Uncategorized

KARIBUNI AZURA HEALTH AND FITNESS TUFANYE MAZOEZI!

By  | 
Wale wapenzi wamazoezi mnakaribishwa sana Azura Fitness Centre kujiweka fit.Wale wenzangu na mimi tunaotaka kutoa manyama uzembe njoo tujiunge.Wapo wazi siku zote kuanzia alfajiri mpaka saa nne usiku.
Kuna wakati nilianza hapa tena nikapewa ofa ya kuleta watu wawili wadau wangu wa blog lakini sikufanikisha.Majukumu yakawa mengi safari za hapa na pale sikuendelea.Ila sasa nimerejea rasmi na ilinilazimu kukutana na mtaalamu wa afya na chakula kwa vipimo na maelekezo maalum kabla sijaanza mazoezi.Hivyo vikombe ni kwa ajili ya vipimo vya chakula zile potion.Kwa sisi ambao hatubebi zege wala kufanya kazi ngumu lazima ule kidogo kidogo kwa maana ya potion ndogo ndogo.Ukichukua thermos kile kikimbe kidogo ndio utakipimia kama ni ugali,wali kwa ujazo ule.Na mboga ndio iwe nyingi hasa ya majani.Lakini chakula kingiii kinaenda kinakaa mwilini kwa sababu hakitumiki kinaenda kuifadhiwa mwilini na kugeuka kuwa mafuta.
Pia tukapima kwa tape measure maalum sio ile ya fundi nguo hahahahahah.Hapo tulipima mikono,kifua,tumbo,paja,hipsi yaani yale maeneo ambayo mafuta hukaaa.
Sehemu ambayo huwa inasisitiziwa isiwe na mafuta ni tumbo,mafuta ya tumboni sio mazuri kabisa.Katika kipimo hiki mwanamke akiwa ana cm 60-80 yupo normal,akiwa na cm 80-88 unaingia kwenye hatari na akiwa kwenye cm 88 na kuendelea uko kwenye hatari.
Na mwanaume tumbo lake anatakiwa kuwa na cm 69-94 ndio yupo normal,cm 94-102 unaingia kwenye hatari,cm 102 na kuendelea ndio upo kwenye hali mbaya.
Na miee nikapima tumbo langu,mtaalamu anasema tumbo ndio chanzo cha mtu kuweza kupata magonjwa yatokanayo na unene kama pressure,sukari au moyo.Ndio maana wanashauri sana kufanya mazoezi kuondoa kabisa kitambi.Mie langu lipo kwenye cm 97 ambayo sio nzuri natakiwa kurudi angalau 80.
Nikapima uzito na urefu kwenye hiyo Weight scale ,maana unaweza kuwa na uzito ambao hauendani na urefu wako.Wenyewe wanaita kipimo cha kupata body mass index. Mie uzito wangu kg 87 na urefu m 1.67
BMI=BW(kg)/BH (m)2 jibu likiwa 18.5 upo under weight
18.6-24.9 hii ni normal weight
25-30 over weight
30-35 obese
35-40 obase stage 1
40-45 obese stage 2
Mie mwanawane niko kwenye 32 inamaana natakiwa kutoa kg 32.Natakiwa niwe na kg 67 kwa sababu ya ukubwa wa mifupa yangu siwezi ntachekesha iwapo ntafikia uzito huo mtaanza kuninyooshea vidole natafuta 75 kgs tu.
 Mazingira ya kufanya mazoezi ni mazuri kiukweli kuna options nyingi za kukufanya wewe ufurahie mazoezi.Kuna mwalimu wa kufundisha kuogelea maana kuogelea nalo ni zoezi pia.
   Mie huwa napenda sana kukimbia huku nje maana nimeambiwa pia kukimbia inasaidia kuburn fat haraka.Huwa nakimbia sio mbio za mwanariadha kimtindo kwa dk 30 hivi.Huku nje huwa tunacheza volley ball pia.
Kuna siku za YOGA jumanne na jumamosi naipenda inasaidia sana kustretch na flexibility ya mwili.Trainer wa kichina noma huyo mtasimaia mpaka vidole na vichwaa.Hapa kuna masomo aerobics, yoga na pilates.
Vifaa vipo vya kutosha wewe tu..
Matrainer wapo wa kutosha
Mazoezi ya kitambi mwe!
 Kitambi nomaaa..wale watu wangu wawili bado nafasi ipo ila nimeambiwa kwanza nipungue mimi ndio niwalete.Ndio maana nakazana hapa nina wiki ya pili.
AZURA HEALTH AND FITNESS wapo Kawe ukimaliza tu daraja kama unatoka mikocheni au piga simu
Tel. +255 786 089780 kuulizia bei na ratiba
 
Karibuni mie naingia kila siku saa kumi jioni mpaka saa moja.

27 Comments

 1. Anonymous

  January 17, 2013 at 12:55 pm

  dada dina pole na hongera sana kwa mazoezi.. ila dawa ya kuepuka kitambi usile vyakula vilivyolala ndiyo vinachangia sana kukua kwa tumbo.. is not easy kula chakula fresh kila siku ila huo ndiyo ukweli.

 2. Anonymous

  January 17, 2013 at 1:05 pm

  Hongera kwa uamuzi mzuri wa kufanya mazoezi. Napenda sana volleyball, sijapata tu muda na sehemu nzuri ya kucheza, ni mazoezi mazuri esp ukimix na jogging.

  Bigup…

 3. Anonymous

  January 17, 2013 at 1:06 pm

  aka Observer

 4. Ruky

  January 17, 2013 at 3:17 pm

  Hi Dina kufanya mazowezi ni vizuri lakini km utaendelea kula vyakula vya wanga mbona hutopungua utazidi kupanuka km baunsa..kula kidunju wanga mengine mchemsho…ya samaki,maji mengi, matunda matunda…nk

 5. Anonymous

  January 17, 2013 at 3:56 pm

  MTOTO WA KIKE KWAPA SAFIIIIIIIIIIIIIIIII KWELI MWANAMKE MAZINGIRA. UMENIFUAHISHA SN MWAAA

  • Anonymous

   January 18, 2013 at 3:42 pm

   Umeona eeeh, jamani Kuna wanawake wakinyanyua mkono mi nataka kulia.Pse pse jamani tujali hii sehemu kama tunavyojali uso.

 6. Anonymous

  January 17, 2013 at 6:17 pm

  Hi Dina

  Hongera kwakuanza mazoezi tena

 7. Anonymous

  January 17, 2013 at 7:47 pm

  habari, nimeurahi kusikia umeanza mazoezi tena, kila la kheri, kwasababu mambo mengi huingia hapo katikati na unajikuta umeachia njiani, sikulaumu huwa hayadhibitiki wakati mwingine…. kwangu mimi wewe ni mfano, ni mkweli na juu ya yote huwa unachukua mambo kama yalivyo, napenda sana huo msimamo…nimejitahidi kweli nisiweke kiingereza hapo katikati kwasababu mwaka huu hilo ni moja ya malengo yangu.kila la kheri dada.

 8. Anonymous

  January 17, 2013 at 7:55 pm

  kweli dinah unaonekana mazoezi hayakuwa sehemu ya maisha yako kwanzia mdogo,,pole,,,kazana utafika tu unapotaka,una shape nzuri anyway,kazana tumbo,,,fanya mazoezi kuwa starehe yako,kilevi or somethin,utaenjoy zaid,,,best of lucks mamy

 9. Anonymous

  January 17, 2013 at 8:31 pm

  Watu watakwenda sana hapo ili wakuone tuu. Haya Dina kila lakheri, mimi nakupenda sana wewe. Nami nina 100kg kwahivyo najua ugumu wa kutafuta wembamba.
  Christine

 10. The Lot

  January 17, 2013 at 9:11 pm

  sasa dada yangu wengine kazi zetu hazieleweki,2najua muda wa kuingia kazini ila muda wa kutoka ndio hatujui na tunatamani sana kufanya mazoezi hivyo tunashindwa kutokana na muda,sasa hivo vitambi sijui hata tutavitoa vipi.

 11. Habbie

  January 18, 2013 at 12:37 am

  Na kwa wale wembamba tunaotaka kuongeza kamwili tupate walau viminofu vya kujazia hizi skeleton zetu . . .vipi huduma inapatikana??

  Hahah manake hizi afya mgogoro nazo . . duh!
  Mtu unajikuta una mwili ambao hauendani hata na umri wako atii!

 12. EMMIE KAHERE

  January 18, 2013 at 7:16 am

  Soon i will join you there

 13. Mama 2 (Mrs M)

  January 18, 2013 at 9:45 am

  Hongera sana Dina kwa mazoezi!

 14. mama Glory

  January 18, 2013 at 9:53 am

  dawa ya kupungua ni kuwa na mawazo, lakini mazoezi ni kujiongezea hamu tu ya kula, kuna unene wa asili kuna uwembamba wa asili, kwa mfano mimi ni mwembamba toka nipo tumboni mwa mama yangu,ila nikiwa mjamzito utanisahau nanenepa mpaka najijutia, lakini nikishajifungua mwili wangu unarudi wenyewe bila dirt wala mazoezi,so mi nasema kila mtu na mwili wake, ila tufanye mazoezi kwa afya ya miili yetu na sio kwa sababu ya kupungua.

 15. Anonymous

  January 18, 2013 at 10:38 am

  Mambo Dina naomba upost ile diet ya kabichi nataka nianzie hapo ukichanyanya na mazoezi ntakuwa vizuri kwa muda mchache.

 16. Anonymous

  January 18, 2013 at 8:00 pm

  dah hii hatareeee,matrainers wako ivo?watu watapona kweli na ayo mashallah mtoto uko bomba ivo hahahahaa.aya tutakuja ata mie nataka kupungua mana mwili siuelewi naona nanenepa tu ilhali najizuia kula-kula

  • dina marios

   January 21, 2013 at 11:24 am

   karibu njoo tufanye mazoezi dada…hahahaahahah matrainer hawana shida na mtu kazi yao ni kukufanyisha mazoezi uwe fit.

 17. Anonymous

  January 18, 2013 at 10:46 pm

  mama Glory, kuwa na mawazo sio sababu ya kupungua, inategemea na mtu,me nikiwa na mawazo nakula sana mpaka utanionea huruma! maana kla nikila sishibi! matokeo yake nanenepeana km gunia la viazi utamu! then mawazo yakiisha huwa napungua vizuri kwani huwa naweza kujicontrol kwa chakula, me sina muda wa kwenda gym, ninachofanya kila asb kabla cjaenda kazi naruka kamba(jump rope) pia lazima nifanye zoezi la tumbo chumbani kwangu kila cku, cku nicpofanya zoezi la kamba na la tumbo huwa najiskia km mgonjwa! pia kumbuka ukianza zoezi la tumbo inaweza ikakuchukua muda wa miezi 6 ndo ukaanza kuona matokeo ya tumbo kukaza/kupungua! so usiwe na haraka ya kuona matokeo, kwa wapenzi wa muziki unaweza ukawa unadance like 1hr kla cku, unahakikisha unadance kweli mpaka jasho linakutoka, hip pop, bolingo au rnb inategemea unapenda mziki wa aina gani, pia inasaidia sana kupunguza mwili ila usisahau kuzingatia mlo wako! beer mwiko, nyama za kuchoma kwa nadra….. ila kuacha beer yataka moyo sana hahahahahaha

 18. mariah

  January 19, 2013 at 11:50 am

  Mambo mumie,mi nataka kujiunga na zoezi,ambapo nitakua naingia jimmy saa kumi na mbili baada ya kazi,nahitaji kujua bei zao plz

  • dina marios

   January 21, 2013 at 11:11 am

   Karibu sana,mwisho kabisa nimeweka namba ya simu ya wewe kupiga kuuliza..maana kuna malipo ya siku,mwezi,miezi mitatu,sita,mwaka n.k

 19. Anonymous

  January 22, 2013 at 5:29 am

  Dina Mambo vp?
  pole kwa majukumu uliyonayo ila nilikuwa nakuomba uipost tena ile diet ya kabichi.

 20. Anonymous

  January 22, 2013 at 10:47 am

  Hongera Dina nakupenda sana kwa kupenda kuonekana smart unajua tuseme kweli mwanamke figure bwana mm ni mnene ila nimeanza ile diet yako sasa nina wiki ya 2 nimepungua mno kama kilo 7. na bado ninaendelea nayo ila hapo juu nimeona hapo kama vile mpangilio wa diet please usituache maana sisi ni wa mikoani na tunataka kupungua pia.
  Nikutakie kila la kheri na nina hakika utapungua tu.

 21. Anonymous

  January 23, 2013 at 9:49 pm

  dada dina kwanza kabisa nakupongeza kwa mazoezi,na nakushauri uendelee ila pawepo na uwiano wa mazoezi na chakula umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza mwili na natumaini ukiendelea utafanikiwa zaidi,pili naipenda sana blog yako ina mambo mazuri ya kuelimisha! napenda pia mazoezi,nitajiunga nawe hivi karibuni!

 22. Anonymous

  January 24, 2013 at 10:22 am

  dina hiyo nafasi ya hao wadau wawili naomba na mie niwemo, natamani sana na muda ninao kuanzia saa 10:30 jioni, nipe dada hiyo nafasi, namba yangu 0752 110517 nipe mama nasubiri nimeshavaa kipensi hapa

  • Anonymous

   January 24, 2013 at 12:31 pm

   Lol some ppl just have have a gud sense of humor!!

 23. Anonymous

  January 24, 2013 at 1:29 pm

  Dina i like your blog na kipindi chako kwasababu unatuelimisha mambo mengi….ahsante sana…….

Leave a Reply