Uncategorized

MAPENZI YANAPOKWISHA …MASKINI HUYU DADA…

By  | 
Ilikuwa ni Sinza mama huyu alitupwa nje ya nyumba baada ya kuvamiwa na mabaunsa chini ya usimamizi wa polisi.Ambapo mama huyu alisema mtu aliyenyuma ya tukio hilo ni aliyekuwa mume wake.Akisimulia kisa anasema yeye na huyo aliyekuwa mume wake wamekuwa na mvutano juu ya hiyo nyumba.Alioana na mumewe mwaka 1998 na kuhamia katika hiyo nyumba mwaka 2000.Mwaka 2007 ndio migogoro ilipoanza baada ya mwanaume kuanza kutokurudi nyumbani na hatimae kutokurudi kabisa.Katika ndoa hiyo wana watoto watatu.Kwa muda wote mume amekuwa akitaka kumtupa nje na watoto wa kigezo kuwa hiyo nyumba sio yake mwenyewe anaitaka.Siku ya tukio jana yake mume alikuja akawachukua watoto akisema anaenda kuwanunulia vifaa vya shule hakuwarudisha.Asubuhi mama anashangaa watu wanaruka ukuta na kuvunja milango kumbe wamekuja mabaunsa na polisi kuwatupa nje.Tukafatilia kwa kumpigia kamanda wa polisi kanda ya Kinondoni na mkuu wa kituo cha polisi osterbay ambako polisi walitoka huko kusimamia zoezi la kuhamishwa mama huyu.Tukaambiwa wao walipata barua kutoka mahakamani kuwa wanahitajika kusimamia ulinzi wakati mpangaji wa nyumba hiyo akitolewa nje.Mwanasheria wa huyo mama anasema wana kesi mahakamani kati yake na huyo mume ambayo haijaisha na inatarajiwa kusikilizwa kwa mara ingine tarehe 2 mwezi ujao.Na mbaya zaidi yeye hajapewa taarifa kuwa ahame ila amevamiwa.
Vitu mbali mbali vikiwa nje baada ya kutolewa nje na ndani kuwekwa mabaunsa kulinda asiingie mtu.
Kama kuna kitu kiliniuma ni huyu bibi pichani.Huyu ni mama wa huyo dada na bibi wa watoto hao ambao walikuwa likizo muda wote shule zilipofunga.Bibi ndio alikuwa amewaleta wajukuu zake na kuishia kushuhudia mwanae akitupwa nje na mabaunsa akiwemo na yeye ni udhalilishaji wa hali ya juu.Nilikuwa namuangalia bibi wa watu na machozi kunilenga majirani wanasema hata kula hakuwa akitaka kula amekaaa kimyaa tu.
Majirani wote walikuwa na huyo mama hasa wanawake wakiongea kwa jazba juu ya mkasa huo.Wakieleza jinsi gani hakupaswa kumfanya hivyo mtu aliyezaa nae watoto tena watatu na wote walikuwa wakiishi na mama yao.

Jioni majirani wakamsaidia kuhifadhi vitu kwenye nyumba zao

Mwenye kubeba kabati,vifurushi vya nguo,vyombo ilimradi wamsitiri mwanamke mwenzao.
Usiku majirani walifanya fujo sana kiasi cha mapolisi kuingilia kati…ishu ilikuwa huyo anaedai ndio mwenye nyumba ajitokeze.Alikuja mpaka diwani wa eneo hilo polisi pia wakaja kuwatoa hao mabaunsa na mama wa watu kurudishwa ndani ya nyumba.
Jana aliamkia mahakamani na mahakama kuamua akae kwenye hiyo nyumba bila kubugudhiwa mpaka kesi yao itakapoisha.Sikiliza heka heka ya leo utakisikia kisa hiki.

38 Comments

 1. Anonymous

  January 16, 2013 at 10:04 am

  Hi Dina

  Kweli jaman mtu ulizaa nae unaweza kumfanyia unyama huu mkeo,Hebu kina baba kuweni na huruma na kama kesi aijaisha kwann atolewe vitu vyake nje tena kwa kutupwa km sio kwake na mbaya zaidi mbele ya mama yake mzazi,tuwe na utu wote ni wa pita njia tu katika dunia hii

 2. Anonymous

  January 16, 2013 at 10:07 am

  Oooh! Jamani nimeumia..pole mamie utalipiwa na M/Mungu.

 3. Anonymous

  January 16, 2013 at 10:16 am

  Hizi roho nyingine kweli balaa? Sasa huyo baba ndio nini kumdhalilisha mama wa wanae hivyo?

  Afadhali maamuzi ya watu wa nchi za wenzetu, uliyeamua kujiengua ndio uondoke kwenye nyumba ukaanze upya!

 4. Anonymous

  January 16, 2013 at 10:17 am

  Mimi ni mwanaume na baba wa watoto. Kitendo alichofanya huyu baba si chakiungwana hata kidogo. Awafikrie kwanza watoto wake na mama aliemzalia watoto hao, yeye aendelee kuishi huko ambako ameishi miaka yote, hapo amwachie mke na watoto.

 5. Anonymous

  January 16, 2013 at 11:38 am

  ndio maana nwdays wasichana wengi hawataki kuolewa. sasa ukiona wenye ndoa ndoa zenyewe ndio hiziiii?? waiii!!! hayo ni machache tu tunayoweza kuona na kuonyeshwa kwenye vyombo kama ivi na yale yasioripotiwa?? jamani tubadilike tujenge taifa lenye vijana wenye maadili mema. coz apo embu fikiria hao watoto watakua na malezi gani apo sasa..?

  • Anonymous

   January 17, 2013 at 10:03 am

   Alie vunja ndoa ya huyu mama ni msichana vile vile au mwanamke. Wanawake ni wachawi wa ndoa zao wenyewe.

  • Anonymous

   January 20, 2013 at 4:27 pm

   Yes pengine ni mwanamke au msichana. Ila kumbuka MUOSHWA HUOSHWA.

 6. Anonymous

  January 16, 2013 at 12:55 pm

  Kweli duniani kunamajaribu jamani lakini huyo mwanaume ajafanya vizuri hata kidogo na malipo nihapa duniani! Mungu amsaidie tu huyo mama naaone nimapito yatakwisha tu.

 7. Anonymous

  January 16, 2013 at 1:41 pm

  huu udhalilishaji unapita mipaka sasa! tunaomba sheria kali zichukuliwe dhidi ya huyo baba ili awe fundisho kwa wengine….mambo gani hayo sasa amefanya?alitaka huyo mama akaishi wapi na hao watoto? nimekwazikaa sana na hii newz.
  .lily arusha.

  • Anonymous

   January 18, 2013 at 8:28 pm

   ndi twendeni tukaipiganie hii haki kwa mchakato wa katiba unaopita sasa!!tuhakikishe sheria inamlinda mke na watoto wake yani mali ya mume nusu yako whether umezaa nae watoto au haukubahatika watoto…na kwa kofi moja atalokupiga segerea wiki nzima ndipo watanyooka hawa shwaini…TUSIBWETEKE AKTIBA NDO MKOMBOZI WETU

 8. Anonymous

  January 16, 2013 at 1:53 pm

  Machozi yamenitoka nimehisi huyo bibi ni kama mama yangu ndio anaona nafanyiwa hivyo jamani kuna unyama ila huu!ni too much. Heri watoto hawakuwepo wangeathirika sana kisaikolojia.
  Ndio maana wakati mwingine hawa mabaunsa hua wanauliwa. Unakumbuka ile yamadale na watu wa sinza nao wangewabonda hata na mawe. Ngedere pori kabisa

 9. Ruky

  January 16, 2013 at 1:58 pm

  mmmmh maneno yameniishia haya mii natagaga nia nchi za watu mpka nigine maaana serekali inatujali sana wanawake kwa ujumla na wanachi wote hapo ninge piga 999 dk 4 hawamalizi wapo mlangoni ungeona huyo mama angelipwa mamilioni na huyo baba angeiyona hiyo nyumba na watoto kwenye picha…hata wanzania wenye kuujinga km huu subutu yake kumfanyia hata awara chamoto atakiona chezea chi ya Qeen

 10. Emmie kahere

  January 16, 2013 at 6:30 pm

  Ee yesu,mpe nguvu mama huyu.me naamin huyu baba atakuja kujuta kwa alichomfanyia huyu mama,kwanza kajidhalilisha mbelehata ya mamamkwe.,mmh ndoa hiz jaman. 2ombe tu

 11. Anonymous

  January 16, 2013 at 9:50 pm

  BAADHI YA WANAUME WANAWEZA KUWA SI WATU DUNIAN.DHULMA GANI HII ANAYOTAKA KUITENDA .KUNA SIKU NILIULIZWA KWANINI NIMEOLEWA NA MZUNGU NILISEMA SIMCHUKII MWANAUME MWEUSI KWAN NDO BABA YANGU.LAKINI NSAJARIBU SIDHANI KAMA NTAOLEWA NAE TENA YALINIKUTA .LAKINI KUNA VITENDO WAFANYAVYO WANAUME WAKWETU WEUSI HAVILINGANISWI HATA NA VYA MNYAMA.SHERIA YA WENZETU UKIOLEWA HATA KAMA WEWE MGUMBA LOLOTE LIKITOKEA UNAPEWA NUSU YA MALI HATA KAMA HUKUCHUMA NAE.HAOWI MKE WA PILI NA HANA KIMADA NA AKIPATA ANAFANYA KISHA HAWAKUMBUKANI HATA KWA SALAM JAMANI SIMAMIENI HAKI ZA WANAWAKE WENZETU TANZANIA MPAKA LINI WANYANYASWE

 12. Anonymous

  January 17, 2013 at 8:13 am

  jamani mi nimetoka kutendwa na boyfriend yaani hapa ndo kidonda kinapona lakini hii picha imeibua yoooote yaliyolala,jamani naumia mno mno mno eh Mwenyezi MUNGU tunusuru jamani, na sitashangaa kama ni huyo mwanaume kashurutishwa n kimada, kweli adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, siolewi ng'oooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

 13. Anonymous

  January 17, 2013 at 8:28 am

  so sad ,no comment!!

 14. Anonymous

  January 17, 2013 at 9:03 am

  wanaume kurukaruka kwao kuna waponza, anaenda anatembea na mwanamke wa nje wanawake wengine wachawi balaa sio akili yake huyo baba, me nimewahi ona mama anafukuzwa tena na mtoto mdogo usiku sana na mvua inanyesha, halafu watu wakaja kumsaidia huyo mama yaani mtu akishika vitu vya huyo mama yule baba anakuja anakupiga kifupi hakutaka mama apewe msaada wowote. kibaya zaidi huyo mama akaondoka ila huyo baba bado akawa anaendelea kumtumia msg za kumtukana yeye pamoja na ukoo wake. wanaume endeleeni tu kurukaruka na wanawake wa hapa mjini mtakiona cha moto. sasa km mkewe alikuwa na kosa matusi ya nini kwa ukoo. mama wa watu aliondoka kistaarabu, hakudai hata kijiko, alisema sitaki ugomvi na mtu, ila bado huyo baba anamchokonoa mara hivi mara vile, nawaambieni wanaume wote msiotulia na wake zenu matakiona cha moto. mnanyanyasa wenzenu utadhani hawajazaliwa. mkumbuke dunia tumeumbiwa wote .

 15. Anonymous

  January 17, 2013 at 9:18 am

  Sasa hapo ndio wangeulizwa TAMWA wanafanya kazi gani, mie naona wangeweza kuandamana kwa ajili hii, au sio uvunjwaji wa haki za binadamu? au wao si ndio wanaowasimamia wanawake kisheria? Au mnaonaje?

 16. Anonymous

  January 17, 2013 at 9:26 am

  hii yote ni wanawake tunapenda kubweteka alivyoona dalili shosti alitakiwa kuchukua hatua mapema! mwanamke kazi bwana

  • Anonymous

   January 18, 2013 at 12:22 pm

   Kazi???? we temea mate chini upite.

  • Anonymous

   January 20, 2013 at 4:33 pm

   Naamini hujui ulizungumzalo. unajua background ya huyu mama au unaongea tu mradi mdomo umetamka au ameshawahi kukuomba msaada? maana nimeelewa huyu baba alihama nyumba sasa naomba nikuulize kama hana kazi wewe ndio ulikuwa unampelekea pesa ya matumizi? Naamini huna hata miaka 25.

 17. Anonymous

  January 17, 2013 at 10:53 am

  Mmh!imenisikitisha sana kweli wanaume wengine ni wanyama, M /Mungu ampe uvumilivu mwanamke mwenzangu.

 18. Anonymous

  January 17, 2013 at 5:20 pm

  Wewe unayesema mwanamke Kazi unamaanisha nini? Mwenzio amechukua hatua Kesi ii mahakamani sasa hatua nyingine ipi? Huyu ni mke halali maana amekaa naye Zaidi ya Miezi Sita. Huyu baba Njaa tu inamsumbua Hana lolote na roho yake ya kwanini? Atakufa na umaskini na umalaya wake.

 19. The Lot

  January 17, 2013 at 9:22 pm

  Mimi ni mwanaume,ila sometime sisi wanaume tunaboa sana,sijampenda huyo jamaa aliyefanya hivyo,mi namuita muuaji.Embu fikiria wasingepata hifadhi kwa majirani wangeenda wapi?Si ndio mwanzo wa watu kuvamiwa na watoto kubakwa.I HATE HIM.

 20. Anonymous

  January 17, 2013 at 11:15 pm

  Inauma sana jamani,hivi hyo baba ana roho ya paka au?

 21. mama Glory

  January 18, 2013 at 9:33 am

  mpaka lini wanawake wa kiafrika hasa tanzania tutanyanyasika? nimesikitika sana, mammy usikate tamaa na malipo ni hapa hapa duniani Munngu atakusimamia na kesi utashinda, pia kuna mdau hapo juu anasema angechukua uamuzi mapema, napenda kumwambia kuwa usione wanawake wanavumilia kwenye ndoa pamoja na manyanyaso yote hayo ni kwa sababu ya watoto, wazazi wanapotengana wanaoumia ni watoto, mtoto ana haki ya kupata malezi ya baba na mama, ushauri wangu kwa wanandoa maombi na swala ni silaha tosha ya kulinda ndoa yako.

 22. Anonymous

  January 18, 2013 at 8:22 pm

  apa ndo nnasema hawa watoto wa kiume tuliowazaa sie wasituletee za ushenzi siku tutawashughulikia watukimbie kabisaaaa,sema tu watoto ndo wanatutiaga huruma tu,malipo duniani na icho kibamia chake atakoma..pumbavu zake ilo jibwa

 23. Anonymous

  January 19, 2013 at 1:07 pm

  tamwa ikitokea tatizo kama hili husikii wakisema ila kwenye siasa balaa sijui wakoje mambo ya msingia kama haya huwasikii ila yangekuwa ya chama ungewaona barabarani wamelala. mungu atakusaidia haki yako utaipata mama

 24. Anonymous

  January 19, 2013 at 1:10 pm

  hao ndio wanaume wetu akipata totozi wewe huna maana tena

  mungu yupo nawe utashinda tu ishallah

 25. paulina

  January 19, 2013 at 4:32 pm

  Hapa nimeona nguzo mama jinsi ilvyofanya kazi……..wanawake tukishirikiana tunaweza yani hapo bila wanawake wenzake kuingilia mama ingekula kwake.pole mama.

 26. damas ishengoma

  January 20, 2013 at 9:47 am

  wanaume wa cku hizi ndo walivyo uko alikokuwa analala kashapewa madawa.alafu hana aibu ya watoto na mama mkwe.na maaskari polisi wa cku hizi baada ya kulinda mali ya raia wanaalibu

 27. Anonymous

  January 21, 2013 at 12:40 pm

  dina yule dada katupiwa tena vitu nje leo hivi ninavyoandika mabaunsa wanatupa vitu nje

 28. Anonymous

  January 22, 2013 at 5:05 am

  MIMI KIDOGO COMMENTS ZA WADAU ZIMENICHANGANYA MAANA ZIMEEGEMEA UPANDE MMOJA TU WA MWANAMKE KWAMBA AMEONEWA. BINAFSI SIJUI UNDANI WA ISSUE YENYEWE LAKINI KAMA TUNGEPATA FURSA YA KUMSIKILIZA NA HUYO MWANAUME KWAMBA IMEKUWAJE HADI AKACHUKUA HAYO MAAMUZI MAGUMU NAMNA HIYO PENGINE HAPO TUNGEWEZA SASA KUWEKA KATIKA MIZANI NA HIVYO KUWEZA KUTOA FAIR COMMENTS. MFANO KWA MAELEZO YA DINA HAPO JUU NI KUWA WAKATI ZOEZI LINAFANYIKA NA MABOUNSA, KULIKUWA NA ULINZI WA POLISI AMBAO NAO WANADAI WALIPEWA BARUA NA MAHAKAMA KUSIMAMIA AMANI WAKATI ZOEZI HILO LINAFANYIKA. KWA MAANA NYINGINE NI KUWA HAPA KUNA MAMBO SISI WACHANGIAJI HATUYAJUI KUHUSU UPANDE WA PILI. NINGEOMBA DINA IKIWEZEKANA UFANYE MAHOJIANO NA HUYO MWANAUME AU NDUGU WA HUYO MWANAUME ILI TUWEZE KUJUA PART II YA HII SINEMA HALAFU HAPO JAPO SISI SIYO MAHAKAMA TUNAWEZA KUTOA COMMENTS ZISIZOMPENDELEA YEYOTE. HAYO NI MAONI YANGU NAOMBA WADAU MSINIELEWE VIBAYA NAJUA WENGI MMEPATWA NA JAZBA HASA BAADA YA KUONESHWA PICHA ZA TUKIO LENGO LANGU MIMI NI KUTAKA TU KUJUA UPANDE WA PILI KUNANI? MWANAMKE ALIKUWA MAKINI KATIKA KUTAMKA MANENO YAKE LAKINI NAONA HAPA WADAU MNASEMA MWANAUME KAPATA KIMADA MWINGINE. HAYA MMEYATOA WAPI? YEYE MWANAMKE KWA MAELEZO YA DINA KASEMA MWANAUME (MUMEWE) ALIKUWA HARUDI NYUMBANI NA HAKUSEMA AMEOA MWANAMKE MWINGINE KAMA BAADHI YA WADAU WALIVYOCHANGIA. KWELI AMA SII KWELI MIMI NA WEWE HATUJUI

 29. Anonymous

  January 24, 2013 at 4:41 am

  Dina hii sinema iliendeleaje? Sikubahatika kusikiliza Leo Tena naomba utupatie mwendelezo. Kuna mdau anasema huyo mdada katupiwa tena vitu nje imekuwaje? Kuna pia mdau ameulizia kupata story ya upande wa pili (yaani kwa mwanaume) anajiteteaje au ana maelezo gani? Ana nguvu gani kisheria inayomruhusu kufanya haya aliyoyafanya?

 30. Anonymous

  January 24, 2013 at 11:11 am

  Mungu atakusaidia mama na kukupa nguvu, vumilia mlilie Mungu akuongoze katika kila jambo unalotazamia kulitenda.

 31. Anonymous

  January 25, 2013 at 9:57 am

  Dunia ina mapito! Nimeumia sana kwa kweli.

 32. Anonymous

  January 30, 2013 at 12:12 pm

  NA mimi nimepata kaumbea ka upande wa pili. Ni hivi: Kuna jamaa anajulikana kwa jina la UDDY ambaye ndiye mmiliki halali wa hiyo nyumba tangu 1995. Huyu Selemani ambaye ni mume wa huyu dada alikuwa mpangaji wa hiyo nyumba na baada ya kuona anashindwa kulipa kodi alimwambia mkewe wahame lakini mkewe alikataa. Mume yeye alihama mwenyewe na kumwambia mkewe amfuate lakini hakufanya hivyo. Baada ya kuona mke hamfuati, Selemani aliamua kuja kuchukua watoto na kwenda kuishi nao. Mwenye nyumba Mr. UDDY aliendelea kufuatilia kodi yake bila mafanikio na ndipo ikabidi suala kufikishwa mahakamani kuwaondoa hawa wapangaji wasiotaka kulipa kodi. Hatimae january mwaka huu (2013) ikatolewa amri ya mahakama kuwaondoa kwa nguvu na ndicho kilichofanyika

  Kwa upande wa huyu bibie, yeye anadai haamini kwamba kweli hii nyumba siyo ya mumewe kwani anadai waliinunua mwanzoni mwa mwaka 2000 (sina hakika kama ana ushahidi) na kilichofanyika ni kuwa mumewe alitaka tu mtalaka wake aishi kwa tabu baada ya kuachana. Mwanamke amedai ataendelea kufuatilia haki yake sasa sijui kama ataipataje wasomaji habari ndio hiyo

 33. Anonymous

  March 25, 2013 at 4:02 pm

  Hakuna cha madawa wala nini, mijianaume mingine ikishatembea nje ya ndoa basi mkewe na watoto huwa ni choo usishangae anaweza kumtumia hata majambazi wakamuibia kila kitu na kubakwa yeye na wanae, hii ndio huitwa LAANA YA UZINZI

Leave a Reply