Uncategorized

PAPA MPYA APATIKANA JANA USIKU!

By  | 
Moshi mweupe ulifuka katika mnarawa paa ya kanisa dogo la Sistina Vatican mjini Rome kuashiria papa mpya ameshapatikana.Hii ilikuwa jana usiku.
Maelfu ya watu walishangilia baada ya kupata ishara hiyo kuwa papa mpya ameshapatikana.Huku kengele za kanisa kuu la mtakatifu Petro na makanisa mengine huko Rome zilisikika.
Baada ya saa moja kupita ndio ikafahamika mrithi wa Papa Benedict wa xvi ni Askofu mkuu wa Buenos Aires nchini Argentina, Jorge Mario Bergoglio.
Papa huyu mpya amechagua jina la Papa Francis 1
Baadae alijitokeza kibarazani juu kuusalimia umati mkubwa wa watu.Papa mpya aliuomba umati huo kukaa kimyaa kwa muda kumuombea.”Naomba mniombee kwa Mungu ili anibariki”
Papa Francis amekuwa papa wa 266 mwenye miaka 76 papa wa kwanza asiyetoka barani Ulaya na watatu asiye muitaliano.

7 Comments

 1. Mama 2 (Mrs M)

  March 14, 2013 at 7:36 am

  Tunamshukuru Mungu, tunamuombea afya njema! ili aweze kuchunga Kondoo zake.

 2. Mama 2 (Mrs M)

  March 14, 2013 at 7:45 am

  Dina mdogo wangu, ulipendezaje siku ya mwanamakuka? Aisee ulipendeza mbayaaaa! haya weka picha wanaojua kunanga tuwasikie watakuwa na yapi ya kusema. kwa kweli ulipendeza siyo siri ulitokelezeeeeaaaa haswaaaa.!!!!!

 3. Anonymous

  March 14, 2013 at 9:14 am

  Tumsifu Yesu Kristo Dina,
  Kulingana na habari za BBC, Papa Francis 1 – wazazi wake ni Waitalian ila amezaliwa Argentina. Siku njema

 4. Anonymous

  March 14, 2013 at 2:49 pm

  Mungu ambariki na amuongoze vyema na aliongoze kanisa katika misingi iliyo imara.

 5. Anonymous

  March 15, 2013 at 4:29 pm

  Dina mamii, papa ni mtaliano kiasili wazazi wake walihamia Argentina ndo akazaliwa huko…

 6. Anonymous

  March 17, 2013 at 7:30 am

  Dina nimependa mtiririko wa habari juu ya Pope umeiongea kwa ufasaha sana hongera. Ni kweli wazazi wake ni Waitaliano hata uki search kwenye wikipedia yake lakini yeye ni raia wa Argentina

 7. Anonymous

  March 18, 2013 at 11:57 am

  THANX DINA…..GOD BLESS PAPA FRANCIS

Leave a Reply