Uncategorized

HUWA NAPENDA KUNYWA JUICE YA KAROTI MARA KWA MARA.

By  | 
Nimejikuta napenda sana juisi ya karoti tena jioni nikimaliza mazoezi lazima nipate glass moja hivi.Watu wengi hawaipendi wanasema sio tamu lakini inategemea imetengezwaje.Katika utengezwaaji ili uenjoy juice yako lazima iwe haina maji yaliyoongezwa wala sukari.Ni juice tuu ya karoti pekeee.
KWAKUNYWA JUICE YA KAROTI UTAPATA FAIDA ZIFUATAZO.
1.Karoti ina carotine ambayo hukupa uwingi wa vitamins A,B,na E
2.Kwa sababu ya uwingi wa madini juice ya karoti inasaidia sana afya ya macho katika kuona vizuri,uimara wa mifupa,meno na kucha.
3.Pia ngozi nyororo nayenye afya bila kusahau nywele.
4.Juisi ya karoti inasaidia kupunguza uwezokano wa kupata kansa ya ngozi na matiti.
5.Ukosefu wa vitamini A husababisha ngozi kukauka,kucha na nywele kuwa dhaifu sasa juisi ya karoti ina uwingi wa vitamin hivyo jusi hii ndio mpango mzima.
6.Kwa sababu ya uwingi huo wa vitamin A husaidia ini kufanya kazi yake ipasavyo.Na inasemekana ili ipatikane vitamin A ya kutosha kunywa juisi hii kila siku sio ukijisikia.
7.Haina cholestral
8.Madini kibao yanapatikana kwenye karoti  Calcium,Potassium,Copper,
Iron, Magnesium, Manganese, Phosphorous
9.Kwa mama anaenyonyesha karoti itamsaidia kupata maziwa yenye afya kwa mtoto.
Hizi ni baaadhi zipo kibao,kunywa jusi ya karoti kwa afya yako. 

20 Comments

 1. Anonymous

  February 26, 2013 at 10:10 am

  pia juisi ya karoti ni nzuri kwa watoto wanaotambaa, inaua minyoo yote tumboni, hakikisha unampatia mwanao kila asubuhi kabla ujampa chochote kama uji au maziwa.

 2. RUKY

  February 26, 2013 at 11:01 am

  Sasa utaisagaje bila kutia maji kidogo? mi huwa nakunywa kwa week mara 2 na huwa wakati mwingine naichanganya na embe ambalo halijaiva sana na tangawizi yote ni kutafuta ladha kweli c tamu ukinywa hivi hivi….

  • Anonymous

   March 6, 2013 at 11:38 am

   Kuna mashine maalumu ya kusagia caroti, na inatoa juice bila maji. ni nzuri ina ladha hata bila kuweka chochote. chagua tu crrot nzuri, ambazo hazijakaa siku nyingi. utapenda. mashine yake ni kama blenda ti
   u na inauzwa bei ya kawaida ya blenda. mimi nilinunua elfu sabini. na nilipata wazo hilo kwenye mtandao, nikitafuta dawa ya macho nilikuwa sioni vizuri na kichwa kinaniuma mara tu nikitoka kazini. nikajua ni madhara ya kutumia computa. lakini hivi sasa niko powa kabisa sbb ya carot Juice

 3. Anonymous

  February 26, 2013 at 12:07 pm

  wao dina thnx kwa kutuelimisha mpz keep it up maana wengine hatuji kitu blessed.

 4. Mama 2 (Mrs M)

  February 26, 2013 at 12:26 pm

  Mambo Dina! Mimi napenda sana Juice hiyo! na nina machine (Juicer) inayosaga vitu vigumu na kuchuja kabisa, isipokuwa ninasikia watu wakisema karoti mbichi zinaleta minyoooo, hebu nijuze kwa hilo mdogo wangu.

 5. Anonymous

  February 26, 2013 at 4:16 pm

  Asante dina nilikuwa sijui na ninanyonyesha ntaanza sasa kunywa mimi na bby wangu.

 6. Anonymous

  February 26, 2013 at 4:58 pm

  Mama 2 Mrs M, unatakiwa uzioshe na maji safi yaliyochemshwa yakapoa kiasi cha uvuguvugu ili kuuwa vijidudu au ukiweza tumia "salad wash" maalumu kwa kuoshe matunda na mbogamboga ziliwazo mbichi. Hutapata minyoo. Mi nikitengeneza juice yangu ya karoti naweka maji kdg ili isagike vizuri.

 7. Anonymous

  February 27, 2013 at 9:36 am

  Nilikuwa siipendi ,but not until u convinced me and bought me a glass!! it awesome sasa natafuta blender yake!

 8. Mama 2 (Mrs M)

  February 27, 2013 at 9:42 am

  Thanx Anonymous hapo juu, nashukuru kwa kunijuza hilo.

 9. Anonymous

  February 28, 2013 at 11:13 am

  NASIKIA PIA INAONGEZA NGUVU ZA KIUME KISHENZI!!!!

  • Anonymous

   March 4, 2013 at 9:17 am

   thibitisha

 10. Anonymous

  March 2, 2013 at 3:27 am

  Thankx?

 11. Anonymous

  March 4, 2013 at 8:14 am

  na ukitaka juice yako ya karoti iwe nzuri zaidi i grate na grater kikangulio cha karoti then uchuje kama tui la nazi huwa inakuwa nzuri zaidi

  • Anonymous

   March 6, 2013 at 11:29 am

   mmh we anony hapo mambo ya kuchuja si ndo uchafu wenyewe, embu nunua juicer , haiwezi kuzidi 65,000, changanya carroti na beetroot, yani hutaugua kabisaaa

 12. Anonymous

  March 8, 2013 at 9:13 am

  dina na wadau, nimeulizia blender hiyo kwenye baadhi ya maduka hawana. Yeyote yule mwenye kujua zinapouzwa, msaada pliz?

 13. Anonymous

  March 19, 2013 at 9:32 am

  ILI WEZE KUSAGA KWA ULAHISI ZICHEMSHE ZILAINIKE KISHA ZIACHE ZIPOE ALAFU UZISAGE UTAPATA MAJI KWA WINGI

 14. Anonymous

  March 20, 2013 at 9:06 am

  Mh! ukizichemsha virutubisho vitabakia kweli?

 15. Anonymous

  March 24, 2013 at 7:50 pm

  NASHUKURU DOGO MAANA HAYA MACHO YA KIZEE NOMA BILA KUYASTUA NA KAROTI ITAKUWA ISSUE

 16. Anonymous

  June 25, 2013 at 9:31 am

  nashukuru kwa elimu

 17. Anonymous

  April 7, 2014 at 3:20 pm

  blenda hizo zanzibar kibaooo

Leave a Reply