Uncategorized

LEO NDIO NIMEJUA BAMIA KWA KIINGEREZA INAITWA ”LADIES FINGER”

By  | 
Nilijua inaitwa okra lakini kumbe marekani ndio wanaita hivyo ila kwa kiingereza Ladies finger.
Kwa nini ziliitwa ladies finger?inasemekana ni kwasababu ya umbo lake lilivyo kama vidole vywa mwanamke.
Bamia hukatwa na kupikwa kwa mapishi tofauti tofauti
Ukaipika kwa urefu kwa maana ya kukata kikonyo na ncha yakekisha kuiunga na nazi.
Hizi zimewekwa tayari kwa kuokwa.Zimepasuliwa katikati halafu kwa ndani ukawekwa mchanganyiko wa vitunguu maji,jeera,coriender,pilipili ya unga,chumvi,mafuta ya kula,tangawizi na nazi vikachanganywa na kutiwa humo.Hii ni recipe ya kihindi ndio huwa wantengeneza hivi.
Huu sio mlenda bali zimekatwa ndogo ndogo zikaungwa vizuri kama zinavyoonekana…njaa inaanza kuniuma sasa maana ninavyopenda bamia.
Mlenda pale unahusika…..ukichanganya na majani ya maboga,nyanya chungu saafi unapika ladies finger zako.
India wanakula sana bamia….hii ni salad ambayo imetengenezwa baada ya kuziosha vizuri ladies finger zako.Unakata kikonyo unaziweka kwenye sufuria na maji kidogo halafu unazichemsha kwa dk 3 hvi ila zibaki kijani kama zilivyo.Unakatakata nyanya vidogo vidogo,vitunguu,pilipili,unatia chumvi,limao kama unavyotengeneza kachumbari.Baada ya hapo unakata bamia kama zinavyoonekana unatia hiyo salad yako tayari kuliwa.
Faida ya kula Ladies finger bamia
1.Inasemekana ni chakula kizuri kwa watu wenye msongo wa mawazo,wanaojisikia weak n.k
2.Ni chakula kizuri kwa wanaotaka kupunguza mwili.
3.Mbegu za bamia zina protine nyingi na mafuta
4.Inasaidia mmeng’enyo wa chakula na kupata choo vizuri
5.Zina vitamin A na C
6.Madini ya potassium,calcium na magnesium
Kula bamia zako  wala usizichukulie poa kisa zinateleza,ziko bomba kiafya.

29 Comments

 1. Mama 2 (Mrs M)

  February 5, 2013 at 12:49 pm

  Umenitamanishaje Dina!!! Hilo bamia kwa samaki wakavu ukaunga na nazi weeee ni balaa, hata mlenda pia kwa ugali uko poa saaaana!! Asante kwa kunijulisha bamia kwa kiingeredha, hata mimi nilikuwa sijui kidhungu chake.

 2. Anonymous

  February 5, 2013 at 3:26 pm

  Ndiyo Dina waingereza wanaita ladies finger!

 3. emma kahere

  February 5, 2013 at 3:50 pm

  Bamia bwana huwa ni tam mnoo.,ukila na ugali mmh chakula kinakuwa kitamujee

 4. Anonymous

  February 5, 2013 at 5:10 pm

  Huo mlenda unavutia sana upate sembe yako nyeupe alafu sasa usonge na ugaliwako laini basi ukifika mdomoni unateleza tuuu hadiraha

 5. Anonymous

  February 5, 2013 at 5:26 pm

  Wawooo kumbe ndo zinaitwa, nazipenda even uchanganye na nyama, dagaa ni poa tu kwa ugali

 6. Anonymous

  February 6, 2013 at 5:59 am

  Hii kitu na dada yake mlenda vimenishinda kabisa……

 7. Anonymous

  February 6, 2013 at 6:37 am

  bamia zinasaidia pia huongeza ute katikati ya maungio ya mifupa, pia zina madini mengi sana ya zinc ambayo yanasaidia uongezekaji wa damu

 8. mama Glory

  February 6, 2013 at 10:38 am

  kwa mama mjamzito bamia ukipika kama mlenda inasaidia kuleta uterezi kwenye njia ya uzazi wakati wa kijifungua, mama mjamzito hakikisha kuanzia umri wa mimba miezi saba hakikisha mlenda inakuwa chakula chako kikubwa nakuhakikishia siku ya kujifungua mtoto atateleza kama vile mlenda unavyoteleza mdomoni, mimi nimezaa nanina watoto wawili kwa watoto wangu wote nimeona faida ya mlenda, hata manesi walikuwa wanashangaa jinsi nilivyokuwa najifungua kwa urahisi, so jaribu leo uone maajabu ya mlenda kwa mjamzito.

 9. Anonymous

  February 6, 2013 at 12:09 pm

  hata watu wa ulcers inasaidia sana bamia,,,

 10. Anonymous

  February 6, 2013 at 4:01 pm

  Da! Jamani wadau mmenitamanisha sana. Yani bamia ukiweka na nyanya chungu ukaange na dagaa zako ugali unashuka tu. Au upike mlenda halafu kuwe na nyama roast na pili pili mbuzi na ugali laini. Mwee utakula huku umewasha feni hadi spidi ya mwisho! Then ushushie na SERENGETI BARIIIDI! Asante mdau kwa elimu ya kula mlenda miezi saba kabla ya kujifungu.

 11. Anonymous

  February 6, 2013 at 4:01 pm

  Da! Jamani wadau mmenitamanisha sana. Yani bamia ukiweka na nyanya chungu ukaange na dagaa zako ugali unashuka tu. Au upike mlenda halafu kuwe na nyama roast na pili pili mbuzi na ugali laini. Mwee utakula huku umewasha feni hadi spidi ya mwisho! Then ushushie na SERENGETI BARIIIDI! Asante mdau kwa elimu ya kula mlenda miezi saba kabla ya kujifungu.

 12. Anonymous

  February 6, 2013 at 4:01 pm

  Da! Jamani wadau mmenitamanisha sana. Yani bamia ukiweka na nyanya chungu ukaange na dagaa zako ugali unashuka tu. Au upike mlenda halafu kuwe na nyama roast na pili pili mbuzi na ugali laini. Mwee utakula huku umewasha feni hadi spidi ya mwisho! Then ushushie na SERENGETI BARIIIDI! Asante mdau kwa elimu ya kula mlenda miezi saba kabla ya kujifungu.

 13. The Lot

  February 6, 2013 at 9:08 pm

  Dada yangu umejuaje maana mi hazipiti siku mbili lazima nile bamia na hii ni kwa sababu sisi kwetu tabora unyamwezini tunakula sana hii kitu na nyanya chungu so am addicted.

 14. Anonymous

  February 7, 2013 at 5:08 am

  Asante kwa kuelimisha jamii kuhusu jina la bamia ila masahihisho kidogo sio LADIES FINGER bali ni LADY'S FINGER

  • Anonymous

   February 11, 2013 at 8:39 am

   Okra ni jina pia la bamia kwa kiingereza.

 15. Kary

  February 7, 2013 at 5:23 am

  Na mm napenda sana,.imenivutia,.ila mm huchemsha tu na kuweka chumvi kidogo na kula hivyohivyo bila hata ugali,.vilevile napenda juice ya bamia,unazisaga vizuri zikiwa mbichi kisha unakunywa bila kuweka chochote,.mim nimeshazoea na ninaona kawaida kabisa,.karibun wote tuufurahie mlo huu jaman,.
  Hilo swala alilosema mama glory ni kwel kabisa mama mmjamzito ni muhim ale bamia ili kurahisisha wakat wa kujifungua,.

 16. Anonymous

  February 7, 2013 at 10:36 am

  Mdau juice ya bamia. Mi napata tabu naona ngumu kumeza.

 17. RUKY

  February 7, 2013 at 11:04 am

  DAAA KUMBE INAMAMBO MENGI HIVI…MIMI C MPENZI KIIVYO LAKINI KWAHIZI FAIDA NTAJITAHIDI SASA.. ISIPITE WEEK..

 18. janeth

  February 7, 2013 at 11:59 am

  yaan me nalipenda zaidi likipikwa na nazi tena nipike mwenyewe thanx kwa faida

 19. Anonymous

  February 7, 2013 at 3:25 pm

  Dina tuwekee na aina nyingine ya mboga za matunda kama biringanya. Mi nazipenda ila kuzipika bado sijazijulia vizuri.

 20. Anonymous

  February 7, 2013 at 3:26 pm

  dah minalipenda week mara tatu lazima nile kumbe zinafaida hivyo sasa ntaongeza rate

 21. Anonymous

  February 8, 2013 at 12:03 pm

  Thx Dina! Mie jina(ladies finger) nilifundishwa na mwanangu tena alikuwa nursery wakati huo,so najifunza vitu vingi kutoka kwa wanangu through shule zao hizi za KIDHUUNGU!!! Wanatusaidia kwa kweli coz sio kila kitu mtu unajua.

 22. Anonymous

  February 8, 2013 at 12:28 pm

  Duh nimepata faida nyingi za bamia barikiwa sana dina na wote mliotupatia faida hususani aliyetuambia kwamba inamrahisishia mama mjamzito mtoto kutoka haraka, niliwahi kusikia kwamba mwanamke akila bamia na nyanya chungu maji maji ya uke yanaongezeka mwanaume akimwingilia inakuwa kama bwawa ni kweli wadau?

 23. Anonymous

  February 9, 2013 at 6:16 pm

  Mdau mi najua nyanya chungu ndiyo zinasaidia kuchochea glands zinazotoa ute wa kulainisha uke hasa kwa wale wenye uke mkavu zinasaidia sana.

 24. Anonymous

  February 9, 2013 at 6:16 pm

  Mdau mi najua nyanya chungu ndiyo zinasaidia kuchochea glands zinazotoa ute wa kulainisha uke hasa kwa wale wenye uke mkavu zinasaidia sana.

 25. Anonymous

  February 9, 2013 at 6:16 pm

  Mdau mi najua nyanya chungu ndiyo zinasaidia kuchochea glands zinazotoa ute wa kulainisha uke hasa kwa wale wenye uke mkavu zinasaidia sana.

 26. Anonymous

  February 11, 2013 at 12:36 am

  ahsante dada kwa kutujuza

 27. Anonymous

  March 8, 2013 at 11:20 am

  Ni nzuri sana hasa kwa wale wenye vidonda vya tumbo unazichemsha tu bila kutia chumvi wala mafuta then unakunywa ule mchuzi wake hutasikia kabisa maumivu ya tumbo kwa wale wenye vidonda!

 28. victoria buzare

  June 1, 2016 at 9:55 am

  Ukizikatakata kwa ufupi kama wa inchi 2 hivi au 3 ukaziunga na viungo alafu ukaweka nazi au karanga kwa mbali alafua upate ugali wa dona na kamuogo kiasi auachi kula.

Leave a Reply