Uncategorized

DRESS CODE:WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA!

By  | 
Kwa sasa hapa ofisini kwangu tuna run promotion ya made in Tanzania na tumekuwa tukihamasisha watanzania kupenda vya nyumbani.Na kuna ile siku ya wanawake duniani tulihamasishana kuvaa nguo za rangi ya bendera ya Tanzania wanawake kwa wanaume.Kwa hiyo kwa kuendeleza hilo nikaamua na mie katika kitchen party gala wanawake/wadada katika mavazi mtakayovaa au kushona tutumie rangi hizi za bendera ya nchi yetu.
Unajua nina hisia kuwa vazi la taifa litokane na rangi za bendera yetu.Kwa nchi yetu hii yenye makabila zaidi ya 100 hapo vazi linatoka wapi?Japo najua kamati ya vazi la taifa wanafanya kazi yao.Bendera ya nchi yetu inatuwakilisha soote bila kujali dili wala kabila i think ni wazo poa hivi.
Najaribu kuwaza tu.

 Najaribu kuangalia rangi tu za hiyo bendera na namna watu walivyozivaa.Huyu kakosa blue.Kijani,nyeusi,njano ipo.

 Blue ya bendera yetu ni blue bahari ile inayowakilisha maziwa,mito,bahari…blue ya kama hiyo skirt.

 African print….hapa tuna blue,njano,kijani…ukishashona nyeusi inaweza kuwa kiatu hivi…labda itategemea nyeusi unaiwakilishaje.

Blue,kijani,njano….

Blue,nyeusi….tumekosa kijani na njano…

 Nimejaribu tu kutafuta tafuta rangi ziweje….ila naamini wanawake wa kitanzania wanajipenda na wanajua kuvaaa manshalah.Kushona au kununua hizo nguo na kuzipangilia sijui utazipangiliaje kwa mapigo yako.Ila itapendeza sana na itafurahisha i cant wait……..

7 Comments

 1. emu-three

  March 25, 2013 at 7:40 am

  Mhh, kweli kila fani na mfanisi wake, nimekupata mpendwa tupo pamoja

 2. Anonymous

  March 25, 2013 at 8:22 am

  nimeipenda sana hii Dinnah. Christine

 3. Anonymous

  March 25, 2013 at 10:07 am

  sipati picha watu watakavyotokelezea…..

 4. Esther

  March 25, 2013 at 10:32 am

  wahooo!!!nice colour,kama nawaona wabongo watakavyo pendeza,

 5. Mama 2 (Mrs M)

  March 25, 2013 at 11:57 am

  Kwa kweli rangi zinavutia! Dina wewe ni mbunifu sana mdogo wangu! Watu watatokelezea sana!

 6. Cymah Wandelt

  March 26, 2013 at 7:36 am

  Dina mama wewe ni noma, nimependa huu ubunifu wako. Mungu akusimamie na kila kitu kiende salama. pamoja.

 7. Fred, AR

  April 27, 2013 at 6:25 pm

  Hello Dina, nimefurahi kujua wewe ni home boy. Big u mwanakwetu! Fred

Leave a Reply