Uncategorized

AMVCA WALIPOMPA TUZO YA HESHIMA MZEE OLU JACOBS!

By  | 
Juzi nilikuwa naangalia tuzo za African Magic Viewers Choice Awards.Tuzo za filamu za kazi za wasanii mbalimbali Africa ambazo ziliandaliwa Multichoice.
Kulikuwa na washindi wengi wa category mbali mbali za nyuma ya camera na mbele ya camera.
Katika category zote nilivutiwa na tuzo ya heshima iliyokwenda kwa Mzee Olu Jacobs ambae jina lake kamili ni Oludotun Jacobs.Kwao Naigeria ni mshindi wa tuzo nyingi kwa miaka yote ambayo amekuwa akicheza filamu.Ila hii ndio mimi niliishuhudia na nikaipenda.
Olu Jabobs kwenye picha akiwa na  Biola Alabi, MD, M-Net Africa
Nilipenda sana speech yake baada ya kupokea tuzo yake ya heshima.Inaleta raha kuona kuna wazee maveteran ambao walianzisha indusrty na kuifikisha hapo ilipo.Alitoa story namna walivyoanza kwa taabu na kuonekana kama wehu hatua iliyopelekea hata kupoteza marafiki.Marafiki waliwakimbia na kuwakwepa enzi hizo wakiangaika kuigiza kwa taabu.
Lakini leo hii Nollywood imekuwa inawapa heshima na wanatengeneza pesa.Wale marafiki zake waliokuwa wanamkwepa miaka hiyo leo hii ndio wanapiga simu wakimwambia awasaidie vijana wao kuingia Nollywood.Yote kwa sababu walipigana na kusimamia ndoto zao za uigizaji.”When you fall u stand up and try again,again,and again’Alisema.
Akasema tumeshuhudia watu mbali mbali wakipokea tuzo kwa kazi nyingi nyuma ya camera make up artist,script writter.Hii inamaanisha usikimbilie kuigiza, wewe kupenda uigizaji haimaanishi una kipaji cha kuigiza tafuta na ujue una kipaji gani “Know what you want and pray that when you see it, you recognize it,” huu ndio ushauri aliwapa vijana.

 Nilifurahi sana yeye kupata tuzo ya heshima kwani nimekuwa nikimuona sana katika filamu za Nigeria na navutiwa na uchezaji wake.Alisema kwa lolote analolifanya anahakikisha analifanya vizuri.Iwe ni katika kuwa baba,kulea familia yake na katika uigizaji wake.
Anatambulika kama international Actor kwani ameshacheza movie na Jean Claude Van Damme na maisha yake ya ujana ameishi sana nchini Uingereza kabla ya kuja nyumbani Nigeria.

  Amesomea mambo ya uigizaji katika chuo cha Royal Academy of Dramatic Arts kilichopo London Uingereza.Kwa miaka ya sabini alicheza tamthilia kadhaaa za huko huko Uingereza kama till death do us apart,the goodies,the ventures,barlow at large n.k
Kiufupia alianza kuigiza miaka ya sabini na mpaka sasa katika miaka yake ya 71 bado ni kivutio na yupo hot katika role zile za watu wazima.Kwa sababu ya baba yake kutokutaka asomee dramatic arts mwaka 1964 alitoroka nyumbani na kwenda nchini Uingereza kusoma.Akiwa kule ndio akamwandikia barua kumwambia baba yake kuwa yupo Uingereza.Aliporudi nyumbani Nigeria mwaka 1979 alikuta bado filamu hajizakuwa kabisa.

 Olu jacobs ana mke anaeitwa Joke Silver ambae pia ni mwigizaji wa miaka mingi.Wamejaaliwa kupata watoto wawili wa kiume.

Katika tuzo hizo Tanzania pia tulipata 
Best
Local Language Swahili –
The Ray of Hope, Sameer
Srivastava and Sanjni Srivastava
wa pili pili entertainment

Natamani sana kuona na sie tuna tuzo zetu za filamu.Nione wazee kama King Majuto,Mzee Small,marehemu Mzee Kipara,Mzee Pwagu n.k wakitunukiwa tuzo kama hizi.   

 ”When you fall u stand up and try again,again,and again’
Olu Jacobs
   
“Know what you want and pray that when you see it, you recognize it,”
Olu Jacobs

Be inspired….am inspired!

9 Comments

 1. emma kahere

  March 11, 2013 at 2:37 pm

  Mercy johnson nae amepata nimependa pia,maana safar hii anajituma sana,yan akiigiza kijijin,mjin,kichaa kote utapenda.wenze2 wako mbal sana c sijui 2nasuasua kwanin

 2. ruky

  March 11, 2013 at 8:56 pm

  daa nikweli huyu mzee ni noumer na yule aliyefariki juzi nae anasema alianzia jermani kuigiza….miaka hiyo hiyo…

 3. Anonymous

  March 11, 2013 at 9:12 pm

  huyu bwana kibogo.na mimi pia namfagilia kweli.accent yake ya kingereza chake ipo perfect kabisa.marehemu steven kanumba na yeye alikuwa anamfagilia kweli.waigizaji wa naija wengi wao kwenye interview wanajua sana kujielezea.nimeangalia interview zao nyingi,ni watu ambao wanajua kujielezea.na wengi wao wamesoma

 4. Anonymous

  March 12, 2013 at 7:19 am

  kweli dina me mwenyewe nampenda sana anavyoigiza, cjui kwann TZ atuamui kuleta tunzo za filamu bac kilimanjaro wajitaidi kuwakumbuka na wasanii wa filamu, ushauri tu, najua boc ruge akiwaamasisha ujumbe utafika

  • MOJAONE

   March 13, 2013 at 3:30 am

   Waigizaji wetu wa hapa wanashindana kwa kashifa tu lini tutaendelea.

  • MOJAONE

   March 13, 2013 at 3:33 am

   Hapa Bongo kungekua na tuzo nani star anaongoza kwa kashfa .. maana nashindwa hata kuwaelewa hawa mastaa.

 5. Anonymous

  March 12, 2013 at 11:57 am

  “Know what you want and pray that when you see it, you recognize it,” Safi sana Olu Jacobs. I will take this, thank you so much.

 6. Anonymous

  March 18, 2013 at 6:23 pm

  Hao wanafanikiwa kwa kukubali kukosolewa…wasanii wetu wanajua sana kabla ya kujua…..akipata"VEROSA" na nyumba moja toooooshaa sanaa…

 7. Anonymous

  April 12, 2013 at 8:08 am

  " when you fall, u stand up and try again, again and again.." we usually give up wen we fall but now mark dat.. thenx OLU JACOBS…………

Leave a Reply