Uncategorized

HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

By  | 
Mwanamke ni dada,shangazi,mama,bibi,mama mdogo,mama mkubwa,mke na mpenzi.Siku hii ya wanawake duniani tuisherehekee tukionyeshana upendo na mshikamano.Wanawake sisi wenyewe ndio tunaangushana wenyewe kwa wenyewe.Mwanamke akilianza jambo kama hajafanikiwa basi wanawake wenzie wataanza kumtia moyo na kumwambia atafika tu.Akishaanza kuonyesha mafanikio mwanamke huyo huyo ataibua vikwazo,maneno,kejeli na kila karaha za kumshusha mwanamke mwenzie.Na hili ndio adui yetu mkubwa tunapigana vita sisi kwa sisi.Tutafikaje?
 Mimi binafsi mpaka kufika hapa nimekutana na vikwazo vingi lakini nimepambana.Japo inafika wakati watu wanakuona mbaya ila lazima uwe na maamuzi hata yale yaliyo magumu.Mwanamke ukijitoa sana,ukiwa muelewa sana,ukiwa mpole sana wapo wanaokuchukulia kama dhaifu na kuona ni haki yao wewe kujitoa kwao lamiza tuwe na mipaka.Mimi naamini mwanamke UKIJIAMINI na ukiwa na IMANI utafanikisha lolote lile duniani.Mimi ni mkristu hata bwana Yesu alisema ukiwa na IMANI utaweza kuamuru mlima usogee na ukasogea.Na hili litawezekana kama ukijiamini na ukiwa na imani.Ukijiamini utatambua nguvu yako,sauti yako,uwezo wako wa kufanya lolote.Ukijiamini utajipenda na utaweza kuwapenda wengine.Ukijiamini utaweza kusimamia ndoto yako na kuakikisha unaifanyia kazi ili kuwa kweli.Ujijiamini hutanyanyasika wala kuwa jalala la wengine kutupa uchafu wao.
 Tunasafari ndefu sana lakini kwa imani tutafika tuendelee kuwa imara,shupavu,tusimamie mipaka yetu,tusimamie ndoto na malengo yetu,tusikatishwe tamaa na yoyote kubwa zaidi TUJIAMINI.

Asante kwa picha my dear brother Ahmad Michuzi a.k.a Supu.

49 Comments

 1. jack

  March 8, 2013 at 12:09 pm

  Dina umependeza,nimependa sana ulivyovaa, big up!

 2. emma kahere

  March 8, 2013 at 1:08 pm

  Mungu akujalie ufike mbali na malengo yako yatimie.ikiwezekana ufike hadi BBC au CNN.,because baada ya mama yangu mzaz unafwata wewe.u always inspire mim na najitahid sana kupita njia zako,naamin n muongozo mzur kwangu.may God be with u always,

 3. MOJAONE

  March 8, 2013 at 2:05 pm

  Nimezipenda hizo nywele na hilo Taji lake yaani hapo imekosekana nguo ya kitenge na kuwa Kiafrika zaidi.

  • dinamariesblog

   March 12, 2013 at 6:38 am

   hahahahaha basi siku ingine nitaivalia kitenge…

 4. Anonymous

  March 8, 2013 at 2:24 pm

  Well said Dina..nlpockia kwenye radio wakkucfia I was 'oooh! can't wait to c u! Umependeza mamy..unatupa moyo dada zako tupambane kike…'GENDER AGENDA..GAIN MOMENTUM'

 5. Anonymous

  March 8, 2013 at 3:01 pm

  wow..am reading and am like this lady is wise and beautiful..a symbol of a true super woman..happy women's day Dina

 6. MOJAONE

  March 8, 2013 at 3:15 pm

  Nahisi raha kuzaliwa mwanaume kwa sababu upo wewe mwanamke kwa ajili yangu, na nipo mie kwa ajili yako.

 7. Anonymous

  March 8, 2013 at 4:10 pm

  wow Dina! hizo heleni ni nzuri saaaaaaana… naziomba pls

 8. Anonymous

  March 8, 2013 at 4:30 pm

  Lov u dina…umependeza.

 9. Anonymous

  March 8, 2013 at 5:17 pm

  Asante Dina, maneno matamu kuyameza na mazuri kuyatafuna.Mimi ni mwanaume na maneno haya yatanisaidia hata kuwahimiza wanangu ambao wako over 13 yrs.Ubaarikiwe sana na endelea kukaza buti kwani bado hujafika mahali unapotaka ufikie.

  • dinamariesblog

   March 12, 2013 at 6:43 am

   Oooooh nashukuru sana sana na Mungu akujaalie wanao wakue na waweze kuwa na hekima na busara ya kuishi katika dunia hii yenye mengi mazuri na mabaya tele yatokanayo na wanadamu.Naamini nitafika tu Mungu ni Mwema!

 10. Anonymous

  March 8, 2013 at 8:00 pm

  Cute, cute, cute. Congrats Dina, keep moving ahead,even sky is not a limit

 11. ESTHER

  March 9, 2013 at 8:39 am

  dada yangu umependeza sana nimependa ulivyo vaa.naitwa Esther wa mabibo beer (windhoek)

 12. Anonymous

  March 10, 2013 at 9:13 am

  Umependeza sana dadanu,I love you so much Dina…

  • dinamariesblog

   March 12, 2013 at 6:51 am

   Thanks for loving me….nakupenda pia hahahaha utasema Dina ananipenda wakati hanijui.Hii ni kimoyo moyo!

 13. RUKY

  March 10, 2013 at 2:04 pm

  NIKWELI DINA ADUI YA MWANAMKE NI MWANAMKE MWENYEWE SO TUJIPENDE NDIYO TWAWEZA KUPENDANA…PENDEZA DINA ILE MBAYA…

 14. Anonymous

  March 10, 2013 at 3:04 pm

  Nakuombea kwa rangi hizohizo 2015 mjengoni

 15. Anonymous

  March 10, 2013 at 7:51 pm

  mmh umependeza ila hilo shati ulitakiwa kufunga vifungo vya kwenye mikono..nakushauri ufunguwe face acoount nyingine ya face book…maana mh..hiyo ingine imesha kuwa km kila mtu..

  • dinamariesblog

   March 12, 2013 at 6:46 am

   Nashukuru kwa ushauri nitafungua fun page huko face book.Kuhusu shati nilitaka kulivaa kifunky hivi sio kirasmi sanaaa.All in all thank you!

 16. Mama 2 (Mrs M)

  March 11, 2013 at 4:55 am

  Du umependeza sana Dina! kweli unaipenda Tanzania yako. Saafi sana.

 17. Anonymous

  March 11, 2013 at 1:54 pm

  Kumbe nawe chi chi em!!!!

  • dinamariesblog

   March 12, 2013 at 6:49 am

   Hivi unafahamu rangi za bendera ya nchi yako ni kijani,blue,nyeusi na njano!?

  • Anonymous

   March 12, 2013 at 8:30 am

   nafahamu sana

 18. Anonymous

  March 12, 2013 at 8:29 am

  Dina naona hii umejibu sababu umesifiwa ukikosolewa unakasirika shukuru kuna anae kutakia mema kwa kukukosoa usinune mwaya kama siyo ni siyo tuu kama ndio ni ndiooo.

  • dinamariesblog

   March 12, 2013 at 10:54 am

   NIMEWAJIBU WOOOTE kwa sababu ujumbe huu ulikuwa special na maalum kwa ajili ya siku ya wanawake.Kwa vile nimejibiwa ndio maana nimerudi na mimi kuonyesha kuwa nimefurahishwa na salamu zao pia.
   Kama comment za sifa zinakujaga nyingii sana kuliko hata za kukosolewa na sio mara zote naruddi hapa kujibu chochote.But this was special ndio maana hata wewe pia nimekujibu.Asante sana!

 19. Anonymous

  March 12, 2013 at 10:17 am

  ASANTE SANA DINA ULIVYOMJIBU HUYO ANONYMOUS HAPO JUU ASILETE SIASA HAPO TUNAZUNGUMZIA BENDERA YA NCHI . PENDEZA SANA DINA KEEP IT UP MY DEAR

 20. MOJAONE

  March 12, 2013 at 10:56 am

  Du naona mabadiliko makubwa sana hapa umeaanza kufatilia na kujibu au kuweka kument zako ktk kila coment … unatupa moyo sana tuendelee kucoment bas linabaki tatizo ktk kuchelewesha ku update hasa siku za ijumaa, jms na jpili.

 21. Anonymous

  March 12, 2013 at 11:54 am

  mwaaa dina umependeza sana upo kawaida sana dina hiyo ndio heshima ya mtanzania sio kujichubua mpaka mishipa yote inatoka nje.

  msalimie gerald hando mwambie namtafuta sana

 22. Anonymous

  March 13, 2013 at 12:03 pm

  Umependeza sana Dina,
  Says
  Mama B

 23. Anonymous

  March 14, 2013 at 7:16 pm

  Mi napenda hair style jamani inakupendeza sana. Naomba usibadilishe labda mpaka mwakani. Says bella

 24. Anonymous

  March 14, 2013 at 7:17 pm

  Mi napenda hair style jamani inakupendeza sana. Naomba usibadilishe labda mpaka mwakani. Says bella

 25. Anonymous

  March 16, 2013 at 11:25 am

  Da dna we mkali sana hasa ukiwa pele redioni mi nakwisha kabisa na kucheka yaani ni full kuenjoy

 26. Anonymous

  March 26, 2013 at 6:07 am

  luking guuudo mrembo

 27. Anonymous

  April 9, 2013 at 6:45 pm

  Dina vip kuhusu picha ya nguo uliyoonyesha umevaa spack , natamani kuiona kweli maana ilikaa vizur mnoooo!unaweza kutupa muonekano mwingine zaidi ukiwa umeivaa?

 28. Leipzig

  April 11, 2013 at 5:07 pm

  Kumbe Dina wewe ni CCMagamba

 29. Farida Ismail

  April 21, 2013 at 10:47 am

  My lovely sister you look good,Luv u so much….I wish one day to meet with you jamani me nipo Iringa Dadangu ntakupataje naomba unisaidie…

 30. Anonymous

  April 21, 2013 at 10:51 am

  U luk gud sister nakupendaje,I wish one day to meet with u jamani…mie nipo Iringa ntakupataje??

 31. Anonymous

  April 24, 2013 at 12:49 pm

  you look good,natural and beuty, its very rare now days to find tha colour, wengi wameamua kuwa wazungu wakidhani ndo uzuri. big up

Leave a Reply