Uncategorized

WALE MNAOTAKA KUTENGENEZA NYWELE KAMA ZANGU

By  | 
Baada ya kuonyesha nywele zangu nilivyoziweka siku hizi kuna maswali kibao yanakuja nimezifanyaje?
Kukaaa kwangu kimya sio kwamba sitaki kushare nilikuwa navuta time ili nikupe jibu sahihi.
Mimi binafsi hizi nywele nilikuwa natengeneza mwenyewe nyumbani kwa shampoo na conditioner.Mwanzo alinitengeneza rafiki yyangu Jajos baadae akaja kunitengeneza Musa Hussein.Kutoka hapo nikawa nimejua nini cha kufanya mwenyewe sikuwahi kwenda saloon.
Nilialikwa jana saloon inaitwa DASHING  kupata huduma yoyote nitakayotaka.DASHING ipo mikocheni kwa nyerere karibu na AZIZI hair cutting saloon ile ya wanaume.Nikiwa napata huduma wakaniambia wanaweza kuniweka fresh zaidi nywele zangu ndio wakanihudumia kama picha za mwanzo zinavyooekana.
Kuna mdada mwingine alikuja kwa mengine na nywele zake natural akashawishika kutengeneza.
Hizi sio dread ni kama rough dread na ili ziweze kukaa lazima nywele ziwe natural bila dawa ndio zinakubali zenye dawa zinateleza.Ukijua namna ya kuzitunza hizi ukioga unaweza kuzivuruga zikawa kawaida na kuzibumba tena kwa shampoo unayooshea nywele.
Kama utapenda unaweza kupita saloon hiyo ya DASHING wakakutengeneza na kupata huduma zingine.
Kwa wale mliokuwa mkiniuliza natumaini nimewajibu.Kama hujanielewa pia ruksa kuuliza.

44 Comments

 1. RUKY

  February 20, 2013 at 2:30 pm

  DINA YAANI NILIPANGA NIKUULIZE MAANA NILIONA KAMA UNA BANA NAPENDA UTUELEWESHE UNAVYO FANAY MWENYEWE NYUMBANI PLZZ

 2. Anonymous

  February 20, 2013 at 6:51 pm

  Umependeza Dina. Umeanza kuharibu ngozi yako mamaaa, sijui umeanza kutumia nini? Unazidi kuwa mweupe. Haitakupendezea, baki na rangi yako mamaa, just tunza ngozi yako ingae vizuri basi. Lv u!

  • Anonymous

   February 21, 2013 at 11:33 am

   caroligt…….

  • dinamariesblog

   February 21, 2013 at 1:01 pm

   SITUMII MKOROGO MAMA/DADA NINA MAFUTA YA MGANDO YA BABY JOHNSON NA YALE YA MAJI NIKIPAKA NGOZI YANGU INA NG'AA KAMA UNAVYONIONA.UKIONA WEUPE SOMETIMES NI PICHA SETTING ZAKE INAWEZA KUNITOA MWEUPE AU MWEUSI.

  • dinamariesblog

   February 21, 2013 at 1:10 pm

   TENA NILISEMA NITAYAONGELEA HAYA MAFUTA HATA OFISINI NAYABEBA YANASAIDIA SANA HUPAUKI PIA.Hasa sisi tunaokaa kwenye ma ac ngozi zinapauka na kukakaa maaa yanasaidia.Unaweza kuwa na kile kikopo kidogo unakibeba kwenye pochi.

 3. Anonymous

  February 20, 2013 at 7:13 pm

  Asante sana Dina, ubarikiwe kwa kuwa na roho nzuri, yaani umeniondolea tatizo kubwa lilikokuwa linanikabili la nywele! Asante sana

 4. Anonymous

  February 20, 2013 at 7:22 pm

  RANGI ZIMEKAA FRESH! BADILISHA BASI HYO SAA KILA SIKU HIYOHIYO

  • dinamariesblog

   February 21, 2013 at 1:02 pm

   SAA NINAZO 4 ILA HII NAIPENDA ZAIDI MWAYAA.

 5. Anonymous

  February 20, 2013 at 8:18 pm

  JAMANI FASHENI NYINGINE ACHENI ZIPITE SIO ZOTE ZINATUFAA HILI SHATI DINA WALAI NINGEKUTANA NA WEWE NINGEKUPITA. HALIJAKUPENDEZA NA LIMEKUFANYA MNENE. EPUKA NGUO ZITAKAZO KUFANYA MNENE, AU M2 MZIMA SN WE BADO UNAITA SO USIACHE NGUO ZIKUANGUSHE

  • Anonymous

   February 21, 2013 at 11:34 am

   umeonaeeee kuigaiga kubaya sana

 6. Anonymous

  February 21, 2013 at 12:23 am

  Hi Dina! Je unatakiwa kuosha kila cku? 2. Na mafuta gani unaweka kwa shinning? 3. Dash ipo jengo gani hapo kwa nyerere?nijuze niko natural and i like the hair style

 7. Anonymous

  February 21, 2013 at 4:06 am

  hii style inaitwaje da dina?and ni how much kufanya hvyo?

 8. Anonymous

  February 21, 2013 at 5:52 am

  asante dina pia umependeza sana

 9. Anonymous

  February 21, 2013 at 8:57 am

  Mm shda yangu ni uso.cna chunusu ila niliwah kuwa nazo hapo mwanzo wakati nasoma o level sasa nipo chup ila tatizo ni black spot.zinanikera sana na mbaya zaid uso wangu nikitumia tu sabun za kunukia hzi natoka na vpele sabun yangu kuu ni ya kipande hzi za mche.au zile za manjano coz hata za magadi zinaniunguza uso.naomba unisaidie kunimbia ni kipodoz gan kizur kitanifaa kuondoa hiz black spot na niwe soft ili ngoz ya uso wangu ipendeze?

 10. ireen steven

  February 21, 2013 at 9:07 am

  Da dina me nilikuwa naomba unisaidie dawa ya kutoa black spot uson rang yang ni maj ya kunde c mweupe wala c mweuc.pia tatizo ni sabun ya kunawia uso mana sabun zote za kunukia zinanitoa chunusi kwa ss natumia sabun ya mche au kipande.nikitumia ya magad inaniunguza..namba nisaidie kipodoz kipi kitaniondoa hzi black spot ili niwe soft na wa kuvutia zaid.

  • Anonymous

   February 21, 2013 at 10:16 am

   Irene nenda Jackz cosmetics wapo sinza madukani nadhani au tembelea blog ya shamimu zeze upate contact za Jacks wana product nzuri ila uwe na pesa mamii. mie nilikuwa na chunusi na black spot haifai nilinunua pro-active kit nilitumia in a week nikawa kama mtoto inabidi utumie kdg sana coz mie nakupagawa kwa chunusi nikawa napaka nyingiii ikaniunguza. chunusi na black spot kwishinei. siku hizi napaka mara moja kwa wiki au nasafisha tu uso baasi. imenisaidia saaaaaaaana

   DA J

 11. Anonymous

  February 21, 2013 at 10:56 am

  Eti dina nauliza sh. ngapi? kutengeneza

  • dinamariesblog

   February 21, 2013 at 1:03 pm

   MIE SIKULIPA NIKIPATA MAJIBU NTAKUFAHAMISHA.

 12. Mama 2 (Mrs M)

  February 21, 2013 at 11:38 am

  Hizo nywele nimezipenda Dina! Hata kuna siku nili comment nikakuambia acha zibaki hivyo hivyo ndogo, kumbe ndo style. Umependeza, ila kweli shirt halijakutoa kiviiiile, kuna nguo zako ukizivaa, ebwana unatoka bomba ile mbaya.

 13. Anonymous

  February 21, 2013 at 12:30 pm

  ,hiyo style me huwa siipend kabisa na wewe hata haikufai unaonekana mchafu na vikolokolo vicvyo na mbele wala nyuma badilika bhana zile wiving zinakupendeza xana ni hayo tuu

  • dinamariesblog

   February 21, 2013 at 1:05 pm

   MWAYAAA MIE NDIO NIMEJISIKIA KUWEKA UNAJUA SIWEZI KUISHI KWA KUMPENDEZA KILA MTU.NISIPOFANYA NINACHOPENDA MIMI NITAISHI KWA MWONGOZO WA KILA ANACHOSEMA MTU.ASANTE KWA USHAURI BUT KWA SASA NAJISIKIA HIVI MY DEAR.

  • RUKY

   February 21, 2013 at 5:09 pm

   DINA MBONA HUJANIJIBU NA MIMI JAMANI KWANYUMBANI ULIKUWA UNAFANYAJE NYWELE MWENYEWE?

  • Anonymous

   February 22, 2013 at 6:24 pm

   yaani katika dunia hii kuna watu siku zote kazi yao kuponda tu vivu tu unakusumbua yaani katika mia wote wanasema amependeza na syaili wewe tu umekurupuka na kuponda si ujione kuwa wewe ndio unatatizo watu kama ninyi huwa mnaniboa sana yaani saa zote kijiba cha roho badirika wewe mwenyewe si ajabu mbaya ata kuvaa au kuoga vizuri hujui
   shame on you.

  • Anonymous

   February 22, 2013 at 8:25 pm

   Hahahahaa! Watu wengine mnapeeeenda kukosoa wenzenu, nyie mmejiona?? Dina umependeza bwana.

  • Anonymous

   March 5, 2013 at 2:31 am

   Binafsi siyapendi hayo mawigi bora rasta mara kumi. Nimeipenda hiyo style yako Dina inaitwaje? Hebu nilekeze ulivyokuwa uanfanya mwenyewe nyumbani ili nami nijaribu. Unatumia mafuta na shampoo ya aina gani?

 14. Anonymous

  February 21, 2013 at 1:30 pm

  Kuna watu wana mambo. Sasa ulitaka atengeneze style unayotaka wewe? Unachekesha kwa kweli.

 15. Anonymous

  February 21, 2013 at 3:43 pm

  pole kwa mjkm dada angu!samahani niko nje ya mada nakuomba unisaidie kuulizia ni product gn naweza kutumia isiwe cream ili ning'ae na niwe soft coz mm ni mweupe ila nimefubaa ngozi yng usoni siielewi kbs na sijawahi kutumia cream huwa natumia lotion ya vaseline…….nakuomba dada unijibu kwny email yng pls(julliethaloyce@gmail.com)

 16. Anonymous

  February 21, 2013 at 9:46 pm

  wengine tupo mbali Dina, please, toa instruction jinsi ya kutengeneza mwenyewe home

 17. Anonymous

  February 22, 2013 at 7:37 am

  Dina
  Hivi ndivyo inavyotakiwa unashare na wadau wako kwani wanakupenda sana! Na hivi unawapa motisha, na wala usijali changamoto naamini nyingine zinakujenga na kukufanya ubadilike zile za kukukwaza usiumie wewe mtu maarufu sana, sisi hatujulikani labda na sisi tungekuwa tunakosolewa sana hata na hao wanokukosoa hatujui dosari zao zaidi ya kuona utumbo wanaouandika!

 18. Anonymous

  February 22, 2013 at 7:53 am

  We anony una matatizo na una tabia ya kucontrol watu. Yani Dina aache kutengeneza style anayoipenda kisa wewe huipendi, who are you kwake? Bora angekuwa mpenzi wake napo hata mpenzi hawezi kumpangia aweje. Unachekesha! Mpangie mumeo kama we ni she, na kama ni he mpangie mkeo. Grow up woman/man. Puu! Mmezidi jamani!

 19. Anonymous

  February 22, 2013 at 7:53 am

  Dina mimi nina natural ndefu cha kunana kipafu hyo style yako itanifaa mamii?

 20. Anonymous

  February 22, 2013 at 7:58 am

  Good Answer Dinna

 21. Anonymous

  February 22, 2013 at 12:11 pm

  Safi sana dina wengine kila kitu wanakijua wao npe gwala

 22. emma kahere

  February 22, 2013 at 6:07 pm

  Ua my best radio presenter in town,but now naona kama unaelekea kuwa mshaur na mwongozo in my life,kila nikionacho kwako nam napenda kukfanya hchohicho.,duu umependeza sana my dear,

 23. Anonymous

  February 24, 2013 at 3:39 pm

  Duuu dina umepungua vizuri nipe siri

 24. Anonymous

  February 25, 2013 at 11:06 am

  dinaa nampenda na maanini wengi mnampenda na mnamtumia kam role model,bt kuna wakati moyo unaweza ukapenda kitu flan bt kikawa si kizuri kwako so kumshauri pia sio mbaya,dinna unamuonekano flan hv wakidicent sasa ukianza kujicharua na hayo madred kwakweli unaonekana kabisaaaaa umevamia fani,we saizi mtu mzima act ladysh hayomambo ya swaga unaweza ukatupia maramojamoja wkend bt sio ndo ufanye staili yaaaaako,kuna kitu ambacho bado hujajitambua dina nataman ujijue thaman yako then ujijulie wat to wear n wat to put as ur personality,i thnk u will kill moooooore,huko unakoelekea sasa hv na hzo nywele mweeee,hapana aiseee.

 25. Anonymous

  February 26, 2013 at 10:26 am

  We annony hapo juu una ugonjwa wa "JELOUS SYNDROME". Pole sana. Mi mwenyewe nina miaka 36 lakini nimeshanyoa nywele zangu na kuzistyle kama Dina. Na je umeshamuona Teddy Mapunda wa Montage ltd naye amestyle hivyohivyo. Fanya kitu roho inataka. Kuna watu wana 50s lakini wana dread locks. Kipenda roho dada!

 26. Anonymous

  February 27, 2013 at 8:28 am

  Kwali izo nywele hapana na tumekuomba iyo diet yako iliokufanya upungue mbona hautupi

 27. Anonymous

  February 27, 2013 at 8:55 am

  annoymus hapo juu,unasema mwenzako ana jelous ,hujamuelewa aliye tangulia ,anachosemea sio kwamba staili ni mbaya nooo,bt kwa dinna haijampendeza.yawezekana we unapendeza coz imeendana na wewe ulivyo but kwa dina even me BIIIIIIIG NOOOOOO.

 28. Anonymous

  February 28, 2013 at 5:35 am

  Haters all of you hapo juu. Who are you kumwambia eti big no, big no kwenu kwake big yes.

 29. kaka jamal

  February 28, 2013 at 10:10 am

  mi mwenyewe kuhusu hiyo styl sijaipenda kabisaa hapo kwa dina,hapendezei mambo hayo bwana,acheni kusifia uongo bana,

 30. Anonymous

  March 5, 2013 at 9:22 am

  Una rangi nzuri Oprah wangu wa bongo. Wakubali wakatae wewe ndo Oprah wengine wanaiga vilivyo vizuri Toka kwako. Wenye Wivu watakoma we ndo unasonga mbele

 31. Anonymous

  March 8, 2013 at 2:25 pm

 32. Anonymous

  March 15, 2013 at 7:10 am

  Dina tuambie basi iyo huduma sh ngapi

Leave a Reply