Uncategorized

PESA NA MAJINA YAKE

By  | 

PESA INA MAJINA MENGI KULINGANA NA MAHALI NA MATUMIZI
1.Kwenye ibada inaitwa Zaka/sadaka
2.Msibani inaitwa rambirambi
3.Shule inaitwa Ada au Karo
4.Kwenye vyombo vya usafiri inaitwa nauli
5.Ukiinunulia haki inaitwa rushwa
6.Kumdhamini mtu mahakamani inaitwa dhamana

Mengine tukumbushane?

18 Comments

 1. Anonymous

  December 4, 2012 at 7:40 am

  Dina dear, usikatishwe tamaa na watu wachache wasiokupenda na wanao tafuta blog zenye kuruhusu matusi kukuharibia jina lako. Nimesikitika sana, jinsi mwenye blog mmoja alivyo achia comment za ajabu kuhusu wewe na zamaradi, kuna mda binadamu unatakiwa kutumia akili tu kufanya maamuzi na mtu kama owner wa blog una uwezo wa kuruhusu comment itoke au isitoke. Nilimwandia ujumbe huyo blogger kumwambia kuwa si vema alivyo fanya. Inasikitisha sana, mtu kuruhusu blog yako iwe ndio sehemu ya watu kutolea mahasira yao, na mawivu yao kwa watu, bora uweke comment lakini usiweke majina ya watu.

 2. Anonymous

  December 4, 2012 at 7:47 am

  Ikilipwa kwa mfanyakazi huitwa mshahara na ikilipwa kwa kibarua huitwa ujira. Ililipwa kwaajili ya pango la nyumba huitwa kodi ya nyumba.

 3. Anonymous

  December 4, 2012 at 9:03 am

  kwingine inaitwa Hongo

 4. Anonymous

  December 4, 2012 at 9:55 am

  ukilipia pango inaitwa kodi, ukitoa kwao na mwanamke kwa ajili ya kuoa inaitwa mahari, ukimpa mtu inaitwa msaada.

 5. pam

  December 4, 2012 at 10:18 am

  kwenye vikao vya harusi inaitwa uchakavu

 6. Anonymous

  December 4, 2012 at 11:01 am

  1. ukinunua bidhaa ikibaki inaitwa chenji
  2. kwa walevi ukitoa kwa baa medi inaitwa bakshishi (tip)

 7. Anonymous

  December 4, 2012 at 11:55 am

  ANONYMOUS 1 NAKUUNGA MKONO KABISA HATA MIMI SIKUFURAHISHWA KABISA NA BLOG HIYO KWANI NAONA HALIFURAHI SANA KUONA MIJIMANENO INAYOWAHUSU WENZAKE NAYE AKAFURAHISHWA SIYO VIZURI KABISA JAMNI KWANI DINA NA ZAMARADI WALITOKA WAPI KWENYE MAZUNGUMZO YENU !! DINA TUNAKUPENDA SANA SISI WASHABIKI WAKO NAMBARI ONE HIVYO WASIKUSUMBUE MTOTO!!

 8. ruky

  December 4, 2012 at 5:21 pm

  jamani kumbe wengi mliona hata mimi kwakweli nilichukia sana mwenye blog tatizo lake anatafuta umaarufu wake uliyopitwa mwaka 47 anatafuta umaarufu kwanguvu zote kila akijaribu hakuna mtu anamuona sasa anapoona watu km kina dina na zama wamemkuta kasaaulika alafu wao wana shine like diamond anatafuta pakuwashushia wakuache mtoto wa watu dina wetu we love u girl

 9. Anonymous

  December 5, 2012 at 5:45 am

  Yule ana utindio wa ubongo mumsamehe tu na ameathirika na ugonjwa wa wivu na chuki ndo maana anaachia zile commet za zamaradi

 10. Anonymous

  December 5, 2012 at 12:31 pm

  ukilipia ili upate mke inaitwa mahali

 11. Anonymous

  December 6, 2012 at 11:05 am

  KATIKA MICHEZO YETU YA KUHAMISHIANA PESA MTAANI KINA MAMA TUNAIITA UPATU

 12. Anonymous

  December 6, 2012 at 5:49 pm

  in Russian tunaiita Dingyi (деньги)

 13. Ald

  December 7, 2012 at 10:35 am

  tukitaka kufungulia biashara tunaita MTAJI/CAPITAL

 14. Anonymous

  December 9, 2012 at 6:56 am

  Ikiwa kipato kwa wafanyabiashara inaitwa FAIDA,

 15. Anonymous

  December 11, 2012 at 10:14 am

  ukipewa na mwajiri kwa matumizi ya safari inaitwa posho ya safari, mshahara ukikatwa kila mwezi na kuhifadhiwa katika shirika la hifadhi ya jamii na ukadai pesa yako baada ya kuacha kazi inaitwa mafao au penshini. shirika la umma likingezewa au likipewa pesa na serikali yake inaitwa ruzuku.

 16. Anonymous

  December 19, 2012 at 9:01 am

  Kwenye Semina au Vikao inaitwa supporting Documents

 17. Anonymous

  December 19, 2012 at 11:07 pm

  nawapa tano wote mliochangia mada hii kweli mko juu

 18. Anonymous

  February 21, 2013 at 6:09 pm

  Wakati mwingine ikitoka kununua haki inaitwa mlungura

Leave a Reply to Anonymous Cancel reply