Uncategorized

PUMZIKA KWA AMANI SAJUKI,MAPENZI YA MUNGU YAMETIMIA!!!

By  | 

 Alipangalo mola mwanadamu hawezi kulipangua Sajuki amekwenda…..
amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili.

Alilazwa hapo kwa wiki mbili ambapo alikua
anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo
alipangiwa kurudi tena December 2012.

 Baada ya kurudi nchini hali yake ilikuwa nzuri tu na mwili ukaanza kurejea kama anavyoonekana kwenye picha hapo akiwa na Wastara mkewe.Pamoja na kuwa katika hali hii bado alikuwa ni mgojwa.
Mwezi wa kumi na moja 2012 Sajuki alifanya tour aliyoiita asante Tanzania kwa lengo la kuwashukuru watanzania walipomchangia.Lakini kilichokuwa nyuma ya pazia ni kwamba alikuwa akikusanya pesa ili arudi India kwa matibabu.Akiwa mkoani Arusha
katika 
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini  hivi karibuni alianguka.Na yeye mwenyewe kukiri kwa kusema
“Sijisikii vizuri, hali yangu ni mbaya.”
Baadae mwenyewe alisema kuwa pamoja na kuumwa,haikuwa rahisi kurudi katika vyombo vya habari tena kwa ajili ya kuomba Watanzania kumchangia kwa ajili ya fedha za matibabu kwa awamu nyingine. na muda wa kurudi ulikuwa umefika.
 Kwa takribani wiki mbili Sajuki alikuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.Na ilifikia hatua ya mheshimiwa raisi Jakaya Mrisho Kikwete kuamua kumsaidia kumpeleka India kwa matibabu.

Pamoja na msaada lakini bado kulikuwa na changamoto kwamba tatizo kubwa lililomzuia Sajuki
kurudi India ni pumzi ambapo walikua wanatafuta ndege yenye huduma ya gesi.

Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho
ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki
ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo
kumsafirisha mpaka India.

Sajuki alikua na tatizo kubwa la kupumua
wakati huu ambapo   upumuaji wake ulikua unabadilika
mara kwa mara.

 Pole sana Wastara ulijitahidi kadri ya uwezo wako kuhakikisha mumeo anapona.Ila yule aliyetuumba ndio ameamua na akipanga lake hakuwa wa kulipangua.Pole kwa familia,mashabiki na watanzania kwa ujumla.
Msiba upo nyumbani kwao Tabata bima na mazishi kufanyika keshokutwa katika makaburi ya kisutu.
Kwa mujibu wa baba yake mzazi,marehemu alizaliwa mwaka 1986 na amefariki akiwa na umri wa miaka 27.

Mungu ailaze roho ya marehemu Juma Kilowoko mahali pema peponi,Amina.  

24 Comments

 1. Anonymous

  January 2, 2013 at 12:26 pm

  Ameitwa akiwa bado mdogo jamani mie ata siamini kwani ni kati ya watu niliokuwa napenda apone Mungu amtie nguvu mke wake ndugu jamaa na marafiki tutakukumbuka

 2. Anonymous

  January 2, 2013 at 12:40 pm

  Pumzika kwa amani ndugu yetu,,,, nasi tupo njiani twaja. Mungu kakupenda zaidi,,"""Inalilah wainalah lajinuun"" AMIN!!!

 3. R.Ngaiza

  January 2, 2013 at 12:43 pm

  KWELI MUNGU AKIPANGA NA AMEPANGA, PUMZIKA SAAMA SAJUKI. TULIKUPENDA ILA MUNGU KAKUPENDA ZAIDI. IMENIUMA SANA. POLE SANA WASTARA MUNGU AKUPE NGUVU KWELI WEWE NI MWANAMKE WA SHOKA. MFANO WA KUIGWA. MUNGU AKUTAZAME NA MWANAO

 4. Anonymous

  January 2, 2013 at 1:59 pm

  ooo jaman polen sana familia ya sajuki…pia wastara mungu akupe moyo wa uvumilivu mama

 5. Anonymous

  January 2, 2013 at 2:12 pm

  Inna lillah waina illahy rajium,R.I.P Bro. Pole kwa wastara,ndugu, jamaa na marafiki.

 6. RUKY

  January 2, 2013 at 2:42 pm

  KIISLAAM TUNAAMBIWA MITIHANI NI IBADA SO MUNGU AMEKUPA MITIHANI MINGI SANA WASTARA WA KUKUPIMA IMANI YAKO NA KUKUKUMBUSHA KUWEZA KUMTAJA MOLA WAKO KILA MARA BILA KUMSHIRIKISHA INSHAALAH MOLA ATAKUPA WEPESI UWE NA NGUVU YA KUENDELEA KUMUOMBEA MUMEO AMPUMZIKE PEMA PEPONI…AMEEEN…

 7. MDAU

  January 2, 2013 at 3:34 pm

  R.I.P

 8. Anonymous

  January 2, 2013 at 4:26 pm

  so sad! RIP SAJUKI

 9. Anonymous

  January 2, 2013 at 6:07 pm

  R. I. P SAJUKI TULIKUPENDA SANA MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI. Wastara Mungu yu pamoja tumwomwombee kwa mungu apunzike kwa amani. Bwana ametwa jina lake lihimidiwe.

 10. EMMIE KAHERE

  January 2, 2013 at 10:31 pm

  Dina kesho alhamis ukifka tu kwenye leo tena weka mwimbo wa MBONI YANGU.,uwafikie wote waloguswa na msiba huu.,binafsi naguswa sana hasa nkikumbuka jinsi ww ulivyohangaika kuchangisha ili kupigania uhai wa sajuki.may GOD BLESS YOU DINA.

 11. sabrinah

  January 2, 2013 at 11:05 pm

  so sad, innalillahi waina ilahi rajuun

 12. Anonymous

  January 2, 2013 at 11:37 pm

  Inasikitisha sana lakini ukweli ni kuwa KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA. DUNIA HII NI UWANJA WA MPITO TU KWA VIUMBE VYOTE. Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya ndugu yetu Juma mahali pema peponi.Amin.

 13. Not Hater

  January 3, 2013 at 6:45 am

  Amin

 14. Anonymous

  January 3, 2013 at 9:18 am

  Pole sana Wastara Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu
  BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

 15. wa ukwejeh

  January 3, 2013 at 11:44 am

  Nashindwa kujieleza bt ol in ol,,Wastara pole ktk kpnd hk kigum

 16. Anonymous

  January 3, 2013 at 12:59 pm

  Pole wastara unaweza kufuru kwa mitihani inayofululiza kwako jikaze ila kumbka ukiona matatzo yanazdi ujue lipo jema ambalo mungu amekuandalia

 17. Anonymous

  January 3, 2013 at 1:18 pm

  Sajuki uliteseka sana na ugonjwa Mungu ameamua akupumzishe

 18. Anonymous

  January 3, 2013 at 2:30 pm

  Pole sana wastara'Mungu akupe nguvu na moyo wa imani'poleni sana familia,poleni bongo movies,pole sana Dinna unamchango wako mkubwa Mungu amlaze mahali pema peponi(mama caren)kimara

 19. Anonymous

  January 4, 2013 at 12:13 pm

  Pole sana Wastara, hakika Mungu ni mwema siku zote na kama yeye alivyosema ya kuwa ni mume wa wajane basi hakika hatokupungukia baada ya kifo cha mume wako. Pole sana, sipati picha ya maumivu unayopitia bali yeye aliye wa haki atakusimamia.

  on a different note; Dina u know how to write chronologically! hongera sana aisee

 20. Anonymous

  January 4, 2013 at 3:25 pm

  hakika namlilia wastara eee mungu mpe moyo wasubira huyu dada maumivu aliyokuwa nayo wewe ndo unaju

 21. Anonymous

  January 5, 2013 at 5:55 pm

  RIP SAJUKI, POLE SANA WASTARW, MUNGU AKUPE NGUVU

 22. Anonymous

  January 7, 2013 at 1:45 pm

  Msiba jaman unauma na hauvumiliki wala kuzoeleka nampa pole wastara namuomba mungu anipe wepesi kwenye hili niliwazalo niwe namkumbuka kumrehemu coz amekufa siku moja na anti yangu kasoro siku za kuzika nna maumivu sana moyoni mwaka nmeuanza vibaya ila hatuna jinsi kazi ya mungu haina makosa na hakuna atakae ishi milele wao wametutangulia tu.

 23. Anonymous

  January 8, 2013 at 2:53 am

  Wastara pole sana. Mungu akutie nguvu na akufute machozi. Kama Jina lako, Wastara hasumbuki, WA mbili havai moja. Si mpango WA Mungu kumsononesha mwanadamu. Hakika Mungu Yu pamoja nawe,ataendelea kukushika kwa mkono WA kuume WA haki yake. Pole dada,kikombe hicho ni kichungu mno

 24. Anonymous

  January 8, 2013 at 2:51 pm

  pumziko la amani na mwanga wa milele umwangazie.amin

Leave a Reply