Uncategorized

MSANII WA FILAMU KAJALA MASANJA AACHILIWA HURU LEO!

By  | 
Leo ndio siku hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili muigizaji Kajala iliposomwa.Katika kesi hiyo Kajala alihukumiwa miaka nane jela au kulipa faini ya milioni 13.Hivi ninavyoandika Kajala yupo nje baada ya pesa hizo kutolewa na muigizaji mwenzake Wema Sepetu.
Katika kesi hiyo ambayo Kajala hakuwahi kupata dhamana alikuwa ndani muda wote.Machi 15, mwaka jana Kajala na aliyekuwa mumewe walifikishwa mahakamani
wakikabiliwa na kosa la utakatishaji fedha haramu ambapo kwa mujibu wa
sheria kosa hilo halina dhamana.
Washtakiwa hao walikuwakabiliwa na makosa matatu, kosa la kwanza ni la kula
njama ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa kwa kuhamisha
umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.
Shtaka
la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo halali
umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007. Shitaka la tatu ni la
kutakatisha fedha ambalo walilitenda Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijua
ni kinyume cha sheria.
Kajala pichani walipocheza filamu ya DEVEL KINGDOM ya Kanumba pamoja na Noah Ramsey wa Nigeria.
Habari zaidi kesho katika movie leo na Zamaradi Mketema aliyekuwepo mahakama ya kisutu wakati hukumu hiyo ikisomwa!
Pia hongera Wema Sepetu kwa kumshika mkono msichana mwenzako dada!

18 Comments

 1. Anonymous

  March 25, 2013 at 11:11 am

  Dina usiseme ameachiliwa huru as if hakupatikana na hatia. The issue is amepatikana na hatia hivyo kuhukumia kifungo cha miaka mitano jela au faini ya milioni kumi na tatu.

 2. emma kahere

  March 25, 2013 at 11:11 am

  Wema sepe2,azidishiwe pale alipotoa.maana kutoa nimoyo

 3. Anonymous

  March 25, 2013 at 11:40 am

  Mungu amsaidie sana wema jamani kutoa ni moyo cyo utajiri, kwa hali ilivyongumu kamuokoa, ndo kajala ajue rafiki wa kweli ni yupi? hongera wema kwa moyo wako

  • Anonymous

   April 3, 2013 at 11:06 am

   BORA ANGESAIDIA WASIO JIWEZA NA WANAO HITAJI HUDUMA YA HOSPITAL NA HAWANA PESA ZA KIJITIBU. KUTOA NI MOYO MOYO GANI NA WANAJUANA VILE WANAFANYA HUO UFISADI WAO NANI ASIYE JUA HAKUNA CHA BURE SIKUHIZI.

 4. Loveness Andrew

  March 25, 2013 at 12:13 pm

  Pole kajala ndo maisha………..lakin WEMA, Mungu akuzidishie popote etakapopungukiwa wewe ni msichana mwenye roho ya kipekee sana,ni wachache ambao wangeweza kuthubutu kufanya ulichokifanya…..MUNGU AKUBARIKI WEMA SEPETU

 5. Anonymous

  March 25, 2013 at 1:14 pm

  Hongera sana wema na mungu akuzidishie hata wakisema nn ww ni shujaa na utazidishiwa zaidi

 6. Anonymous

  March 25, 2013 at 1:35 pm

  big up sana wema unarandana na jna lako kla la kheri mama najua mola atakuzdishia mara nying zaid ya hyo uliyotoa,huyo ndo WEMA sasa

 7. HabbieH

  March 25, 2013 at 1:43 pm

  Hatimae ametoka jamani . . . Pole yake kwakweli maana hayo mapito si mchezo kbs.

  Hongera zimwendee pia wema kwa kumjali mwenzie.
  Mwenyezi Mungu amjaalie zaidi.

  • Anonymous

   April 3, 2013 at 11:06 am

   WAACHE UHARAMU WAO.

 8. Anonymous

  March 25, 2013 at 10:10 pm

  Nimeona kwenye habari 13 milioni au kifungo baada ya hukumu kutoka wasanii walichangishana na wema kaendaclufata pesa zilizobakia je katoa beivgani?mkumbuke ilisha changwa pesa tayari ye kamalizia ila naimani pesa alizotoa ni nyingi m kungu ampe atamlipa wema wake na wote walio shiriki kusapoti kajala

  kimamii

  • Anonymous

   March 26, 2013 at 10:57 am

   Hakuna msanii hata mmoja aliyechangia zaidi ya Wema kuzitoa hizo hela zote yeye mwenyewe, vyombo vingine vinatoa ripoti juu juu tu kabla ya kupata habari kamili.

 9. mwanamgeni

  March 26, 2013 at 7:06 am

  big up wema u r the best mamy kla la kheri TZ 2mekukubali umerudisha furaha kwa wa2 weng sana

  • Anonymous

   April 3, 2013 at 11:08 am

   BORA UJENGE SHULE WATOTO WAPATE ELIMU SIYO HUO UPUUZI KISA KUPATA JINA DAMNNNNNNNNNN

 10. Anonymous

  March 26, 2013 at 7:08 am

  hongera sana wema Mungu akuzidishia mara mbili, na je mume wake kesi yake imefikia wapi? nisaidieni wadau

 11. Anonymous

  March 26, 2013 at 7:38 am

  Mbona mapedeshee wa bongo movie hawajasikika wapi Ray,Steve Nyerere au huwa wanamwaga hela kwa wasanii jukwaani tu?? Mwambie Zamaradi awachane hao

 12. Anonymous

  March 26, 2013 at 3:08 pm

  da big up sis wema ingawa watu wanakuchkulia vngne hla let dem say cz unajua unachkfanya hyo nkns gan unahnkana mwema kama ulvyo wema

  • Anonymous

   April 3, 2013 at 11:09 am

   anajua zitakavyo rudi.

Leave a Reply