Uncategorized

SOUL BOY….MOVIE YA KENYA.

By  | 
Katika kutazama tazama kwangu movie juzi jumapili nikakutana na movie hii ya nchini Kenya,SOUL BOY.
 Inamuhusu kijana ambae anawajibika kutekeleza masharti saba ili kuokoa nafsi ya baba yake.
 Amelala usiku na kuota ndoto mbaya sana.Asubuhi anaamka na kukuta baba yake mgonjwa sana na ameshindwa kufungua duka.Anamuuliza baba vipi baba anamjibu nimepotea.
Mtaani kuna story kuwa kuna mwanamke wa ajabu ajabu ambae ukikutana nae hasa wanaume wanapoteza mwelekeo.
 Hivyo anaingia mtaani kuhakikisha anamuokoa baba yake katika hali aliyokuwa nayo.
 Anafanya kila njia kukutana na mwanamke huyo ili aweze kumsaidia baba yake.Huko anapewa masharti saba ya kukamilisha kwa siku moja.
 
Angalia trailer yake.Movie ipo kwa lugha ya kiswahili na kiingereza.

5 Comments

 1. emma kahere

  February 27, 2013 at 7:31 am

  Unanunua wapi movie nzur kama hizi dina?,nijulishe maana namimi nataka niwe naenda kununuamaana za mitaan ukiangalia mara2 tu zina scrach.pliz nijulishe niwap wanunua.kaz njema

  • dinamariesblog

   February 27, 2013 at 10:53 am

   Nanunua library or kupewa na marafiki kama hii sijanunua nilipewa niangalie na mimi.

 2. emu-three

  February 27, 2013 at 9:07 am

  Tunashukuru mpendwa upo juu,…kwenye matawi machanga.

 3. Mama 2 (Mrs M)

  February 27, 2013 at 12:06 pm

  Story yake inaelekea inavutia.

 4. Anonymous

  February 27, 2013 at 7:23 pm

  inaonekana iko nzuri .Nimeona trailer ya movie za wenzetu mfn hiyo na Nigeria. za kwetu ziko tofauti kubwa baadh ya Film za bongo ikianza trailer zinafatia trailer nyingine na nyingine mpaka hamu inaisha.Sielewi labda kwa kuwa mie siishi bongo naletewa tu Film au ndo ziko hivyo.Unakuta move nzuri lakin ukija part two .´mmm

  Jaribu kutafuta move ya kinaigeria DRY MY TEARS ANDIKA KTK Google utaiona

Leave a Reply