Uncategorized

SAFARI NDANI YA TRENI…DAR MPAKA MORO(DMM)

By  | 
 Safari ilianza saa mbili asubuhi kuelekea huko Morogoro katika kijiji cha kisaki.Hii ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 13 ya clouds fm.
 Wanaclouds fm pamoja na wasikilizajinwadau mbalimbali wa ujumla tuliungana katika safari hii.Lengo lilikuwa kufurahi na kula bata pamoja.

 Hili ni eneo ambalo treni inapita katikati ya mwamba.

 Mbuga ya Selou tulijionea wanyama kama vile swala,tembo,twiga na nyumbu

 Ndani ya treni kulikuwa na mziki watu walikuwa wakiruka debe harariiiiii
 Kijijini Kisaki tulipofika kulikuwa na ngoma za kiasili
 Tulishuhudia bwawa la maji moto

 Nyama zilichinjwa na kuchomwa mambo ya kuku wa kienyeji,swala,mbuzi na ng’ombe.Wenyeji nao walichelewa kuchoma lakini watu walikula japo kwa kuchelewa kutkana na njaa na hamu.

Saa kumi na moja safari ilianza ya kurudi Dar es salaam.Nasikia mwakani itakuwepo nyingine ikiwa imeboreshwa vizuri zaidi maana tunaamini mapungufu yalikuwepo.Ila panapokuwa na mapungufu ndio unapata kujua namna ya kuweka ubora.Ila safari ilikuwa nzuri sana.

1 Comment

  1. Shangwe

    December 31, 2012 at 2:14 pm

    Nice

Leave a Reply