Uncategorized

THE IMPOSSIBLE MOVIE

By  | 
Hii movie ni true story iliyowatokea familia moja ya waliosafiri kwenda Thailand kwenye vacation.Wakiwa huko na furaha na kila kitu ghafla kitu kikubwa na kibaya kikatokea.Ilikuwa tarehe 26 dec  2004  familia ikiwa kwenye swimming pool  nje ya hotel ndio janga la Tsunami likatokea.
Yaani ukiangalia filamu hii lazima ulie namna gani walipata shida.Watoto walibebwa na maji kivyao,mama kivyake na baba kivyake.Ghafla janga hili likawatengenisha.
Kwa bahati nzuri mama na mtoto wa kwanza Lucas wakakutana.Kasheshe baba yuko wapi?na watoto wengine wawili wako wapi?

Unaambiwa ukimaliza kuangalia hii filamu utahakikisha unawapa upendo uwapendao hasa familia yako.Watoto wako,mke wako,mume wako kubwa zaidi sio hadithi ni kweli imetokea.FAMILIA hiyo mwisho walionana baada ya kupoteana.Kitu special kuhusu hii hadithi ni kwamba katika Tsunami wapo waliopoteza ndugu,familia,mke,mume,watoto lakini wao ilikuwa bahati they survived.

 Itafute uione ni movie mpya lakini sijui kama imeshapatikana library.

Ukiangalia utagundua katika maisha hakuna HALI ya kudumu.Iwe ya raha ipo siku itabadilika ikiwa ya huzuni ipo siku itabadilika.Na pia matatizo yanavyoweza kukupa ujasiri na uvumilivu.Matatizo hayo hayo yakakuonyesha kuwa sio mara zote watu wakujali wewe tu inafika wakati lazima uwajali na wengine.Matatizo yanaweza kukufanya ujue kiasi gani unawapenda ndugu zako maana ipo siku utaamka utajikuta upo peke yako na wao hawapo.

9 Comments

 1. RUKY

  January 29, 2013 at 3:20 pm

  MMMH BONGO MKO FASTER SIKUHIZI…HUKU NIMEIYONA KABLA YA MWAKA MPYA NDIYO IMETOKA…NADHANI..

 2. Anonymous

  January 29, 2013 at 7:45 pm

  mambo da Dina movie hiyo natamani kuiona je wewe umeipata wapi pls nielekeze na mimi ningependa kuiona

 3. Anonymous

  January 30, 2013 at 2:21 am

  siku nyingi naona trailer tu kwenye tv kwamba inaoneshwa kwenye cinema wkt huu (huku uk)lkn sijatilia akilini sana ila leo nilipopita kwnye blog yko ulivoielezea imenivutia nimeamua niiangalie online kiukweli sikufanya makosa ni bonge moja la movie, naniukweli ulivosema ukiangalia utalia afu utaipenda familia yko, lucas is my hero kamsaidia sana mama yke na pale anamuita baba yke 'dady' wale wadogo zake wanamuona wanamuita 'lucas lucas' wanapiga mbio sana kwenda kukumbatiana na kaka yao nimelia sana afu kidogo baba nae anatokea aah lazima mafua yatoke, kiukweli film ni nzr and ahsante dinah.

 4. Anonymous

  January 30, 2013 at 10:55 am

  dina inapatikana wap hii movie

 5. Anonymous

  January 31, 2013 at 4:00 pm

  kweli dina inapatikana wap hapa bongo jmn its sound iko poa sana

 6. Anonymous

  February 3, 2013 at 2:42 pm

  Mi nimempenda Lucas,mtoto bongela kamanda.

 7. Anonymous

  February 4, 2013 at 9:28 am

 8. GRADUUU

  February 7, 2013 at 8:18 am

  https://www.youtube.com/watch?v=tGnjYsdVDwM then unadownload kutumia any downloader uliyo nayo kama real player

 9. ireen steven

  March 3, 2013 at 9:16 pm

  Ni movie nzur mno ndo nimeangalia leo nimelia sana inackitisha…kiukwel maisha ni duara pia.

Leave a Reply