Uncategorized

UPENDO WA MAMA SOKWE KWA MWANAE

By  | 
 Hapo kama hujipendi jaribu kumshika huyo mtoto wake.
 Mhhhh sijui ndio maana tuliambiwa binadamu wa zamani walikuwa nyani wakaanza kubadillika na kuwa watu katika lile somo letu la evolution!!!Maana kuna sokwe na nyani mpaka leo hawajabadilika kuwa watu.Sasa sijui yale mabadiliko yaliishia huko zamani???!!
 Unaambiwa mama sokwe ni mkali sana anapokuwa na mtoto mdogo anakuwa nae muda wote.Atamnyonyesha,atamsafisha na kuhakikisha yupo salama kwa kumbeba muda wote.

5 Comments

 1. Anonymous

  January 7, 2013 at 4:11 pm

  My dear dina mi nataka nikwambie kitu kimoja au nikushauri kitu ni hv hawa wasichana wa kazi mnawasaidia sana kuwatetea kwenye vyombo vya habari wasiteseke au wasiteswe lakini hamuwaambii wao wafanye kazi zao kwa bidii ili wathaminiwe mi nina msichana haamkii mjeuri ukimwambia kitu anasema anaenda wanawake live sasa mnapokua mnarusha mada redioni ongeleeni na hili pia maana naona inageuka kero baada ya ukombozi kwa samahani kwa kupost sehemu isiyo sahihi

  • Anonymous

   January 10, 2013 at 7:42 am

   Dada wasichana wa kazi ni pasua kichwa, mimi nimetimua wote, nilikuwa na mwizi balaa (huyu anakwenda na kurudi), mwingine anajisifu yeye anaamka saa moja hawezi kuamka alfajiri, mchafu, mharibifu wa vitu, mbadhilifu, mfujaji, na mbaya ya yote hafundishiki. Akaanza kufundisha tabia za kimalaya watoto wangu wadogo (7 yrs) namna ya kukata viuno kitandani, ilipofikia hapo tu nikatimua siku hiyo hiyo, sasa nina amani na nimejipanga na kazi zinaendelea. Hawafai (walio wengi).

 2. Anonymous

  January 8, 2013 at 12:26 pm

  Dada Dinna hizo picha za Sokwe zimenigusa sana, nimekaa nikatafakari kuwa Huyo ni mnyama tuu hana uelewa kama ss binadamu, lakini anaupendo mkubwa sana kwa mwanaye.Hivi ni mara ngapi tumesikia kwenye vyombo vya habari mtoto kaokotwa jalalani, kawekwa kwenye mfuko wa rambo n.k. ni ss binadamu tunafanya hivyo,na tunajidai tunamjua Mungu. Huyo Sokwe hata Mungu hamjui.Me nimeguswa sana kwani kuna kitu nimejifunza kutoka kwenye hizo picha.

 3. Anonymous

  January 11, 2013 at 7:28 am

  wewe mdau wa mwisho unasema sokwe hamjui mungu?wanyama wote wanamjua mungu ila sisi ndio tunawalazimisha kuwa hawamjui mungu maana wao mungu alivyowamba ndivyo wanavyofanya lakini sio sisi tunarohombaya,tunawivu,chuki,ubinafsi namengine lakini mnyama kadri mungu alivyomuumba ndivyo anavyoishi

 4. Anonymous

  January 21, 2013 at 8:38 am

  Da dina hawa ni wenzetu ila sema wao walinyimwa kauli mwenyewe c unaona????

Leave a Reply