Uncategorized

NI KWELI UNAWAPENDA WATOTO WAKO WOTE KWA USAWA?

By  | 
Hii ni kwa wazazi wenye watoto kuanzia wawili na kuendelea.Kila mzazi ukimuuliza kama anawapenda watoto wake atakujibu ndio tena sio kidogo anawapenda sana ndio maisha yake.
Ni kweli anawapenda sana watoto wake lakini sio upendo unaolingana kuna mmoja anapendwa zaidi ya wote.Kuna mmoja ndio kipenzi chako zaidi ya wengine huu ni utafiti uliofanywa baada ya wazazi kuulizwa na kuambiwa wawe wakweli na kubainisha hilo.
Wadau mnasemaje mnahisi hili linaukweli?je wewe una mtoto kipenzi kuliko wengine japo wote unawapenda?wakati ukikuwa katika familia yenu umeliona hili kwamba kuna mmoja alikuwa kipenzi cha mama au baba??

27 Comments

 1. Anonymous

  February 21, 2013 at 3:47 pm

  Hi Dina

  Kweli yapo mie baba yangu ananipenda kuliko wenzangu na tupo sita nisipompigia lazima alalamike vipi mama yangu mbona kimya na alinizoesha toka nipo mdogo mpaka kutoka nilikuwa natoka nae na nikirud shule kama sijamuona kitu cha kwanza kumuuliza mama leo baba anarud saa ngapi na yeye akirud ilikuwa lazima aulize mwanangu sijamuona yupo wapi?So mpaka sasa nimeolewa dina huwez amini maudhi nikikosana na Mr.lazima nimwambie ananipa ushauri siku zinaenda mpaka mume wangu ananiambia baba yako anakudekeza sana kila kitu anakusikiliza.So kweli wazazi wanatofautiana katika kupenda watoto wao

 2. Anonymous

  February 21, 2013 at 7:26 pm

  kwa maoni yngu wanapokuwa wadogo i mean kuanzia miaka kumi kushuka chini unawapa upendo unaofanana ila unapay much care kwa mdogo kuliko wote,mm ni baba wa watt wa 3,wa kwanza ana miaka 9,wa pil 4 na watatu ana mwaka mmoja na nusu,kilichopo nawapenda wote ila much care nakuwa nayo kwa yule mdogo kuliko wote,cos stil hajui chochote,nachoamini mapenzi ya baba yanalalia kwa mtt mmoja kwa sababu tofauti mfano wanapokuwa wakubwa kila mmoja ana tabia zake,unakuta mmoja mjeuri tu,hana adabu kwa wakubwa,hapend shule,aambiliki na unapata kesi za kila aina kuhusu yeye automatically utamtetea mwisho wa cku utamchunguza na kugundua mshenzi tu kibinadamu mapenzi juu yake yatapungua na unakuta mwingine anapenda shule,ana adabu zake,ana muheshimu kila mtu,anafanya kazi za nyumbani i mean ni verse versa wa mwanzo automatically utampenda na kuzidisha upendo juu yake,ndio maana saa ntingine utakuwa una mwambia mwenzie hebu ongea na kaka yako,haina maana amekushinda malezi but stimes ni mambo ya mwenyezi mungu tu,mfano sisi tupo wanane am the first born baba alikuwa ananipenda sana kiasi kwamba wenzangu wakitaka kuomba kitu lazima waniambie ongea na dingi cos anakusikiliza ww,nillimuwin dingo cos nilikuwa napenda shule na nafaulu hakuna nachomwambia kinakwama he have 2 do,all in all watt wote unawapa credit zilizo sawa tu ila kuna mwingine anazipoteza kadri anavyokuwa,hayo ni maoni yangu tu.

 3. Anonymous

  February 21, 2013 at 9:02 pm

  Dina, ni kweli kabisa! Ingawa ni ngumu kukubali unapoulizwa,bt ukweli ndo huo,mimi ni mama wa watoto 3! najaribu sana kadri ya uwezo wangu kuwaonyesha upendo sawa, bt nafsi bado inanisuta, kuna kaupendo kamezidi kwa first born wangu.Familia yetu ni ya watoto 7! mimi nilikuwa kipenzi sana wa baba! mama mpaka kesho anampenda sana last born wetu! so hivyo ni vitu vipo.

 4. Anonymous

  February 22, 2013 at 10:31 am

  Dina mimi ni mama wa watoto watatu (3), ndugu zangu huwa wananiambia nampenda sana mtoto wangu wa kwanza kuliko hawa wengine (ni wa kiume). Ingawa mimi mwenyewe naona upendo wangu uko sawa kwa wote only wanatabia tofauti huyu wa kwanza ananijali na huwa hata nikichelewa kurudi nyumbani anakuwa wa kwanza kunipigia simu kumbuka ndo kwanza ana miaka 9. Wa pili hana time na mimi yeye ni baba yake tu na ni wa kike. Watatu bado mdogo less than a year ingawa nduguze wanadai nampenda sana kuliko wao.

  Kwa upande wa familia yetu du dada yetu wa kwanza kuzaliwa anapendwa sana na baba na mama. sisi wengine hatu ufanye nini uzito wa kuappreciate unakuwa mkubwa kwa dada hata kama katoa sh.10 wewe umetoa 100 yeye ataonekana katoa kikubwa.

  Mada nzuri kwa kweli nimekumbuka mbaali….

  Mama Watatu

 5. Anonymous

  February 22, 2013 at 11:37 am

  Ni kweli kabisa,mie nakumbuka, Ndugu zangu walikuwa wakilalamika kuwa mama anampenda kaka yetu zaidi

 6. Anonymous

  February 22, 2013 at 11:41 am

  Hiyo ipo lkn tunaposhindwa kujizui kuficha na kuionyesha wazi wazi inaleta madhara kwa watoto wenyewe, Mf:kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na pia yule anayehic hapendi humpelekea mpaka kudrop darasan na kufanya vibaya, so tujitahidi kuficha hisia zetu.

 7. Anonymous

  February 22, 2013 at 12:52 pm

  Yani Dina mimi sina mtoto ila naishi na wazazi wangu haki ya nani kunaupendeleo.. Mimi nipo na dada yangu.. Anapendelewaje?? Yaani hata nijitahidi vipi lazima mama atoe kasoro.. Hawezi ongea Na mimi kama anavyo ongea na dada yangu.. Ila mimi naelewa hiyo hali hamuwezi kupendwa sawa so nina play part yangu kama mtoto.. Kuheshimu mzazi na kutenda yaliyo Mema. Na nimejiahidi kutoweka kinyongo kwa mama au hata huyu dada yangu.. I think nna moyo wa kipekee..

 8. Mama 2 (Mrs M)

  February 22, 2013 at 1:37 pm

  Bado sijajifanyia utafafiti kwa kweli kujua mtoto gani ndiyo kipenziii changu, isipokuwa napendaga tu tabia ya mtoto wangu wa kiume, kwani ana huruma, anapenda kutumwa na kujituma kuliko wawili wa kike, so najikuta napenda tabia yake. Ila kusema nani kipeeenzi sijajijua, ingawa kuna wazazi wako hivyo, hata mtoto awe na tabia mbaya vipi, kwake kama ni kipenzi chake basi ni hivyo, humwelezi kitu.

 9. Anonymous

  February 22, 2013 at 1:46 pm

  Nikweli Dina wazazi huwa wanaupendeleo kwa watoto hata kwenye familia yetu nimeona watoto wengine wakipendwa zaidi ya wengine kuna mdogo wetu wa mwisho wa kike anapendwa na mama na baba hiyo ni balaa sijaona, baba anaweza hata akaonyesha dharau ya wazi kabisa kutoka kwa dada mkubwa akaonyesha kumpendelea huyo mdogo.

 10. Anonymous

  February 22, 2013 at 11:48 pm

  hi mbona ipo sana ni vizuri mzazi asiseme yalikini akisema inaleta mtafaruku kati ya watoto!

  wazazi wengi wa sasa hivi wanathamini watoto wao hasa wale wenye kipato kikubwa na kuwasikiliza kwa kila kitu kwa sababu tu wanapesa wewe mwenzangu namie husikilizi wala kutiliwa manani na hata upendo

  kimamiii

  • wanty John

   February 25, 2013 at 11:27 am

   kidogo nina experience tofauti nadhani wazazi saa nyingine wanawapenda sana wale watoto ambao kwa ukorofi wao wameharibu maisha yao let say una kaka mlevi na asiyejishughulisha kijijini utashangaa huyo ambavyo mkituma hela nyumbani mama/baba atampatia…tena wazazi watapenda mbebe mzigo wa watoto wake na ikiwezekana hata yeye mwenyewe mumbebe despite makosa aliyonayo…..basi hao wewe au nyie mliojikwamua kimaisha mnajikuta mnamlea huyo jamaa

   mama mwemezo

 11. Anonymous

  February 23, 2013 at 12:25 pm

  DINA, umenigusa sana maisha yangu na mama yangu.
  Tangia nimekuwa nimekuwa nikidhani ni mama yangu wa kambo but hata leo ukimuuliza anasema anatupenda watoto wake wote kwa usawa, but its not real!! Mamaangu anampenda sana dadaangu, mimi ni basi tuu kwa vile pia ni mwanae.
  but kuna sababu nyingi zinasababisha hili kutokea, kama tabia za watoto, mazingira ya familia, nk.
  ILA MM NI MUATHIRIKA MKUBWA SANA WA HII KITU NA NAOMBA MUNGU ANISAIDIE NISIJE KUWAFANYIA HIVI WATOTO WANGU, MAANA IMENIUMIZA NA KUNIATHIRI MNO KATIKA MAKUZI YANGU!!

  vivien

 12. Anonymous

  February 23, 2013 at 1:12 pm

  Dina hyo ilikuwa zaman kwa waliotutangulia cz walipenda kutumia majna ya kurth, akijfungua mtoto hupewa jna la bibi yke au babu yke. So mzaz ambaye jna hilo hutoka upande wake anaona yule ni km mama yke au baba yke cz of tht name. Bt now dys no. Mimi ninao wawil lkn nawapenda wote sana. Mama Nasri / Nasra.

 13. mariam gama

  February 24, 2013 at 7:35 am

  UKWELI DADA DINA

 14. mariam gama

  February 24, 2013 at 7:38 am

  NI KWELI DADA DINA UPENDO HATA CKU MOJA HAUWEZ KUWA SAWA

 15. Anonymous

  February 24, 2013 at 9:19 am

  MAMA ANGU ANAMPENDA SANA KAKA ANGU KULIKO MM! HUWA TUNAMWITA MTOTO WA MAMA!

 16. Anonymous

  February 25, 2013 at 11:24 am

  Duh, ni kweli Dina. Mi ni wa pili kuzaliwa, mama ananipenda saaana hata mimi nalijua hilo mpk dada angu na mdogo wetu wa mwisho wa kike wanalalamika. Baba anampenda sana huyo wa mwisho, kasheshe iko kwa dada yetu yy ni neutral kwa wote.
  Lkn huwa inategemea na mazingira kama mkaka wa mwanzo alivyocomment. Mimi nilikua napendwa sana na baba zamani coz mdogo wetu wa mwisho alizaliwa mi nikiwa form 2 so kama vile mdogo nlikua mwenyewe then nilivyomaliza chuo ss mambo ya kuwa na mchumba ss hapo ndo tukaanza kukosana na mdingi mpk nilivyoolewa. Dada yetu yeye alikua hapendi shule anapenda sana arts ss na wazazi tena si unajua wanataka wakuhesabie madarasa na vyeti ndo wawe proud na aliolewa mapema sana ndo kabisaaaa wakawa kama wamemsusa!

  Nice topic Dina, duh kweli umenikumbusha mbali. Personally nina mtoto mmoja,najisubiria na mimi nione nitakuaje, Mungu nisaidie katika hili.

 17. Anonymous

  February 26, 2013 at 11:04 am

  Kwa kweli dada Dina, Umenifikisha penyewe. Mimi nina watoto wawili wa kiume wote nawapenda sana kuliko kitu chochote mmoja ana miaka 10 na mwingine 6, but first born wangu ni zaidi kwani hata wakifunga shule atakwambia haendi kwa bibi yake aniache mwenyewe. Huyu mdogo asilimia kubwa alilelewa na bibi na babu yake kipindi cha uzazi kilipoisha sikuwa na mdada, na hapo natakiwa kwenda kazini yeye hana shida isitoshe alichukua jina la babu yake sasa ndio hapo bibi na babu walipozidisha mapenzi kwa mjukuu wao. Hata akienda hana time na mimi atakwambia tu mama njoo tukae wote iwe kwa bibi au kwa mama yake mdogo. Ingawa mdogo ndiye namwangalia zaidi- Mama Joachim & Johnson

 18. Goodman Manyanya Phiri

  February 28, 2013 at 11:07 am

  Hili swali aliji kabisa; kwanini USAWA? Je usawa uliwahi kuonekana wapi duniani? Mbona vidole havipo sawa ikiwa umihimu wake pamoja ni sawa?

 19. Anonymous

  March 5, 2013 at 2:57 pm

  Dina mie sikuwahi kubaini kama nilikuwa napendwa hasa kwa kuwa sikulelewa na baba kwani alifariki nikiwa mdogo na mama sikuwahi kuishi naye kwani nililelewa na bibi na mama yangu mdogo na hata nilipokuja kukaa na mama haikuchukua muda naye alifariki soo…kujua mahaba zaidi hata kwa wanangu sijabaini mie nawaona wote sawa kiasi mama yao anashangaa!

  Baba Junior wa Magomeni

 20. Anonymous

  March 9, 2013 at 9:16 pm

  Mimi ni mama mwenye mtoto mmoja tuu (7yrs) niliachana na baba yake since she was 3 month na akawa hataki kumuhudumia kwa lolote,nikamlea mwanangu kwa shida na mateso sana kias ya kwamba mpaka sasa amekua msichana wa miaka 7 sijisikii hata kuzaa mtoto mwingine maana nahis kama bado sijampenda/kumpa mapenzi ya kutosha na nahis kama huyo atakayekuja atanifanya nipunguze mapenzi kwa huyu,so najihis kabisa kama vile sitowapa mapenzi sawa watoto wangu wengine watakao fata kama nimpendavyo huyu first born wangu kutokana na maisha niliyopitia nae maana hawa wengine watakaomfata naamini wao watazaliwa kwenye maisha ya raha na kupata kila watakalo since naishi europe kwasasa na najiweza Alhamdulilah.

 21. Anonymous

  March 20, 2013 at 3:01 pm

  Vipi Dina,Ni kweli mapenzi kwa watoto hayalingni. mimi ni mama wa watoto wawili nawapenda wote lakini mdogo ambaye ni wa kiume nampenda zaidi coz bado ni mdogo na ananijali, akiniona sipo normal huwa ni mwepesi kuniuliza mum vipi mbona your so sad today lkn mkubwa ambaye ni wa kike hana shughuli na mm ukizingatia, nawalea mwenyewe mume wangu alifariki miaka saba iliyo pita hata huyo mdg hamjui baba ake.

  Mimi kwetu nilikuwa kipenzi cha baba kwani kwetu kulikuwa na tabaka watoto wa kike ni watoto wa baba na wa kiume watoto wa mama. Na hiyo iliniathiri sana kwani baba yangu alipofariki nilipata matatizo makubwa ya kuugua vidonda vya tumbo na presha katika umri mdogo.

 22. Anonymous

  April 1, 2013 at 10:14 am

  Hi DM
  Salam Dina wazazi huwapenda watoto wao wote kwa usawa lakini muda unavyozidi kwenda watoto wakianza kuwa naufahamu wa mapenzi hapo ndio penzi la kweli kati ya mtoto na mzazi huanza kuchipua kwa maana kuwa mapenzi ni njia mbili ya kupeleka na kurudisha penzi unapompenda mtoto kama mzazi pia yeye aanatakiwa akupende mzazi wake kwa njia unayompenda
  Mzazi hawezi kumpenda mtoto asiye mpenda mzazi wake ila atatimiza majukumuu tu kama ya mzazi ila mapenzi yanakuwa hakuna

 23. Anonymous

  April 7, 2013 at 7:32 pm

  haya mambo yapo ila tunatakiwa tujitahidi sana kutokuonyesha kwa watoto wetu. Mnafahamu story ya Bwana na Bibi Isaka na wanawe Esau na Yakobo. Esau alikuwa kipenzi cha baba, Yakobo slikuwa kipenzi cha mama. Nadhani mziki wake mnaujua. Familia iliishia kuparanganyika. Yakobo nae katika watoto 12 alikuwa anampenda yusufu. Mnakumbuka ndugu zake walichomtenda kwa hili? kuna waliokuwa tayari hata kumtoa roho…. be careful guys.

 24. Eliud samwel

  April 9, 2013 at 8:46 am

  Dada dina Mimi kwa upande wangu napendwa zaidi katika familia yangu kwani mama huwa hataki hata nikae mbali nae.

 25. Beibe sadick

  April 9, 2013 at 8:54 am

  Dina 2b honest am sufferin alot wit my mum yani utafikiri sio mama yangu yani anaweza akakaa na wa2 nakuniongelea vibaya cku nikiwa nahela ananipenda nikiwa cna hela mie sie mwanae

 26. Anonymous

  April 26, 2013 at 2:41 pm

  ni kwel kabisa beibe sadick hata mama yangu ndio hivyo alivyo mapenzi yapo kwa ajili ya kitu na mimi ndio mtoaji misaada ya kila kitu namshukuru mungu kwa hilo ila mama yangu mapenzi yake yote yako kwa kaka yangu mkubwa tumezaliwa wawili na baba yangu alishafariki nikiwa na mwana na nusu so sijui mapenzi yake kwa maana nilikuwa bado mdogo sana,ila sikufichi roho huwa inaniuma sana mpk ndugu zangu wote huwa wanasema kabisa wazi na sio kwa kusema tu yako wazi na mama akiwa ananiongelea mm huwa haniongelei kwa mazuri kabisa isitoshe huwa ananiponda hata kwa vitu ambavyo sio vya kweli,nahenyeka mm namajukumu yao wote mpk watoto wa kaka yangu hajishighulishi na kazi hataki ila mpk sigara ya kuvuta mama amnunulie yaani ni kila kitu na pesa ya kuweka mfukoni kuna baadhi ya mambo mengine mpk yanatia hasira kwakweli ubaguzi wa live namshukuru mungu hatukai pamoja maana ni hasira tu yaani,sitaki kuwa kama mama yangu kwa watoto japo nina mtoto mmoja ila hata akiongezeka mwingine sitofanya hivyo hii tabia inajenga chuki kwa watoto japo kuwa sitaki kufanya ubaya wa aina yoyote ama kukata misaada ila inauma sana haya mambo yapo tena sana.

Leave a Reply