Uncategorized

MAAKULI KATIKA KIJIWE CHA RODIZIO BRAZILIAN GRILL

By  | 
 Dar es salaaam sasa hivi maeneo ya kula yapo ya kila namna ukitaka kula vyakula vya nchi zingine duniani ushindwe wewe kwa kweli.Hapa ni Rodizio Brazzilian grill  Mikocheni.
 Nilipenda tu namna salad na matunda walivyoyapanga na kuandaa kwa namna ya kukufanya upate hamu ya kula.

 Salaad na matunda tu hapa

 Hapa ndio utaangalia unataka kula nini wali mweupe,chips,ndizi za kukaanga,na mchuzi wa samaki,nyama,kuku n.k

 Au utabeba salad na matunda na ungoje mzunguko wa nyama,kuku,samaki,nyama mpaka ya mamba ipo
 Inshort ni nyama hizo nilizotaja za kugrill zinapita hapo unakula mpaka useme basiiiiiii ndio wanakuwa hawaji.Mapaja ya kuku hayo unayoyaona.
Siku hiyo nilionja mpaka nyama ya mamba ipo kama samaki kwa harufu mpaka ladha.
Hapo zinapita soseji za kuku,ng’ombe,yaaaani kila ukijuacho na sio lazima kila kinachokuja ule unasema tu hiki ntakula na mniwekee kiasi hiki usichotaka kiache kipite.

 Linakuja nanasi la kuchoma mwishoni limewekwa asali na mdalasini wanakwambia kazi yake ni kusaidia digestion ya chakula tumboni.

29 Comments

 1. Anonymous

  February 15, 2013 at 1:22 pm

  Dina kwanza umependeza,pili mi nina rafika yangu ankaa maeneno hayo,na nikiendaga huko hua naishia kuangalia tu hapo,kumbe kuna chakula kizuri hivo,je ni sh,ngapi ili nami siku nijipinde nikajipe raha jamani

  • dinamariesblog

   February 19, 2013 at 10:55 am

   Ni Tsh 45,000 tu unakula utakachotaka wewe mpaka utakapotosheka ila haufungashi cha kupeleka nyumbani…

 2. ULSURA

  February 15, 2013 at 2:14 pm

  We kula kula tu,hadi nyama ya mamba umekula!?!?!? Mhh lilivyo baya kwa sura najingoz lakeee aaaaah mi no km ni ushamba bora nionekane hivyo jamani mi siliiiii!!!!

 3. Anonymous

  February 15, 2013 at 2:25 pm

  nlishaenda hicho kijiwe pia, nyama ya mamba sikula bora nionekane mshamba na hlo nanasi wanaweka viungo mpaka linaboa too much sugar!

 4. emma kahere

  February 15, 2013 at 3:05 pm

  I like your pochi,ina colour nzuri.naona ume match na ua top dress.,u look nyc my rolal modal

 5. Anonymous

  February 15, 2013 at 4:36 pm

  ungesema na bei mbona mwisho wa mwezi hapo

 6. batuli

  February 15, 2013 at 6:30 pm

  Dina umependeza sana ulivyopungua jamani.

 7. Anonymous

  February 16, 2013 at 6:51 am

  kiukweli hapa umeonekana kama fododido sijui ni hiyo blause uliovaaa mmmh

 8. Anonymous

  February 16, 2013 at 6:52 am

  kweli hasa hiyo picha ya kwanza.

 9. Anonymous

  February 16, 2013 at 1:59 pm

  I will appreciate if you will let me know exactly where this place is. Can i have their number? I real want to test mamba!

 10. Anonymous

  February 16, 2013 at 3:07 pm

  Naomba kupata direction and cost pliz nawajua hao toka nairob kumbe wametinga bongo thats nyc dinna yolo mdada…!

  • dinamariesblog

   February 19, 2013 at 11:07 am

   Ni mikocheni kwa nyerere utaona mabango yanayokuelekeza kwenda huko karibu na monas pale kuna bango na wamejitahidi kuyaweka ili usipotee utayafata ukiangalia mishale mpaka unafika.Ni Tsh 45,000 kwa mtu mmoja unakula utakachoweza mpaka useme basiiiiii!!!

 11. Anonymous

  February 16, 2013 at 3:47 pm

  Looking good:)
  Duh nyama ya mamba nisingeweza,ningetapika hadi bac.

 12. MOJAONE

  February 17, 2013 at 6:05 am

  Mambo kama haya itabidi kwa sasa tuishi ili tule tu.

 13. REHEMA

  February 17, 2013 at 9:26 am

  UZURI NI MATUNDA KWA WINGI SO HATA KUNENEPA SIO RAHISI, NA UZURI UNULA MARA CHACHE, KUZURI HUKO

  • dinamariesblog

   February 19, 2013 at 10:57 am

   kwa kweli ni wewe kuchagua sio kila kitu uparamie…na ukitaka kuharibu siku hiyo pia ruksa ahhahaah

 14. Anonymous

  February 17, 2013 at 11:26 pm

  Dina me nimependa sana style ya nywele zako! nimechoka kuvaa mawigi na kushonea mawiving, unaweza kunambia unazifanyaje nami niige?

  • dinamariesblog

   February 19, 2013 at 10:59 am

   nikitulia ntawawekea kwa blog mzione ninavyotengeza…kwa picha

 15. Mama 2 (Mrs M)

  February 18, 2013 at 5:30 am

  Haya ngoja nami niende siku nikajionee!

 16. Anonymous

  February 18, 2013 at 6:09 am

  nanasi la kuchoma hilo kali/// mimi ningefakamia nyama tu…kitimoto vip kipo?

 17. Saleh Demwa

  February 18, 2013 at 7:31 pm

  Ahsante sana Binti wa Marios,ila shilingi ngapi?nisije ingia kichwa kichwa hapo,kuumbuka nataka mie!nambie tafadhali

 18. Saleh Demwa

  February 18, 2013 at 7:34 pm

  Ahsante sana Binti wa Marios,ila shilingi ngapi?nisije ingia kichwa kichwa hapo,kuumbuka nataka mie!nambie tafadhali

  • dinamariesblog

   February 19, 2013 at 10:54 am

   Kwa mtu mmoja ni Tsh 45,000 unakula kila kitu mpaka uchoke wewe…

 19. Anonymous

  February 19, 2013 at 11:08 am

  top ni too loose my dear,najua ndo style yake but hiyo imekuvaa. otherwise umepungua nakupa hongera zako Dina

 20. hellen mdimi.

  February 21, 2013 at 3:41 pm

  naitwa hellen, nakupenda sana dina natamani ungekua dada yangu i like you so much my sister naomba nipe nafasi niwe mdogo wako japo cjawahi kukuona nakusikia na kukuona katika picha natamani nikuone uso kwa uso plz my sis. nikutanishe nawe dia coz i love you so much my sister. napatikana mabibo makuburi namba 0655811330, 0757811330 na 0684811330.sitaamini kwa furaha nitakayo kua nayo siku nikikuona.

 21. Anonymous

  February 24, 2013 at 5:01 pm

  Naona umekuwa mwanachama mzuri wa chadema. BIG UP DINA

Leave a Reply