Uncategorized

OSCAR PISTORIUS ANASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMUUA MPENZI WAKE BILA KUKUSUDIA.

By  | 
Kama ulikuwa mfatiliaji mzuri sana wa michezo ya olimpiki mwaka jana 2012 utamkumbuka Oscar Pistorius.
Alikuwa mwanariadha mlemavu kutoka Afika ya kusini aliyekuwa akionekana hivyo pichani pindi alipokuwa akikimbia.Alikimbia mbio za mita 400 na kushinda medali ya dhahabu.
Tukio hilo limetokea usiku Pretoria nyumbani kwake.Oscar mwenye miaka 26 na mpezi wake Reeva Steenkamp mwenye miaka 30 walianza kudate miezi miwili iliyopita.Inasemekana mwili wa mwanadada huyo ulikutwa na matundu ya risasi kichwani kifuani na mkononi na inasemekana amewaambia polisi amemuua kwa bahati mbaya baada ya kuhisi amevamiwa na majambazi nyumbani kwake kumbe ni mpenzi wake.Inahisiwa dada labda aliingia ndani kwa lengo la kumsuprise mpenzi kwa siku ya wapendanao na yeye kuhisi amevamiwa na kushoot.
 Oscar alipokuwa akichukuliwa na polisi 
 Oscar Pistorius ni mwanamichezo mwenye ulemavu wa miguu.Hana miguu yote miwili lakini amekuwa alama ya shujaa kwa walemavu wenzake.Amekuwa akipromote michezo kwa walemavu na pia mlemavu maarufu kwa aupande wa wale walio katika michezo.

 Oscar alipata ulemavu toka akiwa mdogo baada ya kufanyiwa upasuaji wa kukatwa miguu yake.Alikatwa miguu akiwa na miezi kumi na mbili tu baada ya kuzaliwa miguu yake ikiwa haipo sawa.

12 Comments

 1. RUKY

  February 14, 2013 at 2:38 pm

  OMG INASIKITISHA MASKINI MOLA ATAMSAIDIA JAMANI SIDHANI KAMA AMEKUSUDIA NA VILE SOUTH AFRCIC PALIVYOJAA KILA AINA YA UKORA..ITAKUWA KWELI ALIDHA NI JAMBAZI….

 2. Anonymous

  February 14, 2013 at 6:06 pm

  Duuh inasikitisha sana. Haya mshangao umeleta madhara.
  Mungu amlaze panapostahiki.

 3. ULSRA

  February 14, 2013 at 8:58 pm

  So sad!! Pole kwake,nakwa family ya marehem mpenzi wake.

 4. emu-three

  February 15, 2013 at 6:22 am

  Oh kila kifo, lazima kina sababu yake…yote ni mapenzi ya mungu, ukweli utadhihiri, na haki itatendeka, vyovyote iwavyo, poleni sana waliofiwa.

 5. Anonymous

  February 15, 2013 at 6:52 am

  jamani tuwe makini tunapokwenda kufanya suprize kwa wapenzi wetu jamani, maana wengine huzani hivi, ukiona tu anashituka isivyo we jitambulishe mapemaaaaaaaaa yasikukute haya jamani Pumzika kwa aman mpenzi wa OSCAR, lakini huko uliko muombee mwenzako aachiwe muombee radhi mwenzio na aonekane hana hatia mbele za mahakimu maana tayari umemuachia msala mwenzio huo. POLE SANA OSCAR HAYO NDIO MAISHA

 6. Anonymous

  February 15, 2013 at 8:05 am

  Mmmmmmh! Hizi suprise za siku hizi noma jamani 2we tunafikiri kabla ya kutenda lkn ukweli anaujua mungu km ni kwa kukusudia au BAHATI mbaya mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi.

 7. Anonymous

  February 15, 2013 at 8:17 am

  Maskini anatia huruma,inauma dina akukusidia. me irene wa magomeni,

 8. Anonymous

  February 15, 2013 at 10:05 am

  Nina maswali mengi,ila sijui nitamuulizia wapi? kwani mpenzi wake hakupiga hata kelele? kwani alikuwa ana shoot haraka aje?

  May her soul rest in peace.

 9. emma kahere

  February 15, 2013 at 10:05 am

  Duu hizi suprise hizi.,mmh bora ujiendee kwa mpenz wako kwa taarifa tu.

 10. Anonymous

  February 15, 2013 at 11:49 am

  Jamani maskini kaka wa watu hata mimi Naamini Ni bahati Mbaya …Mungu ampiganie na Marehemu eeh Mungu umlaze mahali pema peponi tuamini kuwa siku yake ilifika na wewe Mungu ndiye umempenda zaidi na kumchukua.

 11. Mama 2 (Mrs M)

  February 15, 2013 at 11:58 am

  Sina hata la kusema ni kifo cha kusikitisha sana, kama anavyosema Anonymous hapo juu, ina maana binti hakupiga kelele? pole kwa Oscar!!

 12. Anonymous

  February 15, 2013 at 12:23 pm

  INNA LILLAH WAINNA LILLAH RAJUUN

Leave a Reply