Uncategorized

JUMAPILI YANGU KATIKA PICHA!

By  | 

Jirani na nyumbani kwangu nyumba inayotazamana na kwangu anaishi huyu mtoto anaitwa Chriss.Kila nikirudi nyumbani au akiniona lazima aje nyumbani.Na kila siku lazima aje kututembelea utamsikia tu nje hodiiiii.Jana nimekaa tu nje akaja.kule nje kwa mbali mwenye tshirt ya blue ni mama yake na Chriss.
 Nilikuwa na kamera nikaa nampiga picha wenzie walipoona nampiga picha na wao wakawa wanataka.Pichani Chriss anawazuia wasiingie nikamwambia waache siunajua watoto na mambo yao.
Wakaja dada na sisi tupige picha tupige picha nikawaambia haya wekeni mapozi mpaka nikome mimi.
 Mapozi yakaanza

Yaani nilikuwa napiga picha huku nakufa mbavuu,kila baada ya picha wanakuja kuchungulia picha imetokaje.Nikawaahidi nitawasafishia picha zao niwape ni kumbukumbu nzuri kwao siku moja wakiwa wakubwa.Zoezi letu likaishia hapo maana nilikuwa ninatoka.
 Saa moja moja nikakutana na Fide kwa maongezi ya hapa na pale ya maisha na drinks kidogo.
 Fide ni rafiki yangu ambae amekuwa kama dada kwangu.Tulikutana mwaka 2003 nikiwa kwenye kituo cha daladala tunangoja usafiri.Tukaanza kupiga story mpaka tunapanda daladala nikakosa siti yeye akanipakata tukabadilishana namba za simu ndio hadi leo tumekuwa karibu kama ndugu sasa.
 Tukaa kaa baada ya maongezi kwenye saa nne nikarudi zangu nyumbani.
Nikafika hme sikuwa na usingizi nikakaa kuangalia movie 
 Nikaweka madea’s Big Happy Family
 Inamuhusu mama ambae amekuwa akisumbuliwa na kansa kwa muda mrefu na ameambiwa na dokta siku zake duniani zimebaki chache.Kutokana na mpanganyiko wa familia anajaribu kuandaa chakula cha usiku ili awaambie wanawe nini ameambiwa na dokta.
 Inaonekana katika malezi kuna mahali huyo mama alifeli hivyo inakuwa ngumu watoto kumsikiliza.Hivyo anaenda kumuomba Madea amsaidie kuwakusanya watoto wake kwa ajili ya siku hiyo maalum.
 Nilichoona kwenye movie hii kama baba na mama hamuheshimiani na watoto wanakuwa hawana adabu wala heshima kwenu.
 Unapata taabu sana kuishi na mkeo kumbe ana matatizo ya utoto yanam-hunt mpaka leo.Unaweza kuoa mke kumbe anasiri kubwa hajakueleza kumbe aliwahi kuwa na mtoto yupo analelewa na mama yake wewe kakuficha.
 Kuna familia zina siri kubwa na ni katika sehemu ya kuhakikisha mambo hayaharibiki yanakwenda sawa.Ila baadae yanabumburuka unayemuita mama kumbe ni bibi yako na unayemuita dada ndio mama yako.Ni movie ya muda itafute kama hujaiona mie naiangalia kwa mara ya nne.
 Usingizi nao ukapiga hodi mida ya saa sita nikaenda kulala.

28 Comments

 1. emma kahere

  February 11, 2013 at 4:48 pm

  Nimeiona hii movie dina yan huyu mama alikuwa bongee,nliishiwa mbavu pale alipokuwa anamfokea muuza min market akawasha gar akaingia nayo had ndan.super market yote akaharibu harbu v2.,

 2. RUKY

  February 11, 2013 at 5:20 pm

  WAWOOO DINA VERY CUTE ENJOY…NAPENDA KWELI NYWELE ZINAVYO KAA NIAMBIE BC UMEFANYA NINI?

 3. ULSURA

  February 11, 2013 at 6:13 pm

  Chriss hatareeee nayule dogo asiye nashati balaa!! Hayo mapoz ss mh utoto raha sn!!no mawazo yani full burudani!! Mm penda sn ww inaonekana unapenda watoto!

 4. Anonymous

  February 11, 2013 at 8:05 pm

  Huh!! upweke ulio nao hapo unatia huruma du! afadhali usingetuonyesha hiyo picha kama vile unawaza japo unaangalia hiyo movie. Ila unapendeza Dina ninachopenda ni hizo nywele zilivyo unavutia sana.

 5. Anonymous

  February 12, 2013 at 7:00 am

  Dina napenda nyumba yako ni safi sana, na una mpangilio mzuri, nakuombea kwa Mungu upate mume mwema atakayekupenda kwa dhati,

  love you mom

  gee

 6. Anonymous

  February 12, 2013 at 7:20 am

  i love ur lyf…sweet home

 7. atug

  February 12, 2013 at 8:39 am

  off the topic….dina nimependa sn mapazia yako jamen

 8. Anonymous

  February 12, 2013 at 8:57 am

  Nilipomuona Madea nilijua ni ile movie ya Madea goes to jail itafute nayo ni nzuri sana,Teyler Perry ana movie nzuri sana kama Good deeds,Madea goes to jail

 9. Anonymous

  February 12, 2013 at 9:30 am

  Mambo Dina! Nimepanda halo kashort narration ka wewe na fide mlivyokutana!! Yaani jamani true friendship just happens hakuna kuombana ushoga!me like!!!

 10. Anonymous

  February 12, 2013 at 11:26 am

  hizi move dina unapata wapi sisi wa mikoani tabu tupu ungepataga soft copy hata ukaturushia napenda sana mie move hizo wali wapi huku hakuna

 11. Anonymous

  February 12, 2013 at 12:26 pm

  Jamani dina ujatuambia tukuulize tena maswali mwaka huu kuhusu wewe je? mmerudia na Reuben ndege niliwaona wote fiesta mnapendezaga sana.

 12. Anonymous

  February 12, 2013 at 1:48 pm

  Anayekupiga picha nyumbani saa 6 usiku nae muonyeshe tumjue

  • Anonymous

   September 4, 2013 at 8:59 am

   Hapo chacha

 13. Anonymous

  February 12, 2013 at 8:00 pm

  dina natamani kukutanaga na wewe,one day yes..

 14. Anonymous

  February 13, 2013 at 4:58 am

  dina nakupenda sana…napenda mpangilio wa nyumba yako,na wewe mwenyewe…uko simple…mungu akubariki

 15. Anonymous

  February 13, 2013 at 5:21 am

  Madea ni kiboko. dina napenda maisha yako uko huru. co sie tuliokimbilia kuolewa tunazeeka kabla ya muda. Me pende ww mamii kwako kuko simple

 16. Anonymous

  February 13, 2013 at 6:59 am

  yaani da Dina mi pendaga sna wewe zaid ya sana, tangu 2006, i wish cku moja nitakuja hukohuko Clouds yaan nawpenda, pia mkiwa na gea na zama yaan dddaaah. ishi vyema na majiran ndio mjpango mzima ndugu.

 17. Eliud Samwel

  February 13, 2013 at 8:07 am

  ngoja nami niitafute hyo

 18. Anonymous

  February 13, 2013 at 10:11 am

  NIMEIPENDA SEBULE YAKO MAMY NTAKUITA KWA KIOTA CHANGU KIKIWA TAYARI UNIWEKEE MAMBO VIZURI, WENGINE HATUJUI KUPAMBA HOUSE HAHAHAHAHAHAHHAHAHAH

 19. Bella

  February 13, 2013 at 10:25 am

  Dina jamani tuambie wadau wako kama mmerudiana na Reuben Ndege, nilikuwa naipenda sana couple yenu. Reuben kama utaisoma hii comment naomba ufanye kweli basi, nini tatizo mbona Dina yupo poa sana.

 20. Anonymous

  February 13, 2013 at 1:03 pm

  narudia anaekupiga picha usiku wa manane nani?

 21. Mama 2 (Mrs M)

  February 13, 2013 at 1:04 pm

  Mi hoiii!! na hizo pozi za watoto! Vizuri sana Dina, unaonyesha unapenda sana watoto ndo maana wanakufuata. Watoto ni kipimo kizuri sana cha kujua mtu mzuri au mbaya! hata nyumbani, ukiwa na H/Girl ukiwaona watoto wanapenda kucheza nae basi ujue ni mzuri kwa watoto, lkn kama ni mbaya kwa watoto, wenyewe watakwambia dada hatumpendi. Mungu akubariki sana Dina uje kuzaa watoto mapacha!!!

 22. Anonymous

  February 14, 2013 at 6:23 am

  I lyke tyla perrys movies.its a gud 1

 23. Anonymous

  February 19, 2013 at 6:56 am

  You are doing very fine Dina in various directions. Keep the fire burning and entrust mostly everything in God's blessings. Wewe ni kioo cha jamii, unabeba wajibu mkubwa na mpaka sasa unajitahidi. May God Bless You Dear.

 24. Anonymous

  February 19, 2013 at 8:43 am

  Dina nimegundua watoto sana tu! nawapenda sana wtoto wa kimo hicho malaika wa Mungu they are very innocent havijui nini kinaendelea in life! keep it up! tatizo lako hujibu msg kwa nini? mbona tunakuwa kama tunajikomba daa! soma blogs za nje ya nchi! au Blog ya Mange

 25. Anonymous

  May 16, 2013 at 3:08 pm

  What a cute home..so lovly jaman! U r cmpo n nice as well..I lyk u mom.

 26. Anonymous

  June 19, 2013 at 3:08 pm

  nyumba mzur

 27. Anonymous

  October 30, 2013 at 8:45 am

  Kwako kuzuri,we pia wapendeza,natamani kuja!

Leave a Reply