mingi sana hatumii tena na amekuwa akiwasaidia wengine kuacha kabisa.
  Ray C ni binadamu ambae anaweza kuanguaka kama mwingine yoyote.Namuombea awe na dhamira ya dhati ya kujirudishia THAMANI.Nafasi anayo tena kubwa sana kwani bado kijana.

4 Comments

 1. RUKY

  December 11, 2012 at 6:13 pm

  HATA MIMI NIMEFURAHI NA KUFARIJIKA NAPIA NA UHAKIKA MOLA ATAMSAIDIA KUACHA KM AKITAKA WELL COME BACK RAY C WE MIC U DARLING UNAJUA WEWE UNAKIPAJI NA SAUTI KULIKO MWANAMZI YEYOTE HUKO BONGO….KUBALINI MKATAE….RAY C HAPANA CHEZEA KABISA…

 2. Anonymous

  December 19, 2012 at 9:28 pm

  Rehema umebahatika sana kusaidiwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ili kuachana na yale "madudu". 1. Pongezi Mh. Rais wetu mpendwa JK kwa utu wako. 2. Ray C, nakuomba sana usimuangushe Rais wetu. 3. Achana na "marafiki" ambao hawakutakii mema. 4. Rudi kwa familia yako, hasa mama mzazi wako. 5. Kila la heri.

 3. kilimo kwanza

  December 20, 2012 at 2:56 am

  Mh Rais naomba usaidie na wengine sio mateja tu! Hebu nenda na hapo kwa majirani zako ocean road kituo cha magonjwa ya saratani uone ni jinsi gani watu wanavyoteseka bila kola lolote! Lakini huyo teja uliemsaidia imetokana na starehe zake mwenyewe, na nina uhakika anauwelewa mzuri wa madhara ya madawa ya kulevya toka alipokuwa mtangazaji na bado akajitumbukiza kwenye ulevi huo!

  Mh, msaada wako ni kweli una nia nzuri ila kwa maoni yangu mateja hasa kama huyo Ray C sio kipau mbele kabisa! Mfano mwingine ni Mzee Kaboyonga mpaka amefariki dalili zilionekana mapema! Tumemwona wakati wa uchaguzi wa ubunge wa EALA mzee wa watu hata miguu imegoma, alikuwa akitembea kwa fimbo, a such brilliant person! Ambae angeendelea kutusaidia sana watanzania kuliko burudani ya huyo binti ambayo ina substitute kibao!

 4. Anonymous

  December 28, 2012 at 5:36 am

  chezea madawa wewe ,mshukuru sana huyo baba jk

Leave a Reply