Uncategorized

MARAFIKI ZANGU WA FACEBOOK NA STATUS ZAO

By  | 
 
Aliandika…..Wiki
tatu zilizopita,niligundua store kuna panya,nikanunua
samaki,nikamuwekea kwenye kifuko cha wazi na dawa,asubuhi ya siku
iliyofata nikakuta samaki kama alivyo,nilivyorudi jioni nikakuta samaki
ameliwa ila kifuko kipo,nikajua kwisha habari yake,asubuhi nikakuta
kifuko kimechukuliwa pia…nikajua yupo bado,nikaweka mkate na dawa
nikaondoka,nimerudi jioni nikakuta umeliwa..asubuhi nikasafiri,leo
nimerudi napishana nae jikoni…AMEFANYA NYUMBA YAKE..bora angekuwa
anasaidia kulipa kodi sasa…niambieni dawa ya panya wadau..ananikera
mno mno..
 Baadhi ya comments zilizokuja kwenye status yake
 Don-Elvis Shoo Kaka
Its very SIMPLE, kama unaweza kamata Panya aliye HAI thats GOOD,
Ukishamkamata Mpake rangi NYEUPE mwili mzima mwache akauke then Mwachie
huko Ndani ya nyumba wengine wakimuona watauwa anakimbia mbaya na yeye
atajitahidi kuwafuata wenzake na wenzake watakuwa wanatimka baad ya siku
mbili nyu,ba yako itakuwa PANYA FREE!
Mghamba Jackson Monga unakosea kitu kimoja….usimuwekee dawa…muwekee sumu

Blanca Tengia Plz tafuta mtu au kanunue ile ya Kule SUA wanakodeal na panya!inaua balaa na haachi kula hatakama kashiba.

 Haiya tumpe mawazo ya SUMU gani ya panya ni kiboko!

14 Comments

 1. Anonymous

  January 8, 2013 at 7:23 am

  SIKIA KAKA PANYA UKISHAMUWEKEA DAWA HAKIKISHA HAPATI MAJI AKILA DAWA TU AKIPATA MAJI ANAPONA HAKIKISHA MAJI HAPATI NDO DAWA HIYO.

 2. Anonymous

  January 8, 2013 at 8:49 am

  nimecheka kweli kweli

  • Anonymous

   January 18, 2013 at 8:37 pm

   hunifikii mimi asee nacheka adi leo naposoma izi comments,looh watu wana raha sana smts

 3. Anonymous

  January 8, 2013 at 11:39 am

  mwambie aweke indocin kwenye vitu hao panya wanavyopenda kula. atamkuta amekauka km karatasi

  • Anonymous

   January 18, 2013 at 8:38 pm

   asee nafata huu ushauri natafuta hii dawa,nami pia nashida na panya

 4. Anonymous

  January 9, 2013 at 8:48 am

  halafu usimtegesheee sumu peupe weka sumu yako kwenye chakula halafu ficha hapo anakula haraka sana na kama kunasumu atakufa haraka au angalia asije akawa panya binadamu………?????!!!!!!!!!

 5. Hance Mbuya

  January 9, 2013 at 10:06 am

  panya muwekee mtego wa wavu,tafuta salfet zungushia kwa nje acha sehem ya kuingilia then weka samaki,au nyama choma.Kisha uweke kwa kuuwekea ki2 ili usichezecheze,muda mzuri ni jioni.Mafanikio utayaona.Na akiingia mmoja kama kuna mwingine usiharakishe kumtoa mwache mpaka mwingine aingie!youhead??

 6. Anonymous

  January 9, 2013 at 11:40 am

  Kazi rahisi, hii ni kwako na kwa wengine wote wenye tatizo kama hili, nunua pilipili manga (black pepper) ile ya unga unga, nyunyiza maeneo yote walioko panya, kwenye sakafu kote wanakokatiza, nakupa siku mbili tuh, utabakia mpangaji pekee halali kwenye hiyo nyumba. Zingatia umakini kama una watoto wadogo nyumbani kwako!

  Siri ya urembo ni nini? Panya miguu yake ina unyevunyevu, pilipili inanata miguuni, then inawasha, pili, panya ananusanusa siku zote, akinusa itampalia puani, simalizii uhondo, nakuacha uwaze pilipili ya unga ikikupalia puani inakuwaje! Hiyo ndiyo dawa rahisi na ya haraka, hawarudi tena hao!

  Na kwa faida ya wengine pia, kama una tatizo la sisimizi kuingia kwenye kopo lako la sukari, weka mbegu kadhaa za karafuu kwenye kopo lako la sukari, hawataingia tena kwenye hilo kopo kamwe!

  Thanks.
  Bitozi!

  • Anonymous

   January 18, 2013 at 8:41 pm

   haki ya Mungu wewe!mbona nimekupendaaa?sisimizi mie kwa sukari adi kero karafuu kesho tu nnazo

 7. Anonymous

  January 14, 2013 at 7:31 am

  Du nlikuwa cjui kumbe kuna dawa ya panya na sumu ya panya

 8. Anonymous

  January 15, 2013 at 8:40 am

  nunua zile dawa za vitambitambi inaua kabisa tena inawakausha

 9. Anonymous

  January 21, 2013 at 8:31 am

  Angalia ucje ukajitega mwenyewe na hz sum kuwa makin

 10. petronila massawe

  January 30, 2013 at 9:56 am

  ha ha ha ha ha ha….panya noma

 11. Anonymous

  February 18, 2014 at 9:17 pm

  panya nouma bhana

Leave a Reply